Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Nashukuru sana Doctor kwa ushauri wako ila naomba kuuliza nitumie mbinu gani ili kuweza kupata rufaa maana daktari anayenishughulikia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro hataki kuniandikia rufaa ili niweze kwenda kufanyiwa MRI test akidai kuwa tatizo langu halina haja ya kufanyiwa MRI eti kuwa niendelee kutumia dawa anazonipa ambazo ni NEURO SUPPORT na EYE SUPPORT.Nang'ang'ania kupata rufaa kwa sababu za kiutumishi ili nisipoteze haki zangu km mtumishi wa umma.Asante.
Docta please ushauri wako hapa.
[emoji115] [emoji115]
 
Sawa docta alafu kuna ndugu yngu anasumbuliwa na kapimwa kakutwa na tb anatumia dawa....lkn ikifika usiku kupumua anapata tabu sna anashndwa hta kulala anahema kwa tabu km vile mtu mwenye athma sometimes pumzi inakata hata dakika anabaki kujipiga piga tu afu pia kuna vitu vinamtoka mwilini kama viuvimbevimbe hv ameenda tena hospital wamempima wamesema hamna tatizo.please doctor Nkingwamh naomba msaada wako.
Habari ndugu.
Je hali hiyo ya kupata shida katika kupumua na vivimbe hivyoJe imekuja baada ya kuanza matibabu ya TB au ilianza nyuma?
 
Habari ndugu.
Je hali hiyo ya kupata shida katika kupumua na vivimbe hivyoJe imekuja baada ya kuanza matibabu ya TB au ilianza nyuma?
Dr nina tatizo la meno kutoboka na huwa hayaumi mpkaa linaishaa lenyewe linakuwa kipisi kwa kukatika katika je tatizo ni nini??
 
Doctor,
nina tatizo la kusumbuliwa na uchovu na maumivu ya mwili mda mwingi, hasa wakati wakuamka asubuhi, baada ya tendo la ndoa nasikunziima mbele, au baada ya kufanya kazi nzito yani kubebabeba vitu vizito.
Habari bwana anasbo
Una umri gani ndugu na mili yako iko naukubwa au kawaida
 
Habari Dokta pole sana Na Kazi na Majukumu ya kila siku

nimekuwa na tatizo la Fizi kuvimba sehemu ya juu

Nilihudhuria Katika hospitali Nikapewa Dawa ya Mouth wash haikunisaidia
Nikarudi hospital nyingine wakanipa metronidazole gel lakini Bado naona hakuna mabadiliko

Please msaada wako nitumie Dawa gani itaweza kunisaidia?
Dokta Pitia na hapa...
 
Sasa ndugu inawezekana kukawa na shida kwenye prostate gland.Ngoja tuishuku kwanza. Je kuna hali hizi hua zikikutokea
1 mkojo kutoka Mara kwa Mara
2 unapomaliza kukojoa hua ukihisi mkojo umebakiza kwenye bladder yako
3 kukojoa sana usiku...

1. kutoka vipi apo sijakufahamu kidogo
2. na hili sina uhakika nalo
3. Sina tatizo hilo
4.pindi ikiwa sikunywa maji mengi hua napata maumivu madogomadogo wakati wa kukojoa
5.hilo sijalifaham mkuu
6. kwa kweli siyatambui hayo matatizo ya UTI
7.kweli maumivu huo yanatokeatokea mda mwengine lakini simakubwa
8. nikweli, nafika mapema sana kileleni wakati wa sex
 
Dr,mm ni kijana wa kiume.nimevimba lymph nodes(tezi) za nyuma ya sikio la kulia pamoja na kuumwa kichwa tangu mwaka jana.nimefanya vipimo kadhaa ikiwemo HIV,TB,FBP zaidi ya mara3 lakini hamna tatzo lililoonekana.nshatumia dawa za maumivu na antibiotics kadhaa lakin bado.nimeambiwa nkafanye biopsy waipime.huenda ikawa ni tatzo gani??
 
Daktari nini sababu ya kuhisi moyo unadundia kichwani ama wakati mwingine mwili mzima
 
Umri miaka 34, tatizo: kutetemeka viungo, historia; alishawahi kutumia pombe hapo nyuma akaacha!! Nini matibabu yake mkuu!!
 
Mi tatizo langu nasumbuliwa na.

Tatizo la kupepesuka pindi napotembea ama napoinuka kutoka kwenye kiti ghafra... Ila tatizo hili uzidi hasa pale macho yanapoonesha dalili ya kuchoka( dalili ya macho kuwa mazito kama ninausingizi).

Pia nikitoka mazoezini tatizo hili huwa maradufu ama kama usiku nimelala na Mama wa Toto nikiamka asubuhi nakua kama nimeliamsha tatizo.

Naomba msaada
 
Back
Top Bottom