Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Habari Dada
Pia pole kwa tatizo hilo. tatizo hilo kwa kweli ni wengi wanahangaika nalo kutokana na kuona aibu.

Sababu ya tatizo hili ikiwa ni wa awali(acute) Mara nyingi huwa hauna sababu maalum. Lakini kuna wakati huweza kusababishwa na upataji wa choo kigumu Mara kwa Mara.

Lakini kama tatizo ni lamuda mrefu kidogo,( chronic) magonjwa kama kaswende TB Saratani Na madonda ya utumbo (chroho'ns disease) ni lazima yachunguzwe.

Kama tatizo sio lamuda sana Fanya kama ifuatavyo. Nunua Tablets Metronidazole 2x3x5/7 Pia nunua Caps Amoxilin 2x3x5/7 Pia nunua Tablets Paracetamol 2x3x5/7.
Hizo zote uwe ukimeza kabla kidogo ya kula. Baada ya kumaliza doese hizo, Nenda tena kanunue dawa hizo hizo.

Lakini awamu hii Metronidazole usimeze kwa mdomo.
Fanya hivi asubuhi ukiamka meza Caps Amoxilin pamoja na paracetamol.Kisha chukua maji moto moto kiasi pamoja na kitambaa safi.
Nenda bafuni uwe unakilowesha kitambaa maji hayo halafu unakibandika eneo la haja(Unyeo) kisha kandamiza kiasi ubaki umeshikilia kama. Dakika 2 kisha chovesha tena kitambaa hicho rudia hivyo kama Dakika kumi hivi.

Baada ya hapo chukua Tabs Metronidazole tembe mbili zisage vizuri kisha.
Unga huo ingiza ndani ya unyeo hasa eneo lile lililo na mchubuko.

Fanya hivyo kutwa Mara tatu na uwendelee kumeza Amoxilin na paracetamol 2x3.
Endelea na zoezi hilo muda wa siku tano, huku ukimeza hizo dawa.

UZINDUSHI:
Unapofanya hivyo hakikisha kama ulikua umeshikwa haja jihudumie kwanza swala hilo. Kisha jisafishe vizuri kabisa.
Baada ya hapo endelea na zoezi hilo.
Jingine ni kwamba, hakikisha ukisha weka jitahidi ukae mda mrefu kidogo bila kwenda haja ili dawa inyonywe
Jingine hakikisha umalizapo kujihudumia haja kubwa hakikisha umejisafisha vizuri na kujikausha vyema
Jingine kwakua tuna hitaji mchubuko upone inabidi mda wote wa dawa uwe ukijikinga na kupata haja ngumu kwa kunywa maji matamu tamu( Juice) na kula chakula ambacho ni rahisi kulainika.
Jingine hakikisha kitambaa kila umalizapo shuuri hiyo kifue vizuri kabla ya kukitumia tena.

Fanya hivyo kisha baada ya kumaliza siku tano ya zoezi hilo. Ulete mrejesho
Kama bado tutakupatia ushauri wa vipimo kubaini nilioeleza huko juu.
Asante na karibu tena.
Sawa Dr. Nitafanya ivyo kama ulivyonielekeza....japo kipindi cha nyuma nilipewa dawa hali ikaisha nikasahau kabisa ila imeludi tena....nilipewa za kumeza tu.
 
Habari bwana Wajad.
Kabla ya kukupatia Maelezo Naomba nijue hicho kidonda kina mda gani na kilianza vipi.
Marekebisho:
Anasema kilianza alama nyeusi kama baka mithili ya mahali palipoungua au kama penye ugonjwa was ngozi au fangasi na palikuwa na ngozi ngumu sana .
 
Za leo dokta.
Mama yangu anasumbuliwa sana na mikono kuwaka moto mida ya usiku akiwa ametulia au kulaka.... Tatizo ili lina karibu miaka 2 sasa. Sehem hiyo ni kuanzia kwenye kiwiko kuelekea vidoleni na cha kushangaza ni mikono tu.

Si mkaaji anapenda kujishungulisha na kazi ndogondogo za hapa na pale za nyumbani...kaenda hosp akapata dawa hali ipo vilevile, akatumia dawa za kuchua hali bado, akatumia dawa za majani hali bado pia.

