Karma imelipa tayari.

Polis wa bongo ni vichwa vigumu, wakati nipo taasis kubwa ya ulinzi na usalama nchini wakati huo tulikuwa tukionywa sana kujipendekeza kwa wanasiasa

Mwanasiasa atakutuma ufanye jambo fulani, likiharibika anakukana kesi unabeba wewe kama wewe
Na mahakaman cheo chako kinawekwa pembeni, unashitakiwa wewe
 
Wakati akifanya haya yote yupo wa/aliyekuwa nyuma yake,je nao/naye amekumbwa na karma?.Na kama angedhibitiwa tangu wakati wa tukio la Nape si labda huenda huyo Mfanyabiashara angenusurika?.Leo tunashangilia karma na je huyo Marehemu naye alipatwa na karma ya nani?.
Wachina alikuwa akiwatishia kuwabambikia kodi anawakamata anawasweka ndani siku moja mbili akiwaachia wanampelekea mamilion amewatesa wengi
 
Mkuu sijui nisemeje ila hakuna uuaji mzuri wacha aende jela huyo mnyama ambae afahi kuishi na binadamu yule dogo walichomfanyia hata hiyo hukumu ni ndogo.
Kwa nini asingenyongwa kbs kenge huyo? Nilidhani ni miongoni mwa wale wawili waliohukumiwa kitanzi!
 
Ivi huwa hawana mahakama zao kama ilivyo kwa JWTZ?
Huko huwa wanapelekwa wale walioikosea Serikali.

Wananchi wakikosewa wanapelekwa mahakama za wananchi ambazo kuna loopholes nyingi za kuchomoka.
 
Haya hawayaelewi kabisa Mkuu, Katika taasisi ambazo zinapaswa ziwe mbali na wanasiasa ni Hizi za Ulinzi lakini ilo hawalioni kabisa.
 
Safi sana,hata hawa wengine wanaoteka watu na kuwaua katika awamu hii nao watatafutwa na kushitakiwa na kuhukumiwa.

Ukiua kwa upanga utauawa kwa upanga,ni suala la muda tu haki ya Watanzania walioumizwa na kudhulumiwa haki yao ya kuishi itapatikana, iwe ni kwa jasho au kwa damu, lazima watu wajue na kujifunza kuishi kwa kuheshimiana,madaraka na vyeo ni vya muda tu.

Kuna wengine wanalazimishwa kufanya uovu,wito wangu kwenu,tunzeni ushahidi maana mkija kuhojiwa mkaonekana hamna ushihidi wowote nyinyi ndio mtakaobeba hiyo hukumu.
 
View attachment 3380802
Ilianza hivi


View attachment 3380803
Ikaja hapa

View attachment 3380806
End .


Lesson kila ubaya utalipwa
Mwigulu Nchemba aliwahi kukanusha kwamba Jeshi la Polisi halina mwajiliwa mwenye juna hilo wala huyo mtu aliye pichani siyo Polisi.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…