Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Karibuni kwa maswali yote ya kiafya

Habari bwana idrissi
Mama anasumbuliwa na tatizo liitwalo Peripheral neuropathy.
Bwana idrissi matatizo haya Mara nyingi hua ni kuzorota au kushindwa kufanya kazi kwa Neva za pembezoni mwa mwili.
Na Mara nyingi hua yanasababu, sababu hizo ambazo pengine zimepelekea kuharibu vitamin mwilini
Hasa vitamin B. Sasa kabla sija kushauri ningependa unijulishe mama ana umri gani na je anatatizo la kisukari? Unijulishe hayo kisha nitakua na la kushauri zaidi.
Asante
Miaka 51 hana tatizo la kisukari
 
Habari.
Nikweli kumekua Na ongezeko kubwa la tatizo hilo zaidi kwa Wanawake. Na hii nikutokana sana na mambo ya Urembo.
Kwani kuna baadhi ya vipodozi Na dawa za nywele huchochea sana uzalishaji wa Oestrogen mwilini, kuliko kawaida.
Ongezeko hili la uzalishwaji wa oestrogen huchangia kwa kiasi kikubwa sana cha ukuaji wa fibroids

Kemikali hizi zinazoambatanishwa kwenye vipodozi au dawa za nywele hupenya kwenye ngozi kutokana Na matumizi wanayotumia Wanawake kwa lengo la kupendeza.
Kwa ujumla kemikali hizi. Hazimuathiri mtumiaji kwa matumizi Bali hata kwa kuvuta harufutu.
Ukichunguza wamama au wadada wengi hubadiri matumizi ya dawa kua vipodozi.

Kwamfano kuna dawa zilizo katika kundi la steroids kama vile hydrocortisone,Betamethasone,Dexamethasone,Beclometasone,Clobetasol,Prednisolin nk

Kimsingi dawa hizi ni dawa za allergy Na husaidia kupunguza nguvu za kinga za mwili.
Zinapokua katika mfumo wa Cream,Lotion au gelly husaidia kuondoa allergys kwenye ngozi.

Mbali Na kuondoa allergy bali pia huondoa ngozi ngumu Na rough ya nje. (Ngozi ambayo hutusaidia kutukinga Na miale mikali ya jua, kansa, michubuko Na kadhalika.

Dawa hizi kwa kawaida zinatakiwa zitumike kwa dozi maalum.Na kwa muda usiozidi wiki mbili.
Sasa kwa bahati mbaya wamama au wadada wamekua wakibadirisha matumizi ya dawa hizi Na kuzifanya kua vipodozi.

Kwa kawaida dawa hizi hunyonywa Na kuingia mwilini Na husababisha kwenda kuzuia tezi la adenal linalozalisha hormone ya adrenalin lisizalishe hormone hiyo.Na endapo matumizi hayo mabaya yataendelea, hufanya tezi hilo lisinyae Na kufa kabisa.

Matokeo ni mengi mabaya endapo tezi hili litakufa ambayo yanaweza kujitokeza mbali Na hayo ya fibroids niliotaja huko juu. Yakiwepo ya kupungua kinga za mwili, Na kupungua kwa kiwango cha homon ya Oestrogen.Na ikipungua umbo au shepu ya kike huanza kukimbia.
Hapo matokeo ni kuota ndevu Na sauti nzito kama mwanaume. Maziwa ya kifuani hunyauka. Na kuingia katika ukomo wa hedhi kabla ya umri. Na kua Na sura nzito kama mwanaume nk.

Sasa ili ujue upo katika kundi la waathiriwa. Tazama lotion yako ,Cream au gelly walipoandika "COMPOSISION"au INGREDIENTS ukiona kuna hizo dawa nilizozitaja hapo juu basi tambua upo katika hatari. Chukua hatua haraka kwa kuanza kuziacha

Na ukumbuke hutakiwi kuziacha ghafla, anza kuacha taratibu.kwani ukiacha ghafla kutokana Na nilioyaeleza huko juu utapata matatizo makubwa.
Kwani hapo ulipo kama vipodozi hivyo ushatumia muda mrefu basi huenda tezi ya adenal haifanyi kazi.
Hivyo itabidi uziache taratibu ili adrenal aanze kurudia majukumu yake ya kiutendaji kazi.

Kwa upande wa option za matibabu kwa waathirika fibroids, ziko option mbili.kutegemea Na chanzo chake
Ya kwanza ni matumizi ya dawa ikiwa ni pamoja Na kurekebisha mfumo wa homon.
Ya pili ni upasuaji ili kuiondoa fibroids yenyewe lakini pia mfumo wa homon ni lazima uangaliwe. Vinginevyo, baada ya upasuaji fibroids inaweza kurudi
Msweet nimatumaini yangu utakua umenufaika, karibu tena
Safi dk
 
Kama kichwa kinavyosema hapo nakaribisha maswali yanayo husu afya
Habari za wakati huu Daktari.

Kwanza kabisa natoa shukurani za dhati kwa elimu unayoendelea kuitoa kwa umma.

Naomba kufahamu faida na hasara za kuoga kwa kutumia maji ya baridi vs maji ya moto kitaalamu zaidi kwa watu wazima..... wake kwa waume.

Asante.
 
Asante.
Kwa kweli sina kumbukumbu yakua na tatzio serious la tumbo zaid ya kuumwa tumbo kawaida kabla ya kuvunja ungo. Sasa sikumbuki kama lilikua linauma chini ya kitovu au laa maana sikuwa na uelewa huo. Just nilikua najua tu tumbo linauna. That's all
OK kwakua umesha nieleza menstrual cycle, nadhani tutakua tushapata pa kuanzia.
Naomba niendelee kukuuliza zaidi.

1 ukiwa unableed je maumivu unayoondelea nayo hapo hua yakiambatana na maumivu ya nyonga?

2 Ukiwa katika siku za kawaida (zisizo za hedhi) je kuna maumivu chini ya mgongo ambayo hua yakiendelea mda wote?

3 Je katika maisha yako ya kila siku hua ukijihisi umeshiba hata kama hujala mda mrefu?

4 katika kipindi kile Ukiwa unashiriki tendo la ndoa je kuna maumivu uliokua ukiyasikia, ambayo badala ya kusikia furaha wewe ukawa husikii furaha kwa ajili ya maumivu?
 
Nina tatizo la mgongo kuuma sana hasa wakat wa usiku pia nikikaa muda mrefu nimechek xray hamna tatzo.. Tatzo hili nila muda mrefu toka 2008 nikilala uck had nijikunje ndo napata nafuu siwez kaa kwa kunyooka au kulala nimenyooka unauma sana
Habari ndugu Mawesee.

Kabla sijaendelea kukujibu ninge penda nijue umri wako pamoja na hali ya mwili wako(mnene/simnene)au uzito, kama hutojali!
 
Miaka 51 hana tatizo la kisukari
Sawa Mr Idrissi. Kwa umri huo nadhani inawezekana zikawa nerves zenyewe pasipo kua na sababu yoyote zikawa zimeanza kuchoka.
Na hii ni kutokana na mapito ya shughuri za kimaisha katika miaka ya nyuma, ambayo ni pamoja na Uzazi.
Hivyo naomba njoo PM nikupatie maelekezo. Asante.
 
Sawa Mr Idrissi. Kwa umri huo nadhani inawezekana zikawa nerves zenyewe pasipo kua na sababu yoyote zikawa zimeanza kuchoka.
Na hii ni kutokana na mapito ya shughuri za kimaisha katika miaka ya nyuma, ambayo ni pamoja na Uzazi.
Hivyo naomba njoo PM nikupatie maelekezo. Asante.
habar za jion
 
Habari ndugu Mawesee.

Kabla sijaendelea kukujibu ninge penda nijue umri wako pamoja na hali ya mwili wako(mnene/simnene)au uzito, kama hutojali!
Habar za jion Dr
Mimi napata utata kidogo kuhusu ili
Ivi mtu akiugua ugonjwa wowote kinga zake zika shuka anakua na HIV+? au
 
Nina malengelenge mwilini nini tatizo na dawa yake ni ipi
 
OK kwakua umesha nieleza menstrual cycle, nadhani tutakua tushapata pa kuanzia.
Naomba niendelee kukuuliza zaidi.