NB. Dawa hizo huwa inapunguza tu Makali na c kupona ila usiku akiwa katulia inawaka moto sana na si mchana namnukuu.
Kwa sasa ana miaka 52
 
Marekebisho:
Anasema kilianza alama nyeusi kama baka mithili ya mahali palipoungua au kama penye ugonjwa was ngozi au fangasi na palikuwa na ngozi ngumu sana .
Habari ndugu.
Kwanza kabisa nikupe pole kwa kusubiri kwa Masaa mengi, nikwambietu kwamba nahii ni kutokana na majukumu ya kikazi zaidi.
Lakini kwaupande wa swali la msingi. Ni kwamba majibu ninaweza kua nayo mengi sana. Pengine majibu hayo yakawa ni ya kukuchanganya.
Kwa hiyo Ni naomba ndugu yako huyo mpeleke HSPL ama Maabara yoyote kwanza kisha mpimishe kipimo hiki. RPR au VDRL ili tujue antibodies ya Triponemo katika damu yake.
Hili litatusaidia sana ndugu yangu pakuanzia.

Kwani tatizo hilo ni Dalili ya Magonjwa hatari.
Kwa hiyo kipimo hicho ni sehemu ya mwanzotu ya kufuatilia tatizo hilo. Asante
 
Ukinyonywa uume na mwanamke mwenye virusi kwa sec 15 je,utapata maambukizi?
Habari bwana Idrissi.
Kwanza nikupe hongera kwa ujasiri mkubwa wa kuleta swali ambalo kwa namna moja ama nyingine, majibu yake yatakua ni elimu kwa Jamii.

Ndugu Idrissi mbali na kujua ukinyonywa uume na mwanamke mwenye Virusi, ingawa hujasema ni virusi gani, lakini najua bila shaka utakua ukimaanisha VVU kwa sec 15 Je utapata maambukizi!
Ni kwamba wewe pamoja na mpenzi wako mwenye virusi wote mna haki sawa ya kuishi, kwa afya ilio bora.
Kwa hiyo nikwambietu kwamba usijilinde wewe peke yako. Bali pia mlinde na mpenzi wako huyo mwenye virusi. Ziko kanuni za kuishi na mpenzi wako akiwa na virusi.ili wote wawili mue na afya bora Yani wewe usiambukizwe na yeye aendelee kua na afya bora.
Kanuni hizo hutolewa crinic.

Lakini hapa nitaeleza kwauchatu kwa faida pia kwa Jamii.

Swala la kunyonywa uume sio salama kabisa kiafya, kwani wakati ukinyonywa uume. Sidhani kama utakua umevaa condom. Na swala hili wengi hujisahau na hatimae kuunga mkono hoja kua condom hazizuii maambukizi.
Kumbe watu wanasahau kua wanaifanya condom kua ni kifaa cha mwisho. Baada ya kua wamesha ambukizwa.

Ninayasema haya kwa sababu, Ulimi ni ogani kama ogani zingine.
Na ogani hiyo inaweza kujeruhiwa kama ambayo huweza kujeruhiwa viungo vingine.
1 Kama Ulimi na Mdomo Vya mwanamke Vina michubuko na Uume wako ukawa na michubuko ni rahisi sana kupata maambukizi ya VVU. Ingawa mate pia hua na kitu lisozime ambayo ni kinga.
HUA KAMA HIVI.
Kile kitendo cha kuingiza uume na kuutoa (kuingiza na kutoa,kuingia na kutoa) kwenye mdomo ni lazima na meno hua yanagusa ngozi ya uume ingawa ni kwa mbali.
Meno yanapogusa gusa ngozi ya uume. Husababisha kuchubua tumichubuko twa zamani tulitoko kwenye uume. Tulitopona kutokana na vipele au chunusi tukawa wazi.

Kitendo hicho cha kua wazi hatari inaanzia hapo.
Hapo kama mdomo na Ulimi vitakua na vidonda au michubuko.
Na uume nao utaweza kuvikwangua vidonda na michubuko hizo kwa kitendo kile cha kuingiza na kutoa.
Hapo na vidonda ama michubuko zilizoko mdomoni vitakua wazi pia, na pengine zitakua ziki bleed ingawa si sana kutokana na lisozime ilioko kwenye mate.

Lakini hapo mate yalioko mdomoni yakichanganikana na damu iliotoka kwenye michubuko yatasaidia urahisi wa uambukizaji.
Hapo ninamaanisha Yale mate mate yenye chembe za damu yakaingia kwenye michubuko ilioko kwenye uume Husababisha maambukizi kwa asilimia mia.

Ndugu idrissi Hapo utakua katika hatari kubwa ya kuambukizya VVU.

