Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Mkuu me natatizo la woga sana tena the same time ninahasira hasa pale mpenzi wangu anaponichanganya zile hasira najikuna zimemwangukia mtu hata asiyehusika ila si kwa kupigana hapana ni kwakumfanyia kiburi au kumtolea maneno mabaya na hali hii imenitesa kwa mda mrefu tangu nimebalehe mpaka sasa ninatazamia kuoa. Nilijaribu kuulizia wakaniambia kuwa tatizo linatokana na kutofanya mapenzi kwa mda mrefu. Me kwa upande wangu sijui kama ni tabia ya asili au nilakisaikolojia
 
Nini sababu za ujauzito kutunga nje ya kizazi?
Habari Mali ya mtu:
Ndugu sababu ziko nyingi sana kutegemea na chanzo chake.

Ndugu.mimba kutunga nje ya kizazi, kitaalam hujulikana kama. Ectopic pregnancy .
Hii mimba hua Mara nyingi inajitungisha nje kabisa ya mfuko wa kizazi.
Yani badala ya kukaa ndani ya nyumba ya uzazi(Uterus)yenyewe huenda kukaa kwenye mirija (Fallopian tub). Ambayo mirija hii kazi yake si hiyo. Kazi ya msingi ya mirija hii ni kusafirisha mayai, kutoka katika sehemu yanapozalishwa(Overy), hadi kwenye nyumba ya uzazi ( uterus).

Mara baada ya utungisho misuli inayozunguka mirija ya fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyoko ndani ya mirija hii, husukuma kiini tete au yai lililorutubishwa, na kulipeleka kwenye Uterus.

Kiini tete au Yai lililorutubishwa lifikapo kwenye Uterus hujipachika.

MIMBA KUTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI.

Mimba kutunga nje ya nyumba ya uzazi au ectopic pregnancy.
Ni tatizo ambalo limetokea kuwaathiri Wanawake mbalimbali. Kwa kawaida isipokua Mara chache sana, mimba hizi hua hazikui na kua mtoto kamili.
Aidha mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa kua Mara nyingi husababisha Mama kupoteza damu nyingi kwa kupasuka mrija na pengine kusababisha kifo.

SABABU
Sababu na chanzo halisi cha tatizo hili hakijulikani. Ingawa kuna mambo kadhaa huwa yanahusishwa kusababisha.
Magonjwa ya maambukizi katika mfumo wa uzazi hasa Yale ya uvimbe.
Sababu nyingine ni matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba hii ni kwa baadhi ya wanawake na kuoteana kwa tishu za kwenye nyumba ya uzazi.
Pia uvutaji wa Sigara hua unahusishwa na tatizo hili au kama mwanamke alishawahi kufanyiwa upasuaji wa maeneo ya tumbo.uliohusu mirija ya fallopian. na kusababisha Mrija husika kusinyaa.

Magonjwa ya kingono kama vile kaswende au Yale magonjwa ya ngozi ndani ya uzazi na mirija kua na umbo lisilo la kawaida na kuvimba.
Utoaji mimba, kwa kutumia dawa ama njia yoyote ile kwani tendo hilo hufanya kuharibu miundo mbinu ya mfumo wote wa uzazi na kusababisha isiwe katika hali ya kawaida.
Ni hayotu kwa uchache naamini utakua umeelimika ndugu.
 
Asante mkuu nmekupata vilivyo
 
Habari za usiku machuchu .
Ni kwamba kama hana diabetic basi shida yake ni Neva. (Miultiple sclerosis) Tatizo hili ni tatizo la kiafya ambalo linahusisha kushindwa kufanya kazi kwa neva.
Sababu ziko nyingi ingawa anaumri mkubwa lakini kisiwe kigezo ningependa umpeleke hospitali wamfanyie uchunguzi.
Toa maelezo ya kutosha ili dactari aamue kufanyiwa uchunguzi kutokana na atacho kishuku.
Sawa Dr.
 
