Kashfa IMMIGRATION Dar Airport

Kashfa IMMIGRATION Dar Airport

Lakini hili siyo kila tom dick and harry can harass you. Kama unasafiri sana utawajua nani ni Immigration na nani ni Custom officer. Custom officer akiuliza passport ni verification tu[/COLOR]

Mzee Waga1 inaonekana unasafiri sana. GT asafiri sana kwahiyo hajui kutofautisha,au na wewe ni mojawapo wa walalamikiwa kwahiyo unawatetea wezako,Mimi hata kama sisafiri sana najua tofauti ya Immigration na Custom officer,Kubali upungufu jirekebisheni bana
 
Wow Bro unless unasafiri na airport nyingine

the situation iko hivi pale DIA

1.UNAPOSHUKA TOKA KWENYE NDEGE YAANI KWENYE ZILE NGAZI PALE KWENYE CORRIDOR UTAKUTANA NA IMMIGRATION WAWILI WATATU WANAWASAIDIA WAGENI KWENYE MAMBO YA FORMS ZA VISA AND SO ON

2.KABLA HUJAENDA KWENYE DIRISHA IMMIGRATION UTAKUTANA NA JAMAA WA IMMIGRATION (WANAKUWA MINIMUM 5 OR 6 NA UNIFORM ZA IMMIGRATIONS) NA MMOJA AU WAWILI WATU WA AFYA WATAKUULIZA VACCINATION CARD ETC

3. BAADA YA HAPO UNAKUTANA NA MKANDA WA MIZIGO USOFANYA KAZI ...
PALE NAKO UTAKUTA IMMIGRATION OFFICERS KAMA 7 HIVI WANAZUNGUKA ZUNGUKA KUOTEA WATU


4 UKIMALIZA UTAKUTANA NA CUSTOMS OFFICERS AMBAO HUWA WANASIMAMISHA WATU WEUSI NA KUWAACHIA WAZUNGU


5.KABLA HUJATOKA MLANGONI UTAKUTANA NA WENGINE KAMA 5 HIVI HAWA HUWA WANAKUWA NA MASHATI MEUPE NAO HUJIITA IMMIGRATION OFFICERS AU SIKU NYINGINE UTAKUTANA NA MWINGINE ANAJIITA USALAMA WA TAIFA ATATAKA PASSPORT YAKO na ATAKUULIZA SAME QUESTIONS ULIOULIZWA KWENYE STAGE NUMBER 2




6.KUTOKA NJE SI SABABU KUWA UKO SALAMA, UNAWEZA KUKUTANA NA MTU YOYOTE YULE ANAYEJIITA USALAMA WA TAIFA AU IMMIGRATION SASA THAT WILL ALSO DEPEND ON A DAY!!!



Kama hujakutana nao hao then utakuwa na bahati kubwa sana na inawezekana huwa unasafiri VIP mwenzetu

Be casual Mkuu and dont panic.
Hapa ni bongo and abide by the rules of the day.
Pale wote si Immigration, wako watu wengi tu na kazi zao.
Nani asiyejua kuwa siku hizi bongo ni highway ya kupitisha madawa ya kulevya?
 
Je na wale nchi jirani wanaoshukia hapo DIA na wenyewe inakuwaje??Maana na wenyewe wanasumbuliwa sana,Mfano kuna jamaa mmoja yeye kwao ni Uganda na yeye alikuwa anatokea Sweden kwa hiyo alikuwa anatumia Travel Document ya Sweden ambayo ni ya miaka 5 na anaruhusiwa kuishi kwenye hiyo nchi ya Sweden maishani yake yote,Sasa kwenye Pass yake ya Travel Document wameandika kwamba haruhusiwi kuingia Uganda,Sasa je inakuwaje mtu kama huyo anakuja kwenye nchi alafu anasumbuliwa na kuambiwa kwamba usipotoa hela tutakupeleka kwenye nchi yako ya Uganda ni kwa nini?Au kwa nini asumbuliwe kupewa Visa na aanza kuhojiwa maswali mengi?Kwanza hao Home office wana mamlaka hayo kuingilia Personal za watu??Au inakuwaje hapo??Au ndio usipotoa Rushwa ndio huna haki zaidi??

Red hiyo kaka,
yaani wewe mtu haruhusiwi kuingia hata nyumbani kwao huoni kwamba kuna sababu ya mtu huyo kuchunguzwa sana kwanini aje kwetu? Sasa hapo unatetea kitu gani? Kwanini aje kwetu sasa kama kwao wamemkana? Anakuja kufanya nini kwetu? Nafikiri hapo maafisa watakua sahihi kumsuspect mtu kama huyo na kumfanyia uchunguzi wa kina. Respect!
 