2 MAAMBUKIZI MENGINE
Kuna maambukizi mengine kutokana na Bacteria. Unaweza kuyapata maambukizi hayo ni kama.
Maambukizi ya bacteria aina ya triponemo bacteria huyu ana madhara makubwa. Na kwa bahati mbaya madhara mengine ya bacteria hii huweza jitokeza kwa muda mrefu.
Hata wakati mwingine ulemavu wa viungo au magonjwa ya akili wakati mwingine chanzo iko hapa.
Bwana idrissi usikimbilie kujilinda wewe.
Na mpenzi mwenye virusi nae ana haki ya kuishi. Unapokua nae siotu uwe makini asikuambukize Bali hata wewe unapasa uwe makini usimwambukize magonjwa mengine ya zinaa.
Kwani atapokua na magonjwa mengine kwake ni rahisi sana kuathirika kwakua. Wakati kama huu kinga zake zitakua busy kukabiliana VVU na pengine zinaweza kua zishapungua. Kutokana na pigano la kila siku.
Kati ya kinga zake VVU.

Lakini pia Usimfanyishe sex muda mrefu kwani kufanya hivyo kutamsababishia kumchosha mwili na kuanza kukonda. Na hiyo ni kutokana na tendo hilo kutumia nguvu kubwa.
Kwakua nguvu hutokana na glucose ilioko mwilini mwake. Na kwa wakati kama huu glucose huhirajika sana mwilini mwa mtu kama huyu. Kwakua ndio hufanya kazi katika seli kwa kuzikarabati.
Zile zilizo haribiwa zaidi na VVU kuundwa upya. Kutegemea na uharibifu uliopo.

Kwa hiyo kama utamfanyisha sex sana Hapo itabidi itumike glucose ilio hifadhiwa ili kumfanya awe na nguvu kwenye tendo hilo.
Na hiyo ilio hifadhiwa ikiisha huanza kuchukuliwa glucose ilioko kwenye misuli zake. Hapo ndio utaona anaanza kukonda kwa haraka.
Lakini pia usikae na hofu ya kua Pengine umeambukizwa, bila kupima nenda kapime. Ujue afya yako. Na pia jenga mazoa Mara kwa Mara kua unapima Afya ya mwili.
Ni matumaini yangu utakua umeelimika na umma kwa ujumla.
Asante nakaribu tena.

Sawa Dr. Nitafanya ivyo kama ulivyonielekeza....japo kipindi cha nyuma nilipewa dawa hali ikaisha nikasahau kabisa ila imeludi tena....nilipewa za kumeza tu.
 
Za leo dokta.
Mama yangu anasumbuliwa sana na mikono kuwaka moto mida ya usiku akiwa ametulia au kulaka.... Tatizo ili lina karibu miaka 2 sasa. Sehem hiyo ni kuanzia kwenye kiwiko kuelekea vidoleni na cha kushangaza ni mikono tu.

Si mkaaji anapenda kujishungulisha na kazi ndogondogo za hapa na pale za nyumbani...kaenda hosp akapata dawa hali ipo vilevile, akatumia dawa za kuchua hali bado, akatumia dawa za majani hali bado pia.

NB. Dawa hizo huwa inapunguza tu Makali na c kupona ila usiku akiwa katulia inawaka moto sana na si mchana namnukuu.
Kwa sasa ana miaka 52
Njema kabisa machuchu.
Pole sana. Pia mpe pole mama.
Ninge penda nikuulize!
Je Mama hua anatatizo la kisukari?
 
Asante sana Mkuu. Tunaendelea kujifunza toka kwako. Big up.
Thank you
Habari Ndugu.
Hali kama hiyo ikiwa haiambatani na dalili zingine.
Huenda ukawa unasumbuliwa na mgonjwa ya fizi.

Kuna aina kubwa mbili za mgonjwa ya fizi ambayo ni
1. Gingivitis
2. Periodontitis
Ninakushauri ukaonane na daktari wa meno kwa uchunguzi zaidi.
Mimi sipendi kukwambia unaupungufu kua unaupungufu wa vitamin C.
Kwa maisha ya kawaida sio rahisi kua na upungufu namna hiyo
Kwanza tuanze na sababu ambazo ni tishio ndio tuje kumalizia na mambo ya vitamin.
 