Kama kichwa kinavyosema hapo nakaribisha maswali yanayo husu afya
Hello kaka, kwanza nikupe hongera na pole za dhati kwa muda wako wakujibu mengi unayoulizwa kwa marefu na mapana. Huo ni moyo wa kipekee.
I sincerely congratulate yu. M.Mungu akusimamie na akujalie sawasawa na mahitaji yako
...
Nina shida tatu; kwanza me ni KE (26)sina mtoto na wala sijawahi kushika mimba wala sijawahi kujaribu kushikaa .
kwanza huwa nina mzunguko wa 28 days (hedhi).ila nimekua na tatizo ambalo hunikosesha sana amani, huwa naingia ktk siku zangu kwa siku tano ad saba..huwa ni bleed ambayo ni heavy na wakati mwingine maumivu makali ya tumbo. Pia mara nyingi huwa na bleed ktk hali ya mabonge bonge napata wakat mgumu saana
Haishii hapo, kabla ya siku 28 kuisha huwa najikuta nikipata tena bleed japo sio nyingi lakn huwa kama nyeusi zaid na wakati mwingine rangi kama ya udongo/kahawia. Nimejichunguza nikagundua hii hali hutokea kwenye zile ovulation days yaan kuanzia sana sana siku ya 11 ad 17 baada ya kumaliza siku saba za bleed. Napata wakat mgumu saana kuelewa hili nini
Hosp nilishaenda but just niliambiwa ts hormone imbalance..kitu ambacho sikielew. Napata mawazo saana
Msaada kwanza hili kabla sijaendelea na matatizo mengine. Am ready kutoa maelezo zaid
.hali hii ina miaka takriban 7 japo kuna miezi huwa sipat hali hyo
 
Ndio mda mwengine
Habari ndugu Bilionea.
Kwanza nikuombe radhi Kwa kuchelewa kujibu kwa wakati. na hii ni kutokana na majukumu ya kikazi.
Ni kwamba kutokana na maelezo yako mtu huyo atakua na tatizo kwenye ubongo. Na sehemu yenyewe ni eneo la kati(Serebral cortex).
Hapo vipimo vya CT SCANNER ni muhimu ili Ku prove tatizo hilo sawa sawa.
Kwani dalili za matatizo kwenye ubongo hua kuna wakati, zinaingiliana. Hivyo mgonjwa wa namna hiyo anatakiwa apelekwe hospitali ili uchunguzi ufanyike.
 
Doctor mkuu me nahitaji kujua magonjwa haya kama nitapata ufafanuzi itakuwa vyema zaidi.

1. Kwanini ugonjwa wa amiba kwa kutumia dawa za hospitalini hauponi? Hii ni kwa sababu nimesha wahi tumia kila aina ya dawa za hospital lakini hakuna mafanikio na sio mimi tu hata watu wengine wanasema hivo hivo.

2. Nikweli kwamba ugonjwa wa HENIA iliyoko katika utumbo mpana ambayo imetokeza kwenye njia ya hajakubwa haitibiki kwa dawa za kawaida mpaka ufanyiwe upasuaji. Kuna rafiki yangu ako na matatizo ya Henia
 
Doctor sorry kwa usumbufu wa maswali ya kila aina. Nadhani memesha uliza maswali watatu ya aina tofauti ambayo bado sijajibiwa najua unakazi kumjibu kila anayekuuliza but ndio kalama ulopewa na mungu.

Swali langu la mwisho nikwamba kama mtoto anaweza kuwa na vina sabu kutoka kwa wazazi wake inakuaje baba anakuwa na tabia hizi pendine ziwe mbaya au nzuri lakini mtoto akawa na tabia tofauti na zile za baba yake hii imekaaje
 
Habari Ndugu.
Hali kama hiyo ikiwa haiambatani na dalili zingine.
Huenda ukawa unasumbuliwa na mgonjwa ya fizi.

Kuna aina kubwa mbili za mgonjwa ya fizi ambayo ni
1. Gingivitis
2. Periodontitis
Ninakushauri ukaonane na daktari wa meno kwa uchunguzi zaidi.
Mimi sipendi kukwambia unaupungufu kua unaupungufu wa vitamin C.
Kwa maisha ya kawaida sio rahisi kua na upungufu namna hiyo
Kwanza tuanze na sababu ambazo ni tishio ndio tuje kumalizia na mambo ya vitamin.
Asante sana Dr
 
Mate hayakauki ila mdomoni ndani kule kwenye koo kwenye yale matezi mawili la kulia na kushoto yamekuwa na vitu kama vidonda kumeweka doti doti nyeupe na kuna wekundu na vidot vingne vya rangi kama cream nikiingiza kidole nikikwangua kwa nguvu kinatoka kipande cha kitu kinatoa harufu Kali sana ukikiminya kinaminyika au wakati mwingine hata nikikooa vinatoka hvyo vtu mdomon ukikiminya kinapasuka ila kinanuka sana, kwa nje sasa upande wa kulia ndokuna kauvimbe kwa nje hukioni ila ukishika unaskia kama kigololi hv sahv kinanipa maumivu nikikishika
Habari ndugu Tembocard.Pia pole kwa kusubiri. Ndugu zangu ni majukumu ya kazi.ndio kisababishi kikubwa kushindwa kujibu kwa wakati.
Ni kwamba uvimbe huo kitaalam ni swollen limph nodes.

