Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Gharama zake? installation na monthly?
Kiboko yao ni kuFunga system ya Intruder Alarm kutoka KK Security / Gardaworld, ukipuliza dawa System hailali, akiingiza mkono au kichwa inapiga King'ora, hii inafungwa nchi nzima na unaweza kuchagua system itume sms kwenye simu ya watu wako wakaribu kadhaa, pia kwa ulinzi kamili ni kuunganisha system hiyo na control Room yetu ili pindi king'ora kinapolia wanatuma gari yenye Askari wa KK/Gardaworld kwaajili yakuangalia usalama kwenye eneo lako, inafungwa maofisini,nyumbani na pia inaweza kuunganishwa kwenye electricic fence yako. Wasiliana nami kwa WhatsApp number 0743171049 au email victor.valence@garda.com Nchi nzima.
 
Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!
Wanaume wa dar shida mtaa mzima mnapigwa ......hamna hata doria sinza yote imejaa misaloni na gym tu ni mwendo wa mascrub na masix packs tu bahati yenu wamewaachia marinda
 
Wanapokuja wezi kuwapulizia dawa ya usingizi kusudi mlale fofo na wizi ufanyike, fanyeni hivi kabla hamjalala!
Tia maji kwenye beseni lililo wazi kisha liweke chumbani kwako sehemu ya wazi, endapo wakija wakipulizia dawa tu, Yale maji yaliyopo kwenye ilo beseni basi litanyonya sumu yote iliyopulizwa humo ndani na kukuacha salama.
Na kwa njia iyo utaweza stuka mapema.
Kesho unaenda kunywa maji unakufa. Unakuwa umejiokoaa kuibiwa na unakuwa umepata nafasi ya kwenda mbinguni. Kuishi sehemu zisizo na ulinzi ni hatari sana
 
Nilifikiria kuja kupanga Sinza, kumbe ushenzini sana. Asante kwa taharifa mkuu. Plain A nimeifuta, naendelea na plan B mbezi beach au Goba
Goba na Makongo juuu sehemu angalau kwa Dsm kuishi
 
Kiboko yao ni kuFunga system ya Intruder Alarm kutoka KK Security / Gardaworld, ukipuliza dawa System hailali, akiingiza mkono au kichwa inapiga King'ora, na unaweza kuchagua system itume sms kwenye simu ya watu wako wakaribu kadhaa, pia kwa ulinzi kamili ni kuunganisha system hiyo na control Room yetu ili pindi king'ora kinapolia wanatuma gari yenye Askari wa KK/Gardaworld kwaajili yakuangalia usalama kwenye eneo lako, inafungwa maofisini,nyumbani na pia inaweza kuunganishwa kwenye electricic fence yako. Wasiliana nami kwa WhatsApp number 0743171049 au email victor.valence@garda.com Nchi nzima.
Bei gani
 
Wanapokuja wezi kuwapulizia dawa ya usingizi kusudi mlale fofo na wizi ufanyike, fanyeni hivi kabla hamjalala!
Tia maji kwenye beseni lililo wazi kisha liweke chumbani kwako sehemu ya wazi, endapo wakija wakipulizia dawa tu, Yale maji yaliyopo kwenye ilo beseni basi litanyonya sumu yote iliyopulizwa humo ndani na kukuacha salama.
Na kwa njia iyo utaweza stuka mapema.
Hii mbinu ilimsaidia jamaa mmoja pale Kibaha...ingawa sikuamini ila lisemwalo lipo...
 
Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!
DAWA NI MAJI TU.

Ile spray ikipulizwa kwny chumba chochote chenye maji yaliyo open kwa mfano kwny ndio au karai inafyonzwa yote kwenye maji.

Hata ulaya kuna wakati walikuwa wakiibiwa hivyo.
 
Kuna jamaa yangu alikuwa kampuni moja ya ulinzi, kila asubuhi akirudi anakuta jamaa wameiba hata suruari,

Akawa anaweka umeme 'live wire' kwenye nondo kwa ndani.

