Kwa mtazamo wangu msululu wa lawama unakwenda kama ifuatavyo
1.Serikali ndio wakulaumiwa kwa kuendeleza mtindo "kuzifuga" kashfa, suala kama la Richmond(mfano) wabunge wetu walishafanya kazi yao kwenye tume ya Mwakyembe na tunasubili matekelezo ya maagizo yao ila mpaka leo waziri mkuu anakuja bungeni na kutwambia bado linashughulikiwa, linashughulikiwa mpaka lini? Je hii ndio kasi mpya tulioahidiwa? Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wana jukumu la kulifuatilia suala hili mpaka mwisho wake,au waliache tu hewani wakati maagizo yao hayajafanyiwa kazi?
2.Wabunge wameonyesha kutokua makini kwenye majukumu yao ya kuiwajibisha serikali na wachache wamekili hili,wanauma na kupuliza! Nasema wanauma na kupuliza kwakua wanashindwa kuibana serikali moja kwa moja yaani kua consistent kwasababu ya maslahi ya kichama, serikali inapoona inazidiwa, Makamba(The dentist) anawaita wabunge wa CCM wanakaa na kutoka na msimamo ambao utaipa ahueni serikali kwa maana nyingine ni kuling'oa meno bunge! nahapo ndipo marktime zinapoanza (kama ulivosema MMMK)
3.Watanzania ambao tunajua kabisa kua na wabunge wengi wa chama kimoja ni kansa mbaya kwa Bunge na ustawi wetu kwa ujumla lakini tunaendelea kukichagua chama hichohicho kinachotudidimiza kwenye lindi la ufisadi,kutokuwajibika,kulindana na mengine mengi mabaya. Tunauza shahada zetu za kura,tunapokea takrima za pilau t-shirt na pesa uchwara kumpa mtu dhamana ya mustakabali wetu kwa miaka 5 ijayo(hii ni aibu) huu ni umaskini wa kifedha ama ni umaskini wa fikra?
HII NI AIBU KUBWA! HAKUNA ANAETEKELEZA WAJIBU WAKE
MWANANCHI WAJIBISHA MBUNGE WAJIBISHA SERIKALI WAJIBIKA KWA MWANANCHI.