Yaani ukweli unabaki pale pale kuwa DIA haiko kwenye standards za kimataifa na bado kuna mengi ya kurekebisha.Inawezekana aliyeleta habari hii hapa ametia chumvi ama vipi lakini ukweli unabaki pale pale kuwa aliyoyaweka hapa yapo na yanatokea.
 
Nami nimepitia mara nyingi JNIA, hawa jamaa pale karibu na gate nimewahi kusikia kuwa ni askari wa kitengo cha madawa ya kulevya. Na huwa wanatarget abiria vijana na kuwauliza maswali mawili matatu, na kama hawana mashaka na abiria wanamuacha aendelee, wakiwa na mashaka wanaondoka naye kwenda kumhoji zaidi.

Lakini kwa hawa customs pale airport wengi ni waganga njaa wanaopekuliwa mizigo yao wengi ni watanzania wanaorudi kutoka ngambo lakini wageni wao haswa hawa wazungu weupe wao wanawaachia bila ya kupekua mizigo yao.
 
Rushwa,Uozo na Ufisadi. Kila mtu anastruggle kupata na guess what ambao ni victims ni watanzania wenyewe. Yaani ni balaa.
 
Ni kwa nini wasiongee na hizo International airlines zinazotua hapo ili hizo forms za visa abiria wawe wanapewa kwenye ndege kabla ya kutua?. kwanza humo airport hata pa kuzijazia hizo forms kazi kwelikweli.

Mkuu Yegomasika,

Kwa utaratibu wa sasa hivi, ukiwa mtanzania utakiwi kujaza hizo fomu tena. Unakwenda moja kwa moja na passport yako counter.

Lakini kuna jamaa wasumbufu ambao mimi nimepambana nao si chini ya mara tatu. Ukitaka kutoka, wanakwambia tupe passport yako. Niliwauliza nyie ni kina nani kwani tayari nimepitia immigration. Hawakuwa tayari kusema wanafanya kazi gani lakini ninahisi ni UWT kitengo cha madawa ya kulevya. Mimi uwa wananisumbua kwa sababu ya tabia yangu ya kunyoa kipara mara zote. Sasa wakiniangalia wanafikiri eti mimi ni muuza unga. Niliwaambia wanakosea sana kutumia kigezo cha mtu kunyoa kipara kama indication ya mtu kuwa muuza unga. Huo ni mtindo wa zamani sana na niliwaambia iko siku nitarusha ngumi kwani wanapokuuliza wewe passport yako, wengine wanakuwa wanaruhusiwa kupita bila kuulizwa. Huo nauona kama udhalilishaji ati!!!

Wabuni njia nyingine ya kukamata wabeba unga kama vile kutumia Mbwa lakini si kwa kuangalia passport za watu na kuleta usumbufu usio wa lazima.

Tiba
 
.............Wabuni njia nyingine ya kukamata wabeba unga kama vile kutumia Mbwa lakini si kwa kuangalia passport za watu na kuleta usumbufu usio wa lazima.

Tiba

Asante Tiba kwa kuliona hilo.........maana ni kutafutana ubaya tu kwa mambo wanayoyafanya pale mlangoni........si vibaya ku-check watu pale wanapowashuku.......isipokuwa approach yao si nzuri.............kama wewe ni askari polisi/UWT/Immigration na una nguo za kiraia na uko kazini kwa ajili ya kukagua...........nafikiri njia bora ni

1. Jitambulishe wewe ni nani na uombe kukagua unavyotaka kukagua
2. hawa maafisa wapewe gate lao huko ndani......maana matapeli nao wanatumia hii njia kuwahadaa wanaowasili..........

hivi vitu ni vya kawaida sana mbona.........kukaguliwa sio shida kabisa
 
nadhani in principle tushakubaliana...next stage ni kutaja majina a wahusika
 
Asante Tiba kwa kuliona hilo.........maana ni kutafutana ubaya tu kwa mambo wanayoyafanya pale mlangoni........si vibaya ku-check watu pale wanapowashuku.......isipokuwa approach yao si nzuri.............kama wewe ni askari polisi/UWT/Immigration na una nguo za kiraia na uko kazini kwa ajili ya kukagua...........nafikiri njia bora ni

1. Jitambulishe wewe ni nani na uombe kukagua unavyotaka kukagua
2. hawa maafisa wapewe gate lao huko ndani......maana matapeli nao wanatumia hii njia kuwahadaa wanaowasili..........

hivi vitu ni vya kawaida sana mbona.........kukaguliwa sio shida kabisa

usisahau target ni waafrika tuuu
 
Tangu lini Wabongo wakafanya kazi kwa ufanisi inavyostahili? Ni sawa na gwaride la watoto wa kihindi (no offence meant) ambao kila mmoja anatembea anavyotaka badala ya wote kutembea shoto kulia kwa pamoja na kwa utaratibu unaoeleweka!

