Nkingwamh
JF-Expert Member
- Jan 6, 2018
- 290
- 210
- Thread starter
- #201
Habari ndugu IpanangaMkuu nina shida ya meno kufa ganzi nikinywa soda aina ya pepis na nikitumia dawa ya meno ile white dent nyeupe shida ni nini?
Bila kujali jinsi hali hiyo itokeavyo kama ulivyoeleza. Iwe kwa kunywa soda aina yoyote au dawa ya meno aina Fulani.
Kimsingi tatizo la meno kufa ganzi Mara nyingi hua likijitokeza hasa pale Mtu. anapotumia mswaki hadi zile blashe zake zinaisha ama kua ngumu.
Mswaki uliofikia hali hiyo ni hatari kwa afya ya meno, kwani ule ugumu, unaposwaki huenda kuondoa ile Lea ya nje ya jino.
Na mara nyingi hua inatokea hasa kwenye shingo la jino. Pale ambapo ufizi unaanzia.
Sehemu hii pamoja na Lea ya ndani ya jino.hua kuna vitundu vidogo vidogo hujitokeza ambapo hua vinaruhusu kitu chochote chenye tindi Kali. Ubaridi pamoja na umoto kupenya kiurahisi na kusababisha hali ya uganzi.
Lakini pia hali hii hua wakitokewa watu ambao hua wakilala huku wakisaga meno yao, tendo hilo hua likisababisha kuondoa ile Lea ya nje ya jino(enamel)
Lakini pamoja na hayo hali hiyo pia hua ikiwatokea watu ambao meno yao hua hayako imara hasa kutokana na upungufu wa madini ya casium.
Bwana ipananga ninakushauri fika hospitali ili uonane na wataalam wa meno ili wakufanyie uchunguzi.
Humu unaweza kuelekezwa dawa nyingi sana.
Lakini kumbuka kadiri unavyozidi kuelekezwa dawa bila uchunguzi wa kitaalam ndivyo unavyozidi kuchrlewa.
Ganzi inapotokea kwenye meno ni ishala inayoonyesha kuna vitu vina pita moja kwa moja hadi ndani.
Kwa hiyo wahi matibabu haraka kwa wataalam wa eneo hilo la meno.
Kabla hayajaathiriwa zaidi na kuitajika kung'olewa.