Ni uvimbe ambao hujitokeza baada ya mwili kuumia na kushambuliwa na vijdudu au bacteria.
Kazi maalum ya vimbe hizi ni kugundua na hushambulia vitu au wadudu wanaoingia mwilini na kusababisha magonjwa.
Hivyo ni kitu muhimu sana katika ulinzi au kinga ya mwili.

Miongoni mwa maeneo zinazopatikana vimbe au tezi hizi ni maeneo ya nyonga(groin). Nyuma za masikio chini ya tayari na kidevu.
Nyuma ya kichwa. Maeneo ya kwapani(armpit) na shingoni.

Kukaa maeneo tofauti ni kutokana na eneo lililo na tatizo lilipo kaa.
Kwa hiyo bwana tembocard, napenda nikwambie kwamba uvimbe huo sio wa hatari na hauto kwisha.hadi maambukizi hayo ya streptococcal yatapoisha, mule ndani kwenye koo.
 
Asante sana doctor ubarikiwe kwahiyo nitumie Dawa gani au niache tu hvyo hvyo nitapona
 
Asante sana mkuu.

niliwah kukutana na daktari mmoja akaniambia nina upungufu wa uzalishaji wa sparm,

Ushauri naomba, ni spitali gani au ya aina gani nijalibu kwenda.

na jea kama kuna vyakula au first aid yoyote ya kuweza kunisaidia kwa kuanzia?
Habari ndugu does 2020.
Pia pole kwa kusubiri. Ndugu ni mambo ya kazi ndo sababu kubwa.
Ndugu nenda hospitali ya mkoa.
Hapo daktari utaemkuta. Utamweleza tatizo lako. Na yeye ndio atae kuelekeza uingie chumba gani.
Atapokuelekeza uingie utamkuta daktari wa tatizo lako.
Hivyo uta mweleza na atakuamulia uchunguzi.

Ni vema uchunguzi ufanyike ili tatizo lijulikane liko wapi. Kama ni Mrija imekonda au Mbegu hazizalishwi.
Na kama Mbegu hazizalishwi, atakuamulia vipimo vya damu ili kuangalia chanzo hasa maabukizi ya bacteria.
Ambayo na yenyewe kuna wakati husababisha kuharibu zisizalishwe.

Kwaupande wa lishe ningependa nisiwe miongoni mwa watu wa tiba mbadala. Na hii si kwamba siwaamini "hapana" Bali kuchunguza ndio kutaleta tiba yenye ufanisi.
Kwani ninaweza nikakushauri lishe kumbe Mbegu zina zalishwa ila zinashindwa kwenda kujichanganya na shahawa. Kutokana na kukonda Mrija.
 
Mkuu me natatizo la woga sana tena the same time ninahasira hasa pale mpenzi wangu anaponichanganya zile hasira najikuna zimemwangukia mtu hata asiyehusika ila si kwa kupigana hapana ni kwakumfanyia kiburi au kumtolea maneno mabaya na hali hii imenitesa kwa mda mrefu tangu nimebalehe mpaka sasa ninatazamia kuoa. Nilijaribu kuulizia wakaniambia kuwa tatizo linatokana na kutofanya mapenzi kwa mda mrefu. Me kwa upande wangu sijui kama ni tabia ya asili au nilakisaikolojia
Habari bwana kiti chema
Na pole kwa tatizo hilo. Ni kwamba tatizo hilo linaweza kua na sababu mbili.
1 ni kwamba huenda mfumo wa kemikali yaani neurotransimitters.huko sawa.

Kazi ya kemikali hizi ni kupitisha taarifa mbali mbali za ujumbe, kutoka seli moja ya neva mpaka kwenye seli nyingine.
Iwapo kemikali hizi zikawa na kiwango kisicho sahihi(kupungua ama kuongezeka)
Taarifa hazitoweza kusafirishwa katika seli za Neva na hatimae taarifa hizo hazitoweza kufika kabisa kwa ubongo. ama kufika nusu ama kufika zaidi ya taarifa halisi. Au kwa lugha rahisi taarifa Zinakua zikifika kwa ubongo Zinakua za ubongo.
Hali hiyo ambayo Mara nyingi husababisha utendaji kazi wa ubongo ukawa ni wa uongo uongo.
Yani hapo na maanisha mhusika anakua akipewa taarifa na ubongo zisizo sahihi.