Hii ni kwa sababu nadhalia ilioko sasa juu ya tatizo hilo ni tofauti na zamani. Kwa sasa tatizo hili ukifatiria kwa kina ni kwamba haliishi Bali linapewa likizo ya miezi kadhaa then linarudi kazini. Hali hii inasababishwa na baadhi ya madactari kwa ujumla U.T.I pamoja na homa sio ugonjwa Bali ni alarm inayopiga kuashiria kuna tatizo limeingia mwilini.Na kiukweli Doctor ndie anatakiwa aamue mgongwa upime nini baada ya Kupokea Maelezo toka kwa mgonjwa Sasa utakuta baadhi ya madaktari baada ya kupokea maelezo ya awalitu pale pale anakuandikia KAPIME MKOJO akipima majibu yatayopatikana hapo unategemea yatakua ni nini kama sio UTI. Kwanza tambua Maana ya UTI.neno hili ni kifupi cha maneno ya kingereza yasemayo URINE TRAC INFECTION yaani maambukizi katika njia ya mkojo na tatizo hili ni tatizo la Pili baada ya tatizo halisi. Na unapokutwa na tatizo hili Daktari anatakiwa akuandikie vipimo vingine vya kufuatiria tatizo ambalo limesababisha kuweka maambukizi kwenye nja ya mkojo au kwamsemo huu ( huwezi kuzibua mfereji wa maji taka bila ya kuhamasisha watu wasitupe taka ngumu chooni)kutibu UTI pekee nisawa na kusafisha taka kwenye mfereji wa maji taka wakati muweka taka hizo yupo na anaendelea kuweka.Kufanya hivyo ni sawa na kujenga ofisi ya mkusanya pesa nyumbani kwako. Sasa ninakuamsha kutoka katika usingizi mzito ulionao unapopima na kukutwa na UTI amua mwenyewe kupima vipimo vingine vya Damu mbali na malaria tatizo utalolikuta hapo hilo ndio chanzo cha kuharibu mfumo wa mkojo wako tibia hilo kwa ufasaha maambukizi katika njia hiyo Nayo yataondoka
Vipimo vingine vya damu vipi mkuu vinavyohusiana na uti
 
Vipimo vingine vya damu vipi mkuu vinavyohusiana na uti
Kwanza habari ndugu.
Ni kwamba sijakuambia kuna vipimo vya damu vinavyo Pima UTI
Nilichosema ni kwamba kama umepima urine ukakutwa na UTI
Fanya ukapime vipimo vya damu. Kuchunguza magonjwa mengine mbali na malaria.
Nikiwa na maana tatizo hilo la UTI kama limesababishwa Pengine na Magonjwa ya zinaa Haliwezi kwisha.! Kwa hiyo ndugu sijasema upime Damu kuchunguza UTI.
Hakuna kipimo cha Damu kuchunguza UTI.
UTI huchunguzwa kupitia Urine.
 
Kama kichwa kinavyosema hapo nakaribisha maswali yanayo husu afya

Naomba kufahamu kwa undani zaidi, madhara kwa mtoto anapozaliwa na kunywa yale "maji machafu"..... in layman's language... 'Maji machafu'... Maji hayo ni nini???? Nini madhara anayoyapata mtoto kiafya, kiakili, na mambo ya ziada ambayo kitaalamu unaweza kuyazungumzia. Nini cha kufanya kuweza kuweza kuzuia hali hii....

Asante.
 
Kama kichwa kinavyosema hapo nakaribisha maswali yanayo husu afya
Naomba shule ya huu ugonjwa/hali inayoitwa Autism. Ni ugonjwa gani huu? unasababishwa na nini? Madhara ya ugonjwa huu? Ushauri wa kitaalamu kuhusiana na malezi, makuzi na taaluma kwa watoto wenye hali hii na mengineyo muhimu unayoweza kutuelimisha.

Asante
 
Sawa dr nimekuelewa japo mimi sikuwa nafahamu huy bint kama ameathirika pia kuhusu michubuko kwa kumbukumbu zangu zinavynituma sikupata wala kuwa nayo pia leo ni siku ya 17 tangu tukio limetkea nimetest negative nimeambiwa nirudi mwezi ujao ...ila hofu yangu ipo kwake tu kama alikua anayo au la
Note:vijana tujihadhari ukimwi upo mateso ninayopata mimi kwa mawazo hayapimiki
 
Pole sana Mungu atakusaidia.
 
Naomba kufahamu kwa undani zaidi, madhara ya mtoto anapozaliwa na kunywa yale "maji machafu"..... in layman's language... 'Maji machafu'... Maji hayo ni nini???? Nini madhara anayoyapata mtoto kiafya, kiakili, na mambo ya ziada ambayo kitaalamu unaweza kuyazungumzia. Nini cha kufanya kuweza kuweza kuzuia hali hii....

Asante.
Habari msweet
Kwanza kabla ya kujua madhara.
Ningependa tumjue kwanza mtoto alietumboni.
Anaishije huko, na kwanini anakua!.
Mama au Dada anapo bahatika kushika mimba. Kutoka siku ya kwanza hadi wiki ya 8, ile mimba hutambuliwa kama "Embryo" yaani humaanisha 'kukua ndani'.
Wakati kama huu kwa yule mama mjamzito hujulikana kama Embryonic Period. Huhusishwa na kuumbwa kwa mifumo muhimu ya viungo vya mwili.
Kwanzia wiki ya 8 hadi mwisho wa Mimba, kiumbe hicho hutambuliwa kama Fetus(kijusi) au kwa lugha yetu ni mwana ambae hajazaliwa. Na wakati kama huu hujulikana kama Fetal Period.(wakati wa kijusi) yani mwili kuanza kukua na sehemu Fulani za mwili kuanza kufanya kazi.

