Kashfa IMMIGRATION Dar Airport | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa IMMIGRATION Dar Airport

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Game Theory, Feb 23, 2010.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,570
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Huu nadhani ni mwaka wa nne tangu tumekuwa tukizungumza na kutoa maoni kuhusu kadhia wanayopata wageni wanaoingia Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam DIA.

  Sasa hebu someni hapo chini: hii nimeikuta Michuzi blog:

  Nadhani its about time tukaacha kuongea na kuanza kuwataja kwa majina hawa jamaa.

  Kwa kuanza nadhani ni muhimu tukajua Head of Immigration pale Airport ni nani? na anasemaje kuhusu malalamiko haya?

  Wa pili ambaye anatakiwa kujibu hizi tuhuma ni Meneja wa Airport kwani pamoja na kuwa ni kituo cha kupokea wageni mbali mbali

  1. CUSTOMER SERVICE pale ni poor na inatia kinyaaa kwanza wafanyakazi ni wajeuri na nishaona wanawafokea wageni bila sababu za msingi.


  2. USAFI na UCHAFU wa mwili umeziachafu na wananuka jasho, pili whats so difficult kutengeneza escalators za kupanda kwenda juu na kushuka??


  3. UCHAFU wa JENGO: Sijapata kuona International Airport iliyochafu kama ya Dar na kama imeshindikana yale matandabui yaliojazana mle nayo kazi kuondoa? yapo makampuni ya usafi left and right je wameshindwa hata kuwapa tenda ya kufanya usafi? maana wenyewe ndio weshashindwa.


  4. CONGESTION: halafu aibu kubwa nyingine ni ile idara ya visa ambayo kusema kweli ule msomangano wa wale wageni kujaza form za visa unatisha na if anything ni kinyume cha health and safety.


  5. IMMIGRATION: Its obvious wako understaffed na wako stressed na bila kusahau hawana vifaa vya kufanyia kazi. Lakini hiyo si sababu ya kujaza watu ambao wanapotezea wageni muda pale nje...hivi kuweka watu 8 baada ya customs kuuliza wageni maswali ni nini? I mean mtu keshamalizana na Immigration kisha keshamaliza na Cutoms kwa nini anakutana na watu ambao wanaficha vitambulisho huku wanajiita Immigration officials


  6. JOTO: hivi how hard is it kutengeneza air condition mle ndani? kwa nini utawala wa DIA unawatesa watu kweli ile hali iliyo kama TANURI?


  7.BAG BELTS MBOVU: I can live with the fact kuwa best labda mota imechakaa lakini ile sehemu inayotokea mzigo kwenye ukuta yaani ni CHAFU mpaka mtu unaogopa  Mwisho napenda kuwaomba waende kutembelea Airport ya Nairobi au Kigali waone wenzao wanavyofanya kazi kwa ufanisi.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,133
  Likes Received: 27,104
  Trophy Points: 280
  si Wamewekwa na ndugu zao?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,133
  Likes Received: 27,104
  Trophy Points: 280
  mimi mwenyewe nakumbuka walinifungulia begi langu.it means wanashindwa kuweka mashine za kuscan? au zitapunguza ajira.
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  True wanaboa sana pale airport hasa for regular traveller blah blah nyingi
   
 5. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 9,591
  Likes Received: 37,817
  Trophy Points: 280
  Ni kwa nini wasiongee na hizo International airlines zinazotua hapo ili hizo forms za visa abiria wawe wanapewa kwenye ndege kabla ya kutua?. kwanza humo airport hata pa kuzijazia hizo forms kazi kwelikweli.
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,570
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  VIP nako aibu tupu ...lakini cha ajabu wao wanajengewa terminal yao naona ujenzi wa kasi unaendelea pale!
   
 7. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Jamani unapoingia Airport Dar (Wageni wanaowasili kutoka nje) na kwenda nje (Uraiani) si kweli kwamba Immigration officers wanakuwa karibu na mlango wa kutoka huu ni uongo. Wanaokuwa karibu na mlango wa kutokea ni Custom officers ambao wao ndio huwa wanapekua ulichobeba. Lawama hapa ni za nani Customs au immigration?

  Immigration kama wana swala na wewe utamalizana nao hata kabla ya kwenda kwenye mzigo wako.

  Maswala mengine ni ulalamishi usiokuwa na msingi.

  GT where are the facts?
   
