Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.
Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..
Pengo... utafanya nini....
Binafsi nisingependa kuweka hisia binafsi kama Mzee Mwanakijiji ulivyofanya bila kufanya utafiti, labda umebuni au kuambiwa napengine kuyachukua ya vijiweni.Kanisa haliendeshi shughuli zake kiasa bali kiimani na kwa busara ya hali ya juu kwa kufuata kanuni zake.
Nina mashaka kama Mzee Mwanakijiji unajua utaratibu wa Kanisa Katoliki, kama hujui bora ungeuliza kwa wanaofahamu wafahamishe.
Anavyoropoka Aux. of Bukoba Kilaini ni kinyume cha taratibu za kanisa. Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa kauli iliyoakisiwa na balaza la Maaskofu Katoliki pale Tanzania Episcopal Conference, ni kauli ya pamoja chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Baraza hilo ambalo Cardinal ni member. Hana utaratibu kila askofu au Cardinal kuibuka na kutoa matamko katika mambo mazito kama haya. Naona umeteleza Mzee Mwanakijiji.
Wakatoliki hawakurupuki tu kutoa kauli, wanatulia, wanakutana kushauriana na kupima cha kuzungumza na ndipo kauli inayotolea inaeleweka kwa kila mmoja wao kwa msimamo wa pamoja si mtindo wa wengine kusikia kwenye vyombo vya habari.
Canon Law ndio msingi wa uongozi si cheo cha mtu katika ukatoliki