Baada ya wiki ya kwanzatu ya kuingia mimba, chembe mrundiko ya ndani, huunda nusu mbili.
Ya kwanza huitwa hypoblast, na yapili huitwa Epiblast.
Hizi zote zina kazi tofauti katika maendeleo ya kukua kwa mtoto.

HYPOBLAST
Hii huzalisha ule mfumo wa maji ambao ni sehemu muhimu moja wapo ya muundo wa kupitisha chakula kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

EPIBLAST
Huunda mfumo mwepesi (Membrane) ufunikae mtoto. Na kuhifadhi Amnion fluids, ambayo kijusi kitalelewa humo hadi kuzaliwa.
Baada ya hapo Epiblast pia huendelea kuunda chembe tatu maalum au miundo chipukizi.
Ambazo ni.
1 Ectoderm
2 Endoderm
3 Mesoderm

Ectoderm:
hufanya kazi ya kuchipuza na kuzifanya sehemu muhimu nyingi, ikiwemo Ubongo, Uti wa mgongo,Vichocheo, Ngozi, Vidole, na Nywele,

Endoderm:
Huzalisha au kuunda sehemu za ndani za mfumo wa Pumzi na mmeng'enyo na huzalisha sehemu kubwa muhimu kama vile Ini na Pancries.

Mesoderm:
Huunda Moyo, Figo, Mifupa, Ufupa mwororo, Misuli, Chembe za Damu. Na viungo zingine.

Wakati chembe za damu zinapojitokeza katika ule Mfuko wa maji. Mifereji ya damu, huundwa kote kote kwenye embryo na Sehemu ya mwanzo ya Moyo huanza kuchipuza.

Karibu Mara moja ule moyo unaanza kukua kwa haraka, huanza kujikunja na Sehemu zake muhimu huanza kuumbika.

Moyo huanza kupiga kwazia wiki 3 na siku moja. baada ya kutunga mimba.
Mfumo wa kuzungusha damu, ni mfumo wa kwanza wa mwili. Au kundi la viungo vya kwanza kuanza kufanya kazi.

Kati ya wiki ya 3 na ya 4. Mpangilio wa Umbo la mwili huanza kuchipuza
Huku Ubongo na Uti wa mgongo na Moyo huanza kutambulika Pamoja na ule mfuko wa maji.

Ukuaji wa haraka husababisha kujikunja kwa kijitoto, ambavyo kwa kawaida hua kimenyooka
Mfanyiko huu hujumuisha sehemu ya ule mfuko wa maji na kua sehemu ya kuta ya mmeng'enyo.
Na kuunda kifua na sehemu za mmeng'enyo wa huyu binadamu chipukizi.

Maendeleo hayo ya kibiolojia ya ukuaji wa mtoto yenye kustaajabisha huendelea hivyo hadi kufikia kipindi cha wiki 16 (miezi minne.) Hapo kijusi au kiumbe hicho kipya huanza kufanya kazi karibu viungo vyote.
Na hisia mbalimbali zinazoendelea nje huanza kuhisi na kusikia.

Kipindi hiki sasa Amniotic fluids hutengenezwa kwa wingi kabisa kwa ajili ya kumlinda mtoto dhidi ya maambukizi na kufanya maendeleo ya ukuaji wake yawe bora.
Pia amniotic fluid humpa joto mtoto na kulihifadhi. Pia humsaidia mtoto kwenye mmeng'enyo na upumuaji

MATOKEO YA DHARULA
Kuna matokeo ya dharula ambayo ni hatari kwa kiumbe hicho.
Matukio ya hatari yanapo onyesha viashiria ni haraka mama awahi hospitali.
Ili dactari alichunguze tukio hilo na kulichukulia hatua Mara moja.
1 Chupa ama fuko linalomhifadhi mtoto kupasuka kabla ya wiki 37(Prematura repture of membranes) hali hii ni hatari sana mama inabidi awahi hospitali haraka sana.
Sababu mtoto hapo atakua katika hatari ya kupata maambukizi.
Na usalama wake utakua ni mdogo kwakua Yale maji yanayomlinda yamewahi kutoka.
Hapo dactari atachukua vipimo kubaini chanzo cha tatizo pamoja na maelezo ya mama mwenyewe.