 8. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Customs hata Ulaya wakikushuku wanafungua kila ulichonacho hata immigration UK wana fanya hivyo sioni ubaya hapo wakati huu wa magaidi wanaojilipua.
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,570
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Wow Bro unless unasafiri na airport nyingine

  the situation iko hivi pale DIA

  1.UNAPOSHUKA TOKA KWENYE NDEGE YAANI KWENYE ZILE NGAZI PALE KWENYE CORRIDOR UTAKUTANA NA IMMIGRATION WAWILI WATATU WANAWASAIDIA WAGENI KWENYE MAMBO YA FORMS ZA VISA AND SO ON

  2.KABLA HUJAENDA KWENYE DIRISHA IMMIGRATION UTAKUTANA NA JAMAA WA IMMIGRATION (WANAKUWA MINIMUM 5 OR 6 NA UNIFORM ZA IMMIGRATIONS) NA MMOJA AU WAWILI WATU WA AFYA WATAKUULIZA VACCINATION CARD ETC

  3. BAADA YA HAPO UNAKUTANA NA MKANDA WA MIZIGO USOFANYA KAZI ...
  PALE NAKO UTAKUTA IMMIGRATION OFFICERS KAMA 7 HIVI WANAZUNGUKA ZUNGUKA KUOTEA WATU


  4 UKIMALIZA UTAKUTANA NA CUSTOMS OFFICERS AMBAO HUWA WANASIMAMISHA WATU WEUSI NA KUWAACHIA WAZUNGU


  5.KABLA HUJATOKA MLANGONI UTAKUTANA NA WENGINE KAMA 5 HIVI HAWA HUWA WANAKUWA NA MASHATI MEUPE NAO HUJIITA IMMIGRATION OFFICERS AU SIKU NYINGINE UTAKUTANA NA MWINGINE ANAJIITA USALAMA WA TAIFA ATATAKA PASSPORT YAKO na ATAKUULIZA SAME QUESTIONS ULIOULIZWA KWENYE STAGE NUMBER 2

  6.KUTOKA NJE SI SABABU KUWA UKO SALAMA, UNAWEZA KUKUTANA NA MTU YOYOTE YULE ANAYEJIITA USALAMA WA TAIFA AU IMMIGRATION SASA THAT WILL ALSO DEPEND ON A DAY!!!  Kama hujakutana nao hao then utakuwa na bahati kubwa sana na inawezekana huwa unasafiri VIP mwenzetu
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,570
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Hii ni kweli lakini wao hufanya kazi zao kwa random na tatizo hapa si customs...tatizo hapa ni IMMIGRATION wanaozuga na kupotezea watu muda kwenye lile TANURI aka DIA
   
 11. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  GT

  Huwezi kuvuka Immigration kabla ya Customs wala huwezi kuchukua mzigo wako. Huyu jamaa hasemi ukweli mie nilikuwa Dar muda si mrefu. Wale jamaa wa Immigration kuna sehemu ya WTZ wanaorudi na wageni.

  Huwezi kuvuka uhamiaji kabla passport yako haijagongwa.
   
 12. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
   
  Pale wanakuelekeza mahali pa kwenda kwenye mstari kama wewe ni mgeni unahitaji viza au la, hawawezi kufanya lolote hao wanakuelekeza kwa kwenda wewe ndio utapambana na Immigration officer ambaye ataangalia kama documents zako ziko sawa. Sasa huyu alikuwa mbongo anakwenda kwenye mstari kusubiri zamu yake kabla ya kwenda kwenye mizigo. Passport yako ikigongwa umemalizana na watu wa uhamiaji. Finito.
   
   
  Uongo kama umekwisha gongewa passport hawawezi kukuuliza kitu huu ni uongo - Period!
   
   
  Uongo huu..


   
  GT umesafiri lini wewe? Mbona mimi nilikuwa na mizigo mingi tu na sikupata usumbufu?

   
   
  GT huyo jamaa mwongo mimi sisafiri 1st class sina hiyo pesa. Tuwalaumu kwa mengine siyo hili na mie nabisha sio Uhamiaji walio karibu na mlangoni.
   
  BTW Huyu jamaa kwani hajui sheria? Wewe tena umetoka majuu hujui sheria? Unababaishwa na procedural working routine?
   
 13. Ndjabu Da Dude

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,858
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Hamna cha ajabu hapo, hata Marekani ni hivyo hivyo tu. Utaulizwa ulienda kufanya shughuli gani wakati mtu umetokea NCHI YAKO YA KUZALIWA. Watakusimamisha customs KILA MARA Unapowasili kutoka nje, na masanduku na mabegi yako yote watafungua na kupekua: ila sema inakuwa aibu DIA kwani kila kitu wanafanya mbele ya kadamnasi ya ndugu zako na watu wengine waliokuja kupokea ndugu zao.

  Cha ajabu Wazungu wote watapita bila kubughudhiwa customs iwe Marekani au Bongo.

  That said, blame your mamma for having been born with a Black skin.
   
 14. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Mimi sioni aibu na makabrasha yangu tena hawa wako mlangoni ni customs wanaangalia mambo yao ya declaration etc. nawafungulia haraka sana ili nisipoteze muda na kujiondokea zangu.

