Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.
Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..
Pengo... utafanya nini....
Mm, ni kama tunahitaji Zaidi ya kauli ya Pengo, tunahitaji mjadala na muafaka wa kitaifa juu ya Nafasiya dini ya mtu katika mfumo wa U-Tanzania,
1. Waislam wamelalamika sana uonevu wakati wa Mwlm Nyerere,, sisi kama Taifa tume-Li-address vipi hilo
2. Wakristo wamelalamika sana kila atawalapo Rais Muislam, kama Taifa tume-address vipi?
3. Waliuliwa wapemba katika chaguzi, tumefanya nini kama Taifa
4. Mwembechai?
5. Hizi MOU zinazolalamikiwa kila Siku, ni nani ndani ya Serikali amejaribu kulieleza, walau kauli?
6. Baraza la mitihani?
7. Uteuzi wa upendeleo?
8. Kuongezeka kwa Taasisi za Kikristo, hasa vyuo vikuu, je Tuna sera inayopaswa kuratibu ongezeko hilo
10. Manung'uniko yanayoendelea katika pande zote juu ya nani anaiibia nchi?
11. Kuchinja wanyama,, au ya Pinda, wasira, yanatosha?
By the way unaweza kuwa na Taifa lisilo na common values? Inawezekana kama Taifa ndo mwanzo wa kudadisi what are our.values.
Sidhan Kauli ya Pengo itajibu hayo