Tangu siku alipokuta yebo yebo dirishani hiyo tabia iliisha hapo.
Aisee kuna watu makatili duniani
 
tegesha chupa kwenye nyavu hakikisha unazibananisha na nyavu wakitaka kutoboa zitadondoka na kupiga kelele
 
Sitasahau siku tulipo ibiwa nyumbani nikiwa na babu yangu chumbani mimi nikiwa kadogo nazani ni mwaka 1993.Hii ya madawa kupuliziwa ilikuwa haijawa insu sana kwa miaka ile ila ndo ilitutokea.

Kutokana na mazingira ya kijijini, mzee wetu alikuwa ana nyumba zaidi ya moja hapo nyumbani na sisi kama wajukuu tulikuwa tukilala na babu mimi pamoja na kaka yangu.Asubui baada ya kuamka ndo tukagundua kuwa tumeibiwa. Babu alikuwa na bunduki moja ambayo alikuwa ameiegemeshea ukutani karibu na kitanda,magunia kama manne ya mpungu na mahindi,wakachukua na vitu vingine vidogo dogo, tuliamka saa mbili asubui tena kwa kuamshwa maana haikuwa kawaida ya mzee kulala usingizi wa namna hiyo, kawaida yake yeye alikuwa mtu wa kukaa macho sana wakati wa usiku kutokana na hali ya kuwa na mifugo hapo nyumbani.

Babu alishangaa, alisema mara moja tu alipo amka" tumeibiwa" kuangaria bunduki haipo kutoka nje mlango umevunjwa sijui na mashine gani hiyo. Polisi wakaja wakamchukua babu hadi kituoni baada ya kuangalia mazingira ya huo uporaji.Walienda kumuweka hapo kituoni lakini mkuu wa kituo sijui na nani wakasema haiwezekani mzee kufunguriwa mashitaka kwa kosa la upotezefu wa siraha, mana wengine walijaji ya kwamba huenda ameamua kuiuza kwa majambazi kwa kuwa amezeeka,ila huyo jamaa alikataa akasema huyu mzee kamiliki silaha tangu serikali ya mkoloni na ameshirikiana na sisi aiku nyingi kwa mambo ya kiusalama haiwezekani kumhisia vibaya katika tukio hilo, ikabidi wamuachie, wakamrudisha home mida ya saa nne usiku. Hiyo bunduki ilikuja kukamatwa na polisi katika tukio moja la kijambazi ikiwa imekatwa ule mtutu na kuwa fupi, yani ikipigwa risasi mita mia tatu utazani imepigiwa mgongoni mwako.

Sifa ya mzee ilikuwa ni shabaya, alikuwa mlengaji, sniper, hakuna wa kuweza kumfuata kwa uwezo wake na hivyo alikuwa akitumika a serikali kwa mambo ya kupiga wanyama waliotoka hifadhini na kuanza kuleta madhara kwa raia, mana mnyama mkari ilitakiwa umpige kichwa na ukikosea ukapiga hewa hapo kitimu timu lazima kiwepo mana na yeye anaanza kujihami, walio kaa kalibu na mapori wanajua, utasikia anasema nina hasira kama nyati aliyekoswa na risasi. Sasa huyo mzee alikuwa nauwezo wa kupiga kichwa cha mnyama hata kama anakimbia.
Mara ya mwisho alimpiga mwewe aliyekuwa anachukua vifaranga vya kuku alikuwa ametuakwenye mti pembeni na nyumbani,alipigwa kichwa kikasambaa kwa risasi, yani ilibaki shingo tu kichwa hakipo,wakamchokonoa kwa selele yale ma miti malefu yanayoota katikati ya katani ndo akaanguka mana alikuwa amenasa miguu yake ivo ivo kama alivyokuwa hai kule mtini. R.i.p babu yetu.
 
Wakati DC wa Kigamboni anasema kwa nia njema tu akikamatwa kibaka avunjwevunjwe miguu watu walimtukana humu,ooh haki za binadamu sijui nini. Haya sasa.

Mimi naamini mwizi sio wa kuhurumia hata kidogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom