Mkuu kama matumizi yako ni madogo sawa hatukatai ila kuona 1TB ni nyingi kwa vitu vya 4k+ haupo sahihi.
CD moja tu ya Bluray yenye uwezo wa kucheza movie za 4k, ikiwa ni dual layer ni 50GB na ikiwa ni triple layer ni GB 100. Hivyo movie ya 4k ambayo sio compressed kwenye 1TB ni movie 10 mpaka 20.
Hapo hatujagusa HDR10+ (Hiyo simu inayo), 3D, mambo ya Virtual reality etc nayo yanakula GB za kutosha.
Ukija kwenye games, game hiyo hiyo unadownload wewe mb 500 ama 1GB kwenye simu zenye resolution kubwa kunakuwa na option ya HD textures inaweza kwenda hadi 4GB ama zaidi game moja.
Ukija kwenye miziki ili uenjoy quality nzuri za Hizi simu na Loseless codecs inabidi uachane na mp3 uende format kama flacs nyimbo moja tu inaweza kuzidi mb 200.
Kuna mambo mengi sana mkuu hio 1TB inakata faster.