Hata kama pale Airport wanahitajika maafisa wa aina mbali mbali customs, immigration, uwt, polisi etc etc lengo liwe ni kuhakikisha abiria hawapati usumbufu usio na sababu. Lakini, kinachoendelea pale ni kila mmoja wao kutaka kuonyesha yeye ni nani na ana uwezo kiasi gani wa kuweza kumchukulia hatua abiria hata kama hana alichokosea!
 
Papizo said:
Je na wale nchi jirani wanaoshukia hapo DIA na wenyewe inakuwaje??Maana na wenyewe wanasumbuliwa sana,Mfano kuna jamaa mmoja yeye kwao ni Uganda na yeye alikuwa anatokea Sweden kwa hiyo alikuwa anatumia Travel Document ya Sweden ambayo ni ya miaka 5 na anaruhusiwa kuishi kwenye hiyo nchi ya Sweden maishani yake yote,Sasa kwenye Pass yake ya Travel Document wameandika kwamba haruhusiwi kuingia Uganda,Sasa je inakuwaje mtu kama huyo anakuja kwenye nchi alafu anasumbuliwa na kuambiwa kwamba usipotoa hela tutakupeleka kwenye nchi yako ya Uganda ni kwa nini?Au kwa nini asumbuliwe kupewa Visa na aanza kuhojiwa maswali mengi?Kwanza hao Home office wana mamlaka hayo kuingilia Personal za watu??Au inakuwaje hapo??Au ndio usipotoa Rushwa ndio huna haki zaidi??


Red hiyo kaka,
yaani wewe mtu haruhusiwi kuingia hata nyumbani kwao huoni kwamba kuna sababu ya mtu huyo kuchunguzwa sana kwanini aje kwetu? Sasa hapo unatetea kitu gani? Kwanini aje kwetu sasa kama kwao wamemkana? Anakuja kufanya nini kwetu? Nafikiri hapo maafisa watakua sahihi kumsuspect mtu kama huyo na kumfanyia uchunguzi wa kina. Respect!

Huyo jamaa ni mkimbizi. Unapoomba ukimbizi ni wazi kuna kitu unakimbia ulikotoka wengi wao huwa wanasema maisha yao yako hatarini hivyo basi nchi wanayokupa ukimbizi wanakupa document yao kwa safari za nje na hawakuruhusu kwenda kule ambako watakudhuru yaani nchi uliyotoka.

Huyu jamaa kwa sababu anafahamu akiingia bongo anaweza kwenda Uganda kwa njia ya panya ndio sababu anafanya hivyo. Lakini kama Sweeden wakigundua hilo basi watamnyang'anya hati hiyo ya kusafiria na marupurupu wanayompa kwa ukimbizi wake bandia.

UK wamewanyang'anya Wazimbabwe wengi baada ya ushirikiano mzuri na SA kwani wengi walikuwa wakimbizi na wanakwenda SA then Zimbabwe, Serikali ya UK walipogundua hilo waliweka chambo SA wakiingia tu wanawanyang'anya hati za kusafiri hivyo wanakwama huo ni ujambazi wa kisasa.
 
Ndugu zangu wana JF na pia viongozi wa Serikali wanaohusika ningependa kuwataarifa kuwa kuna vitendo vinafanywa na baadhi ya Maofisa wa Polisi wa Upelelezi hapo uwanja wa Ndege wa kimataifa Wa Dares-Salaam.

Hawa Mapolisi wa kipelezi wakikuona unatoka nje ya nchi wanakungoja tu umalize kutoka nje ya uwanja na hukukamata mpaka kwa ofisi zao za kipelelezi na kuanza kukuhoji na pia kukuweka ndani kwa muda wanaotaka wewe bila ya kosa lolote na wanaanza kukusachi wakihisi labda wewe ubeba madawa ya kulevya na endepo hautakuwa na hayo madawa watakuachia lakini kwa masharti lazima ukae kwao uende Toilet mara 3 ndio waweze kukuachia.