  BTW hivi unafahamu Heathrow airport or any other UK airport kwenda nje huwezi kuondoka na £1000.00 tasilimu kama huna proof jinsi ulivyozipata? Its upon yourself to prove that you have gained that money legally and is yours.
   
 15. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,570
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Binafsi nishasimamishwa zaidi ya mara 4 na jamaa pale mlango wa kutoka

  of course hawakunifanya kitu ni maswali waliuliza lakini ni ya kero na zaidi ya hayo wako watu wengi wanasumbuliwa

  Hii issue ilishawahi kuzungwa kwenye JF ya zamani nikipata thread ntamwambia Steve aimerge maybe utapata idea na si JF tuu ni mpaka kwa michuzi watu washalalamika kuhusu usumbufu DIA

  kataa tuu lakini usumbufu jamaa wa Immigration wanao mle ndani
   
 16. a

  altaaf Senior Member

  #16
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 15, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  hapa jamani mumeongea !

  mwaka jana nilishuka pale dia nikitokea germany na mtoto wangu mwenye umri wa miaka 5 huyu ni mvulana kupitia dubai huko kote tulipewa nafasi za mwanzo kuboard kwa hawa watoto tulipofika pale dar ilikua tofauti wale jamaa hawana hata huruma tulisota pale karibu saa moja na nusu tukingoja hiyo visa mtoto alitoa nguo zote na kubakisha kaptula nguvu zilimwisha alibaki kulala chini akisulubiwa na joto hapana hata maji ya kunywa aliesema tanuri hakukosea jamaa wabadilike !
   
 17. jamadari

  jamadari JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2010
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni Kweli hao ni Vikaragosi Askari wa Ofisa Upelelezi wa Mkoa (RCO) Bw. Nzowa wanao haribu jina lake Bw Nzowa ukifika hapo Aiport nje wanakusubiri na kuanza kukuliza Maswali ya kijinga Unatoka wapi,umeishi huko nje kwa muda gani,kwanini umerudi,umeleta kitu gani kusema kweli wana usumbufu wa kila aina na ndio hao wanao haribu jina zuri la Jeshi letu la Polisi na kulipa Jeshi letu la Polisi sifa mbaya na huyo Mkuu Ofisa Upelelezi wa Mkoa (RCO) Bw. Nzowa anayo habari lakini ananyamaza tu si unajuwa Nchi yetu ilivyoharibika Kwa Rushwa,na Ufisadi. Sasa hao Polisi wa Upelelezi wa Aiport wanakusumbuwa na kukutisha utafikiri wewe ni jasusi unayetafutwa na Amerika kazi yao hao Askari kanzu wa Upelelezi kukusumbuwa utafikiri huko ulikotoka hakuna Askari kuzidi hata wao. Mimi nakusimulia hivyo kuwa yalimtokea Rafiki yangu mwaka jana ikafika mpaka wakamzuia Vitu vyake alivyotoka navyo nje ya nchi na ikafika hatuwa ya kusema atowe Pesa (Rushwa) ya shilling Laki moja ndio watampa vitu vyake ikaenda mpaka miezi sita ikawa wanampa kidogo kidogo mpaka hii leo baadhi ya vitu vyake wamevizuia hapo hapo Aiport Dares-Salaam hii kweli imenisikitisha sana kuwa hao askari wa Bw Nzowa wanawasumbuwa wananchi wasiokuwa na hatia hayo yote wa kumlaumu ni Rais wetu anawapa watu vyeo hata na elimu navyo hivyo Vyeo hawana basi Rais akipenda Mtu amtakae anampa tu Cheo sawa ampe amtakae lakini itabidi Rais amuangalie huyo Mtu anaye taka kumpa cheo amesomea nini huyo mtu anayetaka kumpa Mheshimiwa Rais wetu cheo sio kila mtu ndio ampe cheo ama kweli Waswahili Husema kuwa (Miafrıka Bwana Ndivyo Ilivyo)
   
 18. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Immigation watakusumbua kama huna passport au una scandal flani, Kikubwa watakachofanya ni kukunyang'anya passport na kukwambia uende makao makuu kujieleza kama ni ya wizi au la mengine siyo kazi yao.

  Customs watakusumbua kwa declaration mimi sioni hata kwa nini watu wasumbuliwe kama wanataka ulipie mali unazoingiza lipa sheria si zipo kwa nini kuwe na bughudha? Ni vizuri uji update na current regulations kama una wasi wasi lakini mimi sioni sababu yoyote ya returning resident kuwa na tatizo lolote. kama umebeba cellphones nyingi za kuuza lipa ushuru ndio kodi hii itaendeleza nchi usitake kuingiza bure.

  Vitu vya biashara lipia ushuru tena ni asilimia ndogo tu.
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,570
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyo mtoto sio mtanzania? Kama sio Mtanzania kwa nini hukuchukua viza kabla ya safari?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...