Dactari anaweza akam bed rest ama kumwanzishia uchungu haraka ili ajifungue kama mimba itakua na zaidi ya wiki 34. Yote hayo yanaweza kufanyika endapo dactari atavyoliona tukio lenyewe.

Endapo Dactari ataamua mama arudi nyumbani. Basi anaweza kumpatia antibiotic ili kuumlinda mtoto dhidi ya bacteria. Pamoja na kumchoma mama sindano Fulani za steroid ili kumsaidia mtoto kwenye ukuaji wa mapafu.
Pia wakati chupa hiyo imepasuka na ni kabla ya siku kama nilivyoeleza. Mama inambidi. Awe makini ajiepushe kutumia vyoo vya paplic. Na endapo atatumia awe makini sana.
Vile vile mama asifanye mapenzi kabisa mpaka atapojifungua. Pia mama asijiweke vidole ukeni. Pia asioge kwenye tub bath.Kwani hivyo vyote huweza kumuweka mama katika hatari ya kuongeza maambukizi.
Lakini wa mama inawabidi kua makini pindi mnapoona chupa imepasuka kabla ya muda na kuchunguza Yale maji yaliotoka. Kwani utapokwenda hospitali na maelezo ukatoa kadiri ulivyoona husaidia sana kupata huduma kwa haraka.
Kwani humrahisishia daktari kutokutumia muda mkubwa wa kuamua.
Kwa kawaida maji ya chupa hua hayana rangi wala harufu.
Endapo mama ataona rangi ya kijani au brown na harufu. Hiyo ni dalili ya maambukizi.
Au huenda mtoto amejisaidia choo kubwa. Ama alipata risk Fulani iliopelekea kujisaidia choo kubwa.
Au kama utaona wekundu huenda yakawa maji hayo yamechanganika na damu.
Yote hayo mama atapoeleza humrahisishia daktari kukuwahishia huduma.

Kwa mama aliefikisha wiki 36 chupa ikipasuka daktari huanzisha uchungu ili mama ajifungue kuliko kumwacha. au kumfanyia C- section itategemea na afya ya mama kwa kipindi hicho.

2 Kuna tukio lingine ambalo mama kisha pata uchungu na chupa ime pasuka lakini mtoto anakua kachelewa kutoka. Tukio hili hupelekea mtoto kunywa maji hayo. Ambayo Mara nyingi huwaathiri watoto kwenye mapafu na mfumo wa upumuaji.
Ima kuna wakati mwingine mtoto anaweza kutoka akiwa kichwa kimetazama juu. Hili nalo huweza kusababisha mtoto kuonja au kunywa maji hayo. Maji hayo yakaingia kwenye mapafu huathiri mfumo wa upumuaji.

Baada yakua ushatoka hospitali, kisha ukamuona mtoto ngozi inabadirika rangi kua kama blue hivi. Huenda ikawa mfumo wa upumuaji hauko sawa au alikunywa maji hayo. Rudi hospitali haraka kamweleze daktari.

Hayo yote kama mama atajifungulia katika kituo cha afya Dactari anaweza kuondoa hatari hizo kwa asilimia 80.
Kwa hiyo wamama ninawashauri pale unapohisi mjamzito na kuthibitika mjamzito. Pageuzeni katika vituo vya afya kua ni nyumbani.
Namaanisha chochote utachokiona tofauti wahi haraka katika kituo cha afya na Mara utapoona leba inaanza nenda kajifungulie hospitali.
Hiyo itakusaidia kuondoa hatari hizo nilizo zitaja.
Kwako msweet natumaini utakua umeelimika na Umma kwa ujumla.
 
Hapana Dr. Hana
Habari za usiku machuchu .
Ni kwamba kama hana diabetic basi shida yake ni Neva. (Miultiple sclerosis) Tatizo hili ni tatizo la kiafya ambalo linahusisha kushindwa kufanya kazi kwa neva.
Sababu ziko nyingi ingawa anaumri mkubwa lakini kisiwe kigezo ningependa umpeleke hospitali wamfanyie uchunguzi.
Toa maelezo ya kutosha ili dactari aamue kufanyiwa uchunguzi kutokana na atacho kishuku.
Hapana Dr. Hana
 
Sawa dr nimekuelewa japo mimi sikuwa nafahamu huy bint kama ameathirika pia kuhusu michubuko kwa kumbukumbu zangu zinavynituma sikupata wala kuwa nayo pia leo ni siku ya 17 tangu tukio limetkea nimetest negative nimeambiwa nirudi mwezi ujao ...ila hofu yangu ipo kwake tu kama alikua anayo au la
Note:vijana tujihadhari ukimwi upo mateso ninayopata mimi kwa mawazo hayapimiki
Habari za usiku idrissi.
Hupaswi kua na mawazo ya namna hiyo.
Mawazo ya namna hiyo sio mazuri kwani unaweza itikisa kinga yako ya mwili. Wakati tatizo Huna.
Uwamuzi ulioufanya wa kupima ni wabusara sana. Endelea kufuatilia vipimo awamu kama tatu hivi. Pasipokua na stress yoyote ile.
 
