Kariakoo: Kiongozi wa Wafanyabiashara azomewa

Kariakoo: Kiongozi wa Wafanyabiashara azomewa

Hata makonda wa daladala wangegoma PM angeenda, coz hakuna mkubwa zaidi ya mwenzake

Kariakoo kuwa na wafanyabiashara wenye mtaji mkubwa haimaanishi wanaweza kupinga sauti ya mamlaka

Pm si kaenda Jana? Na akawaomba wafungue maduka, na mkutano mwingine ni kesho? Sasa kinachofanya Leo wasifungue ni kitu gani?

Why Jana walikubali mbele ya PM

Hata kama ikiwa wanachangia 80% ya pato la Tanzania hawana mamlaka ya kutotii agizo la waziri mkuu

Wamefanya ujinga
Karia koo Hawajawahi kugoma na ukiona wamegoma jua kuna jambo la maana. Waswahili wanasema ukinuna uwe na sababu. Wafanyabishara wa Karia koo sababu wanayo. Mimi nafahamu ilo kwasababu i am a business man.
 
Je nisawa kumshinikiza rais wa inchi aje kariakoo?

Je ni Sawa kukataa maagizo ya Waziri mkuu wa inchi?
 
Je nisawa kumshinikiza rais wa inchi aje kariakoo?

Je ni Sawa kukataa maagizo ya Waziri mkuu wa inchi?
Kwa heshima na taadhima Ni sawa kabisa kwani halipwi mshahara? Yeye si mtumishi? Rais anatakiwa kuvaa viatu vya watu anao waongoza na sio kuogopa kukutana nao. Uzuri wa jambo ni kulizungumza.
 
Kwa heshima na taadhima Ni sawa kabisa kwani halipwi mshahara? Yeye si mtumishi? Rais anatakiwa kuvaa viatu vya watu anao waongoza na sio kuogopa kukutana nao. Uzuri wa jambo ni kulizungumza.

Kuzungumza si Jana mlizungumza? Na kikao kingine ni kesho?

Kama mlikuwa hamtaki kauli ya serikali why mlienda kwenye mkutano wa waziri mkuu?

Why Jana pale kariakoo hamkusema kuwa hamtaki mpaka rais aje?

Na Rais hatokuja, ili muendelee kugoma then tuone Nani ataufyata
 
Taasisi zote zina kero, kuna watu wanapasua wagonjwa hawana hata vifaa vya kujikinga mpaka na wao wanapata magonjwa mengine je hiyo sio shida kubwa? Tukigoma kufanya kazi si wagonjwa wengi watakufa ?

Sasa Rais kamtuma waziri mkuu, amekuja na amewaomba, na mkutano mkubwa ni kesho, then mpaka Leo mnagoma for what?

Kama hamuamini kauli ya waziri mkuu how mtaamini kauli ya Rais ?

Wazo Bora ni kuachwa wagome hata miaka 2 then tuone

Na Rais ikimpendeza maduka yote yavunjwe kuwe open space, kuna shida Sana ya parking mjini

Au tufuge samaki tu
Itoshe kusema mawazo yako ni ya kipopoma.
 
Makusanyo Kwa Nchi nzima bl 800, KARIAKOO pekee inachangia bl 300.

Una akili wawasawa kuwaza kuwa unaweza kwenda bila KARIAKOO?
Acha ujinga, hiyo 300bn Kkoo ni kwa mwaka mzima wakati makusanyo ya Tra kwa wastani kwa mwezi saivi ni 1.5tr. Ndio, Kkoo pana umuhimu ila sio engine ya mapato, hata wakigoma kwa mwezi mzima italeta inflation tu ya bidhaa mtaani na wajanja wengine watatumia hiyo fursa kupitisha hizo bidhaa mtaani.
BTW, maduka ya wachina Ubungo yanakaribia kukamilika, Kkoo itakuwa na mbadala na tishio kubwa, hakuna haja ya kwenda China , kila kitu kitaletwa Ubungo, Kkoo inaenda kupotezwa na ushindani unaokuja wa wachina Ubungo.
 
Akizungumza na Wafanyabiashara wenzake wa Kariakoo, Ndugu Mbwana ambaye anatajwa kama kiongozi wa wafanyabiashara hao amewaasa Wafanyabiashara wote wafungue maduka yao kwa vile Waziri Mkuu alielekeza hivyo na kwamba Jumatano kutakuwa na Kikao kati ya Viongozi wa wafanyabiashara na Waziri Mkuu.

Baada ya kauli yake hiyo Ndugu Mbwana AMEZOMEWA KWA KISHINDO KIKUBWA hadi sauti ya wazomeaji kufika Magomeni na Feri, kuzomewa ni Ishara ya kukataliwa na ni aibu kwa aliyezomewa na kwa uungwana, ukishazomewa namna kama alivyozomewa Mbwana unapaswa kujiuzulu.

Ushauri wangu kwenye sakata hili ni huu hapa, Waliofunga maduka yao kusubiri kauli ya mwisho ya Serikali ambao ni 98.9 % waache wafunge hadi wanachosubiri kitimie lakini hao 1.1% ambao wamefungua maduka yao wasisumbuliwe

Namshauri RPC Murilo asijaribu kuwatisha waliofunga kwa sababu vitisho vyake vitachafua zaidi hali ya hewa na akifanya mchezo tutahakikisha anahamishwa kabla ya asubuhi kama tulivyohakikisha Pedeshee Amos Makalla anatimuliwa kabla ya asubuhi, Mgogoro huu umeishavuka level ya Polisi, aache ngazi za juu ziutatue kwa weledi, Yeye anachopaswa kukifanya ni kuimarisha Ulinzi Baaaaasi.

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Hawakumzomea wakati wa speech,just a little murmuring. Lakini haijulikani kama wamefunga maduka au vipi.
Kamanda Muliro anasema wanaotaka kufunga wafunge,watakaofungua maduka atawalinda.
Itakuwa vizuri kuitazama tu hii game inavyoendelea badala ya kujaribu kumtisha Kamanda Muliro.
Serikali inalitanzua hili tatizo kwa mabavu jambo ambalo watu wengine jana walikuwa wanasema halifikiriki.
Sasa tuseme tu kwamba hali ni tete.
Kama jahazi limeondoka bandarini huwezi kutoa last minute advice kwa nahodha . Mchakato wa kuwathibiti hao wagomaji umeanza,kwa hiyo wewe tazama kitakachitokea,acha maneno maneno.
 
Dawa yao Rais awanyamazie kimya ili aone mwisho wao kama hawajafungua wenyewe,serikali ikishaanza kukubali kupangiwa na wapuuzi wachache watavuruga kila eneo nchi sasa itakuwa ni migomo na kila anayegoma atadai kuonana na Rais.
Mbona siku zilizopita walifanyiwa kila aina ya dhuluma lakini hatukuwahi kumuona mjusi yeyote akibinua makalio yake na kubana pua eti anagoma leo Rais amewaondolea adha chungu nzima ikiwemo madeni ya kodi ya mchongo bado mnataka kumchukulia poa!
Mkuu haujui kitu ukisemacho.

Achilia mbali miezi, hapo mgomo ukiendelea wiki mbili tu, athari zake ni kubwa na kwa nchi nzima.

Sekta zote zitaguswa, Mabenki yatayumba, Miamala mpesa, tigo na wenzao wote watalia. Sekta ya usafirishaji itakuwa taabani n.k.

Kwa taarifa yako hao wakigoma mwezi wanaiangusha serikali.
 
Haya waambie wagome mwezi mzima kama hawajatoana roho wenyewe kwa wenyewe,jana na leo tayari wameanza kugawanyika sembuse wiki hawa majuha wanatingisha kiberiti tu.
Eti ooh serikali itaanguka! Wao watabaki salama wajaribu waone kati yao na serikali nani ataomba poo.
 
Nakusahihihisha mkuu Mzomeo mimi nilipishana nao Bunju B pale na ulipita kwa kasi kweli kuelekea Bagamoyo.
 
Hata makonda wa daladala wangegoma PM angeenda, coz hakuna mkubwa zaidi ya mwenzake

Kariakoo kuwa na wafanyabiashara wenye mtaji mkubwa haimaanishi wanaweza kupinga sauti ya mamlaka

Pm si kaenda Jana? Na akawaomba wafungue maduka, na mkutano mwingine ni kesho? Sasa kinachofanya Leo wasifungue ni kitu gani?

Why Jana walikubali mbele ya PM

Hata kama ikiwa wanachangia 80% ya pato la Tanzania hawana mamlaka ya kutotii agizo la waziri mkuu

Wamefanya ujinga
Na mkileta ujinga hata leo J5 hatufungui, akili iwakae sawa
 
Back
Top Bottom