1 ukiwa unableed je maumivu unayoondelea nayo hapo hua yakiambatana na maumivu ya nyonga?

2 Ukiwa katika siku za kawaida (zisizo za hedhi) je kuna maumivu chini ya mgongo ambayo hua yakiendelea mda wote?

3 Je katika maisha yako ya kila siku hua ukijihisi umeshiba hata kama hujala mda mrefu?

4 katika kipindi kile Ukiwa unashiriki tendo la ndoa je kuna maumivu uliokua ukiyasikia, ambayo badala ya kusikia furaha wewe ukawa husikii furaha kwa ajili ya maumivu?
Asante,
1. Miaka ya nyuma ilikua hvo, lkn kwa sasa nina miaka mingi sijapata maumivu ya nyonga wakati wa bleed
2.hapana, sina kumbukumbu za kupata maumivu chini ya mgongo
3.hapana, nikiwa sijalaa njaa inauma sana tu
4. Wakati wa sex nilishawahi hisi maumivu mara chache
 
Habari bwana tembocard
Kwa uvimbe huo hauezi kwisha hata ukitumia dawa, jambo la maana hapo ni kutibu lile tatizo lililoko kinywani.
Kwani hilo ndilo lililoleta huo uvimbe.
Nenda hospitali mweleze dokta hali hiyo, pia na muda liliokuepo nae atahitaji kuliona hivyo atakueleza utanue mdomo, na ataangalia.
Akiviona atatambua type yake kisha atakuandikia dawa za msingi.
Asante.
Asante doctor
 
doctor naomb kuliza ni mda gani virus vya ukimwi vinaweza kuonekana baada y kufanya mapenzi na kuhisi kama umeambukizwa n mwenzi wako na kwenda kupima hospitali?
 
Doctor habar naomba unisaidie kwa hili, eti ni nini kinasababisha uke kuwa mkavu sana yani hata nikiwa sifanyi mapenzi uke unakuwa mkavu ukigusa hakuna maj maj unakuwa kama umeshika paja yan panakuwa pakavu sana hata nikiwa danger day bado kukavu ukigusa kidole kinatoka kikavu hakina hata maji maji, hata nikifanya mapenz naandaliwa hata lisa lizima nitanyonywa uchi mpaka nafika kileleni ila wakat wa kuanza tu kufanya kunakuwa kukavu mpaka tuweke mate au mafuta bila hvyo naumia mpaka nachanika, naomba nisaidie tatizo ni nini doctor
 
Habari ndugu Njoo. PM nadhani tutaelewana vizuri.
Sawa docta alafu kuna ndugu yngu anasumbuliwa na kapimwa kakutwa na tb anatumia dawa....lkn ikifika usiku kupumua anapata tabu sna anashndwa hta kulala anahema kwa tabu km vile mtu mwenye athma sometimes pumzi inakata hata dakika anabaki kujipiga piga tu afu pia kuna vitu vinamtoka mwilini kama viuvimbevimbe hv ameenda tena hospital wamempima wamesema hamna tatizo.please doctor Nkingwamh naomba msaada wako.
 
Doctor,
nina tatizo la kusumbuliwa na uchovu na maumivu ya mwili mda mwingi, hasa wakati wakuamka asubuhi, baada ya tendo la ndoa nasikunziima mbele, au baada ya kufanya kazi nzito yani kubebabeba vitu vizito.
 
Habari za wakati huu Daktari.

Kwanza kabisa natoa shukurani za dhati kwa elimu unayoendelea kuitoa kwa umma.

Naomba kufahamu faida na hasara za kuoga kwa kutumia maji ya baridi vs maji ya moto kitaalamu zaidi kwa watu wazima..... wake kwa waume.

Asante.
Habari msweet😛ole kwa kusubiri Nilikua nimetingwa kidogo ofisini so ikanilazimu kutokuendelea kujibu maswali.
Ingawa ulikua nizamu yako naomba ni kujibu kesho. Kwani swali lako ni swali ambalo la elimu kwa Jamii kwa hivyo nisingependa nijibu kwa kifupi. Ninaonelea nifafanue ili Jamii nayo ipate elimu.
 
Back
Top Bottom