Kashfa IMMIGRATION Dar Airport

hapa jamani mumeongea !

mwaka jana nilishuka pale dia nikitokea germany na mtoto wangu mwenye umri wa miaka 5 huyu ni mvulana kupitia dubai huko kote tulipewa nafasi za mwanzo kuboard kwa hawa watoto tulipofika pale dar ilikua tofauti wale jamaa hawana hata huruma tulisota pale karibu saa moja na nusu tukingoja hiyo visa mtoto alitoa nguo zote na kubakisha kaptula nguvu zilimwisha alibaki kulala chini akisulubiwa na joto hapana hata maji ya kunywa aliesema tanuri hakukosea jamaa wabadilike !

Unataka nani abadirike, hali ya hewa, serikali in general, or immigration in particular? Ulalamishi mwingine bwana!
 
Kuna mdau mmoja aliandika kitu kama hiki kwenye Michuzi blog juu ya wizi pale uwanjani na ubovu wa customer service mle ndani. Watu/watoa maoni walibisha sana wakati alichosema yule jamaa japo simjui ni vya ukweli mtupu because I see it here @ DIA every single day. Mi nafikiri sie watanzania hatupendi kuambiwa ukweli tunapenda kufichiana maovu matokeo yake ni uozo kama huu. Sitashangaa watu wakibisha hata na hili. Jamani tujirekebishe.
 
aisee siku hizi kusafiri kwa anga ni usumbufu.kila mfanyakazi wa idara husika lazima atie mbwembwe..
 
Aliyepost hii thread ni mbumbumbu & kilaza ile mbaya!Si kuwa aliyosema si sahihi,la hasha!Ila nadoubt elimu au uelewa wake juu ya majukumu ya idara mbalimbali za serikali na zisizo za serikali pale airport!Mambo mengine mfano kazi za idara ya uhamiaji yanafundishwa tangu shule za msingi!sasa huyu jamaa cjui alisomea wapi!Katika yote aliyoyaandika,ni moja tu linaloihusu uhamiaji(la congestion kwenye kupata visa),ambalo kimsingi ni tatizo la udogo wa eneo lililotengwa kwa kazi hiyo na ndo maana terminal 3 inajengwa pale kipawa!Wale pale exit gate siyo immigration officials,nenda kawacheki ID zao!Masuala ya bagage belt,escalator,AC,na pumba zingine alizotapika ni za Tza Airports Authority.Usiwe mropokaji,utaonekana kilaza bure kumbe umepitapita shule.
 

Ni kweli huwa kuna watu wanauliza maswali hayo, hata mimi baada ya kumalizana na watu wa customs huku nikidhani sasa naenda kutoka kwenye geti la arrivals, nilisimamishwa na jamaa mmoja hapo mlangoni na akaomba passport yangu, nikampa akaikagua huku akiuliza ninafanya kazi gani Tanzania, na huko nilikotoka nilienda kufanya nini. Kwangu mimi alikuwa mmoja tu peke yake, na hakushughulika na mizigo yangu zaidi ya passport na maswali, then akaniruhusu. Kuna haja ya kujua hawa watu wanafanya kazi kwa ajili ya ofisi gani.

hao ni polisi wa jknia huwa wanakaa mlango wa kutokea na kuchagua watu wa kuwahoji lakini wanaangalia vijana na wachina tu wazungu wanawaogopa
 
Wow Bro unless unasafiri na airport nyingine

the situation iko hivi pale DIA

1.UNAPOSHUKA TOKA KWENYE NDEGE YAANI KWENYE ZILE NGAZI PALE KWENYE CORRIDOR UTAKUTANA NA IMMIGRATION WAWILI WATATU WANAWASAIDIA WAGENI KWENYE MAMBO YA FORMS ZA VISA AND SO ON

2.KABLA HUJAENDA KWENYE DIRISHA IMMIGRATION UTAKUTANA NA JAMAA WA IMMIGRATION (WANAKUWA MINIMUM 5 OR 6 NA UNIFORM ZA IMMIGRATIONS) NA MMOJA AU WAWILI WATU WA AFYA WATAKUULIZA VACCINATION CARD ETC

3. BAADA YA HAPO UNAKUTANA NA MKANDA WA MIZIGO USOFANYA KAZI ...
PALE NAKO UTAKUTA IMMIGRATION OFFICERS KAMA 7 HIVI WANAZUNGUKA ZUNGUKA KUOTEA WATU