Mkuu hujanjbu lakini...
 
Habari Msweet.
Kwanza kabla ya kujua madhara.Ningependa tumjue kwanza mtoto alietumboni.
Anaishije huko, na kwanini anakua!.
Mama au Dada anapo bahatika kushika mimba. Kutoka siku ya kwanza hadi wiki ya 8, ile mimba hutambuliwa kama "Embryo" yaani humaanisha 'kukua ndani'.
Wakati kama huu kwa yule mama mjamzito hujulikana kama Embryonic Period. Huhusishwa na kuumbwa kwa mifumo muhimu ya viungo vya mwili.
Kwanzia wiki ya 8 hadi mwisho wa Mimba, kiumbe hicho hutambuliwa kama Fetus(kijusi) au kwa lugha yetu ni mwana ambae hajazaliwa. Na wakati kama huu hujulikana kama Fetal Period.(wakati wa kijusi) yani mwili kuanza kukua na sehemu Fulani za mwili kuanza kufanya kazi.

Baada ya wiki ya kwanzatu ya kuingia mimba, chembe mrundiko ya ndani, huunda nusu mbili.
Ya kwanza huitwa hypoblast, na yapili huitwa Epiblast.
Hizi zote zina kazi tofauti katika maendeleo ya kukua kwa mtoto.

HYPOBLAST
Hii huzalisha ule mfumo wa maji ambao ni sehemu muhimu moja wapo ya muundo wa kupitisha chakula kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

EPIBLAST
Huunda mfumo mwepesi (Membrane) ufunikae mtoto. Na kuhifadhi Amnion fluids, ambayo kijusi kitalelewa humo hadi kuzaliwa.
Baada ya hapo Epiblast pia huendelea kuunda chembe tatu maalum au miundo chipukizi.
Ambazo ni.
1 Ectoderm
2 Endoderm
3 Mesoderm

Ectoderm:
hufanya kazi ya kuchipuza na kuzifanya sehemu muhimu nyingi, ikiwemo Ubongo, Uti wa mgongo,Vichocheo, Ngozi, Vidole, na Nywele,

Endoderm:
Huzalisha au kuunda sehemu za ndani za mfumo wa Pumzi na mmeng'enyo na huzalisha sehemu kubwa muhimu kama vile Ini na Pancries.

Mesoderm:
Huunda Moyo, Figo, Mifupa, Ufupa mwororo, Misuli, Chembe za Damu. Na viungo zingine.

Wakati chembe za damu zinapojitokeza katika ule Mfuko wa maji. Mifereji ya damu, huundwa kote kote kwenye embryo na Sehemu ya mwanzo ya Moyo huanza kuchipuza.

Karibu Mara moja ule moyo unaanza kukua kwa haraka, huanza kujikunja na Sehemu zake muhimu huanza kuumbika.

Moyo huanza kupiga kwazia wiki 3 na siku moja. baada ya kutunga mimba.
Mfumo wa kuzungusha damu, ni mfumo wa kwanza wa mwili. Au kundi la viungo vya kwanza kuanza kufanya kazi.

Kati ya wiki ya 3 na ya 4. Mpangilio wa Umbo la mwili huanza kuchipuza
Huku Ubongo na Uti wa mgongo na Moyo huanza kutambulika Pamoja na ule mfuko wa maji.

Ukuaji wa haraka husababisha kujikunja kwa kijitoto, ambavyo kwa kawaida hua kimenyooka
Mfanyiko huu hujumuisha sehemu ya ule mfuko wa maji na kua sehemu ya kuta ya mmeng'enyo.
Na kuunda kifua na sehemu za mmeng'enyo wa huyu binadamu chipukizi.

Maendeleo hayo ya kibiolojia ya ukuaji wa mtoto yenye kustaajabisha huendelea hivyo hadi kufikia kipindi cha wiki 16 (miezi minne.) Hapo kijusi au kiumbe hicho kipya huanza kufanya kazi karibu viungo vyote.
Na hisia mbalimbali zinazoendelea nje huanza kuhisi na kusikia.