Na wakikuachia wanavizuia vitu vyako ulivyokuja navyo toka nje ya nchi eti wanavichunguza kwa muda basi hata kama ndio wanavichunguza haitowezekana wewe wakuache na vitu vyako wavizuie tena sio kwa muda mchache inachukuwa hata mwezi mmoja wanavichunguza.

Sasa inakuwaje hivyo vitu vyako ulivyokuja navyo wavichunguze kwa huo muda wa mwezi na haswa ukizingatia umekuja na mabegi ya nguo, zawadi kwa ndugu zako simu ya mkononi, Computer ya Laptop na vitu vingine vidogo vidogo?

Ninachoshangazwa mimi inakuwaje hivyo vitu vyako vinazuia kwa muda wa mwezi eti kwa sababu ya kwa uchunguzi? Swali hili itabidi tumulize Kaimu kamishna mkuu wa Upelelzi ndugu Fred Nzoe inakuwaje watu wake waliopo hapo kiwanja cha ndege cha kimataifa kuwanyanyasa raia wema?

Kwa hivyo vitendo vyao vya kuzuia mizigo yao kwa huo muda wa mwezi mzima kwa kisingizio cha kuvichunguza hivyo vitu?

Hayo yametokea kwa rafiki wangu alie toka nje hivi karibuni kafanyia hivyo na kila akienda huko Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha hapo Dares-Salaam anazungushwa mara aambiwe kuwa Mkuu wa kituo wa Polisi hayupo njoo keshokutwa na akienda hiyo kesho kutwa hurushwa tena njoo tena kesho kutwa hii kweli ndugu zangu wana JF na Viongozi wa Serikali wanaohusika tutaendelea kweli?

Kwa fikira zangu hao wanaohusika hapo Aiport inaonyesha wanataka Rushwa wapewe pesa ili wapate kumuachia huyo Rafiki yangu vitu vyake walivyovizuia bila sababu yoyote ile ya maana. Je Ndugu Wana JF Mnalichukulia vipi hilo suala na hivi karibuni Mheshimiwa ndugu Rais wa nchi yetu JM Kikwete aliwakemea maofisa wa kuzuia rushwa wawajibike kikazi sasa ikiwa Mapolisi wetu wa kipelelezi wanamzungusha huyo rafiki yangu kumpa vitu vyake sasa inapata mwezi hawajibiki, je hao aliowakemea Ndugu Rais JM Kikwete maofisa wa kuzuia Rushwa wanafanya kazi gani?

Ningeomba mnisaidie hilo tatizo langu maoni yenu ndugu wana JF wenzangu asanteni sana.

https://www.jamiiforums.com/habari-...i-wa-upelelezi-hapo-airport-dares-salaam.html
 
kuja jamaa mmoja pale alinitaka nimtoe dollar 100 nilimrushia meneno kwa sauti ya juu ni balaa,akaondoka mwenyewe!
 
Kuna uozo mwingi sana nchi hii lakini sijui kwa nini watu hatuna tabia hata za kuiga kwa wenzetu kama kujifunza tumeshindwa kuiga pia ni vigumu? Kuhusu uchafu DIA panaongoza na watu wana kauli chafu mpaka wale security wa kawaida tu utadhani kila mtu ni mhalifu wakati mwingine wanataka hata kuwapanga watu na kuwaambia wewe kaa pale na wewe kaa hapa. Kitu ambacho ukienda Jomo Kenyata International Airport hapo kwa majirani zetu hauwezi kuviona.
 
Jamani hivi ule mlango wa choo cha wanaume umetengenezwa kweli???? Maana juzi niliingia pale hata kuufungua ilikuwa balaa. Bila msuli wa uhakika ningechemsha. Eti international airport!!!!???? Aibu tupu. Sijui hao wahusika wanafikiri kwa kutumia nyayo za miguu. Shame on them. Wajirekebishe bana! Mpaka hasira kwa jinsi inavyokera.
 
Omari Nundu anaona sawa tuuu
Cheo kapewa siyo kwa ajili ya kufanya hayooo! Hicho cheo ni asante ya jambo mkuu! Au kwa maneneo mengine ni zawadi. Hii nchi yetu itaendelea kididimia katika kila jambo ilimradi tu CCM bado iko madarakani. Nchi itabakia mogofu na ccm itakua inajigamba na kujivua gamba.
 
Back
Top Bottom