KIVIPI NA INAKUAJE
Ni kwamba kama macho ya mhusika yataona kitu cha kufurahisha kawaida.
Ubongo utamualifu mhusika kua anacho kiona ni cha kufurahisha kupita kiasi. Hivyo mtu hapo mtamuona anafurahi ama kucheka sana kwa jambo ambalo ni la kawaida kabisa na pengine jambo lenyewe lilikua si la kumfanya scheme, Bali lilikua ni la kumfanya atabasamu.

Ama macho yanaweza yakaona kitu cha kuudhi kiasi.
Lakini taarifa itayoenda kwa ubongo itakua tofauti, hivyo ubongo utalazimika kutoa taarifa kwa mhusika, taarifa ya uongo.
Kwamba kilichoonekana ni cha kuidhi sana. Hivyo hapo mhusika mtamuona amekasirika sana tena kupita kiasi kwa jambo ambalo hakutakiwa akasirike kiasi hicho.
Hapo ndipo mnashuudia Mtu ana mchoma kisu mwenzie kwa jambo ambalo wangezungumza na likaisha..

Ama masikio yanaweza yakasikia sauti ambayo sio ya kutisha lakini taarifa itafika kwa ubongo tofauti
Na hapo ubongo utalazimika kutoa taarifa kwa mhusika, kua kilichosikika ni hatari sana, na sio hatari ya siku moja ni ya maishani.
Hapo ndipo mtamuona mhusika anaogopa sana tena kwa jambo ambalo sio la kutisha nk.

2 Ni kwamba Nasaba (genetics).
Hapo kama familia ina matatizo haya ya hofu ilio pitiliza. Uko uwezekano hali hiyo ya hofu iliopitiliza kuendelea kadiri ya vizazi na vizazi.

Ndugu kitichema hali hiyo sio nzuri kwanza nikushauri nenda hospitali ukakutane na daktari wa Afya akili.umweleze. tatizo lako. Na uchunguzi wa kina juu ya afya ya akili utafanyika.
 
Doctor habari yako pole na kazi, bado hujanijibu tatizo langu
Habari Ndugu Tembo card.
Nimekujibu swali lako tayari. Na napenda kukueleza ndugu yangu, kwamba Nina jibu maswali, kulingana na yanavyokuja.
Kwa mlolongo ili kila mmoja apate kuona jibu lake nimemjibu. Na aweze kulizika na majibu. Kwani ninaimani wanaouliza maswali wanakua na matatizo juu ya hayo wanayoyauliza.
Kwa hiyo ndugu ni naona kama nisipo fuata utaratibu ninaweza kua mmoja wa kumchelewesha mtu kupata ufumbuzi kwa haraka kwa tatizo lake.
Jingine ukauliza swali nikakijibu ukauliza tena kwa mara ya pili, Basi hilo ulilouliza mpaka nilifikie tena.
Naomba tuwe wavumilivu. Nawapenda na ninawajalini sana,
Asante.
 
Kweli kabisa ... Wakumbuke nawe pia unamajukum kama wao na kazi nyingi zinakungoja pia haupo JF masaa 24 ...umachoka kama wao na pia unahitaji mapumziko na huu ni msaada. Uvumilivu ni msingi + na busara (Ubarikiwe Dr.)
 
Habari ndugu Hosh Kosh
Ndugu kwakua umesha sema tatizo ni la muda mrefu Tafadhali tusiongeze muda wa kuzidi kuathirika mtoto na wala siitaji kujua ana umri gani.

Jambo la maana kwako ni kumpeleka mtoto hospitali kwa wataalam wa eneo hilo. Pale cha kwanza watamfanyia vipimo vya C/S ya huo uchafu unaotoka sikioni. Pamoja na mambo mengine yataendelea.
sawa ndug, shukran nataka nijaribu nipo dar, unadhan unanishaur wap naweza pata matibabu sahihi
 
Dr Mama yangu anasumbuliwa sana na ganzi katika mikono na miguu yake kila mara yeye anajishugulisha na uchomaji wa keki je,tatiz litakuwa nini?..maana ana mwaka sasa linamsumbua
 
Back
Top Bottom