Kipindi hiki sasa Amniotic fluids hutengenezwa kwa wingi kabisa kwa ajili ya kumlinda mtoto dhidi ya maambukizi na kufanya maendeleo ya ukuaji wake yawe bora.
Pia amniotic fluid humpa joto mtoto na kulihifadhi. Pia humsaidia mtoto kwenye mmeng'enyo na upumuaji

MATOKEO YA DHARULA
Kuna matokeo ya dharula ambayo ni hatari kwa kiumbe hicho.
Matukio ya hatari yanapo onyesha viashiria ni haraka mama awahi hospitali.
Ili dactari alichunguze tukio hilo na kulichukulia hatua Mara moja.
1 Chupa ama fuko linalomhifadhi mtoto kupasuka kabla ya wiki 37(Prematura repture of membranes) hali hii ni hatari sana mama inabidi awahi hospitali haraka sana.
Sababu mtoto hapo atakua katika hatari ya kupata maambukizi.
Na usalama wake utakua ni mdogo kwakua Yale maji yanayomlinda yamewahi kutoka.
Hapo dactari atachukua vipimo kubaini chanzo cha tatizo pamoja na maelezo ya mama mwenyewe.

Dactari anaweza akam bed rest ama kumwanzishia uchungu haraka ili ajifungue kama mimba itakua na zaidi ya wiki 34. Yote hayo yanaweza kufanyika endapo dactari atavyoliona tukio lenyewe.

Endapo Dactari ataamua mama arudi nyumbani. Basi anaweza kumpatia antibiotic ili kuumlinda mtoto dhidi ya bacteria. Pamoja na kumchoma mama sindano Fulani za steroid ili kumsaidia mtoto kwenye ukuaji wa mapafu.
Pia wakati chupa hiyo imepasuka na ni kabla ya siku kama nilivyoeleza. Mama inambidi. Awe makini ajiepushe kutumia vyoo vya paplic. Na endapo atatumia awe makini sana.
Vile vile mama asifanye mapenzi kabisa mpaka atapojifungua. Pia mama asijiweke vidole ukeni. Pia asioge kwenye tub bath.Kwani hivyo vyote huweza kumuweka mama katika hatari ya kuongeza maambukizi.
Lakini wa mama inawabidi kua makini pindi mnapoona chupa imepasuka kabla ya muda na kuchunguza Yale maji yaliotoka. Kwani utapokwenda hospitali na maelezo ukatoa kadiri ulivyoona husaidia sana kupata huduma kwa haraka.
Kwani humrahisishia daktari kutokutumia muda mkubwa wa kuamua.
Kwa kawaida maji ya chupa hua hayana rangi wala harufu.
Endapo mama ataona rangi ya kijani au brown na harufu. Hiyo ni dalili ya maambukizi.
Au huenda mtoto amejisaidia choo kubwa. Ama alipata risk Fulani iliopelekea kujisaidia choo kubwa.
Au kama utaona wekundu huenda yakawa maji hayo yamechanganika na damu.
Yote hayo mama atapoeleza humrahisishia daktari kukuwahishia huduma.

Kwa mama aliefikisha wiki 36 chupa ikipasuka daktari huanzisha uchungu ili mama ajifungue kuliko kumwacha. au kumfanyia C- section itategemea na afya ya mama kwa kipindi hicho.

2 Kuna tukio lingine ambalo mama kisha pata uchungu na chupa ime pasuka lakini mtoto anakua kachelewa kutoka. Tukio hili hupelekea mtoto kunywa maji hayo. Ambayo Mara nyingi huwaathiri watoto kwenye mapafu na mfumo wa upumuaji.
Ima kuna wakati mwingine mtoto anaweza kutoka akiwa kichwa kimetazama juu. Hili nalo huweza kusababisha mtoto kuonja au kunywa maji hayo. Maji hayo yakaingia kwenye mapafu huathiri mfumo wa upumuaji.

Baada yakua ushatoka hospitali, kisha ukamuona mtoto ngozi inabadirika rangi kua kama blue hivi. Huenda ikawa mfumo wa upumuaji hauko sawa au alikunywa maji hayo. Rudi hospitali haraka kamweleze daktari.

Hayo yote kama mama atajifungulia katika kituo cha afya Dactari anaweza kuondoa hatari hizo kwa asilimia 80.
Kwa hiyo wamama ninawashauri pale unapohisi mjamzito na kuthibitika mjamzito. Pageuzeni katika vituo vya afya kua ni nyumbani.
Namaanisha chochote utachokiona tofauti wahi haraka katika kituo cha afya na Mara utapoona leba inaanza nenda kajifungulie hospitali.
Hiyo itakusaidia kuondoa hatari hizo nilizo zitaja.
Kwako msweet natumaini utakua umeelimika na Umma kwa ujumla.

Asante sana Daktari kwa elimu hii. Hakika u mwalimu mzuri. Jamii yako tuna kupata vema. Big up.
 
Back
Top Bottom