4 UKIMALIZA UTAKUTANA NA CUSTOMS OFFICERS AMBAO HUWA WANASIMAMISHA WATU WEUSI NA KUWAACHIA WAZUNGU


5.KABLA HUJATOKA MLANGONI UTAKUTANA NA WENGINE KAMA 5 HIVI HAWA HUWA WANAKUWA NA MASHATI MEUPE NAO HUJIITA IMMIGRATION OFFICERS AU SIKU NYINGINE UTAKUTANA NA MWINGINE ANAJIITA USALAMA WA TAIFA ATATAKA PASSPORT YAKO na ATAKUULIZA SAME QUESTIONS ULIOULIZWA KWENYE STAGE NUMBER 2





6.KUTOKA NJE SI SABABU KUWA UKO SALAMA, UNAWEZA KUKUTANA NA MTU YOYOTE YULE ANAYEJIITA USALAMA WA TAIFA AU IMMIGRATION SASA THAT WILL ALSO DEPEND ON A DAY!!!



Kama hujakutana nao hao then utakuwa na bahati kubwa sana na inawezekana huwa unasafiri VIP mwenzetu

hapo kwenye red wale sio immagration officer ni POLISI wa jknia na wa kitengo cha nzowa.
 
Yaani ukweli unabaki pale pale kuwa DIA haiko kwenye standards za kimataifa na bado kuna mengi ya kurekebisha.Inawezekana aliyeleta habari hii hapa ametia chumvi ama vipi lakini ukweli unabaki pale pale kuwa aliyoyaweka hapa yapo na yanatokea.

Haya mambo ni kweli yanafanyika sana pale DIA hata mimi mwaka jana mwezi wa 12 jamaa walifungua bag yng ambayo ilikuwa wraping,ajabu njiani nimepita airport kama 3 Dubai,Doha na ndege transit lakin haijafunguliwa,ajabu hata nguo zng za kuvaa naulizwa kama za biashara!kingine hawa jamaa wa hapo DIA sijui wana nini yaani tofauti na wafanyakaz wa air port nyngne duniani,mtu anapofika hawana sura za tabasam wao ukiwatazama sura zao zimejaa hasira sijui wana nini,kauli zao sasa,na kuna vidada huwa vinakaa mwanzo kabisa ukishuka ngazi pale haa vile ndo utadhani vimetoka kusoma talaka,maana vinamajibu ya ajabu sana,na ni ukweli hiyo haifai kuwa International air port bado sana iko mbali sana na air port za nchi nyingne mbayaa huduma mbovu,
 
Suala siyo kutendewa,suala ni kutendewa na nani?Uhamiaji wanahusika na visa & passport tu pale airport!mambo mengine kama kuibiwa begi na ***** mwingine alioandika **** mwenzio kuna idara zinazohusika.Mbona Tza ina mataahira wengi?au ndi maana nchi inapiga marktime ,haiendelei?someni elimu ya uraia.
 
Red hiyo kaka,
yaani wewe mtu haruhusiwi kuingia hata nyumbani kwao huoni kwamba kuna sababu ya mtu huyo kuchunguzwa sana kwanini aje kwetu? Sasa hapo unatetea kitu gani? Kwanini aje kwetu sasa kama kwao wamemkana? Anakuja kufanya nini kwetu? Nafikiri hapo maafisa watakua sahihi kumsuspect mtu kama huyo na kumfanyia uchunguzi wa kina. Respect!
Hilo ni jambo la kawaida sana tu, na ni kwa wakimbizi ambao wanakimbia nchi zao na kuomba uhifadhi hasa hasa nchi za ulaya - hivyo wanapewa pasi ya ukimbizi inayowaruhusu kusafiri lakini hawaruhusiwi kurudi nchini kwao na hilo linakuwa limeandikwa katika pasi zao.
 
Unataka nani abadirike, hali ya hewa, serikali in general, or immigration in particular? Ulalamishi mwingine bwana!

Sio ulalamishi. Mimi mwenyewe nina mtoto hajafikisha miaka 5 na ninaposafiri mara nyingi huwa tunapita Nairobi yaani pale hata ukienda msalani utawakuta wale kina dada wanaoshughulikia usafi wako standby na mara zote wako tayari kukusaidia. Ingawa Jomo Kenyata wananikera kwa udokozi katika mizigo "registered" lakini wanajitahidi sana kwa mambo mengine.
 
Jamani,tunaojua shughuli zinazofanyika airport tuwasaidie wenzetu hawa!Swissport wanahusika na boarding passes,baggages & passangers care to the board(plane),Uhamiaji ni visa & passport control,Tza Airport Authority wanahusika na security & airport building care n.k,kuna kampuni ya usafi,kuna porters n.k!Kifupi,hapo kuna taasisi chungu nzima!Sasa huyu mshamba kila alilotendewa airport,anadhani ni uhamiaji tu.Uhamiaji makao yao makuu yako Kurasini,pale airport wana kisehemu tu!
 
Back
Top Bottom