Kardinali Pengo, Simama au na wewe staafu kama yamekuzidi...

Watu wa Mungu hawapayuki ovyo ovyo. Wanafanya tafiti kabla hawajasema. Pengo hawezi kuanza kupiga kelele ovyo ana washauri wake na itakapofika muda wake wa kuongea utamsikia. Je, hukuona kele mwanza wakati wa msiba wa marehemu askofu mkuu Mayala? Mimi nashauri, kanisa lifanye mafungo ya siku 9 kulaani vitendo hivi,kama serikali imeshindwa kufanya kazi. Tutaona mwisho wao.
 
HOJA NZURI SANA, ILA Shida yangu na hoja ya MMM ni moja tu, kusema staafu... binafsi naona umeleta siasa. Kinachotakiwa ni sisi kumdai Pengo ahadi aliyotuahidi ya kulinda, kuongoza na kuwakilisha.

Pengo anatakiwa kusimama na kuwajibika, alipewa daraja lile kwa kuwa na sifa na vipawa fulani, basi atuonyeshe.... Dini, wajibu, busara na haki hazina mbadala... hazina blahblah.

TUNAMUOMBEA KILA SIKU NA KWENYE KILA SALA, SIDHANI KAMA HUWA TUNAMUOMBEA AWE BUBU, MPOLE NA MWENYE KUGUBIKA KOMBE
 
Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.

Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..

Pengo... utafanya nini....

USIDHANI Kiongozi huyu mwenye hulka ya upole anafurahia haya au hakuna juhudi yoyote ile anayofanya eti kwa sababu tu hatoi matamko hadharani. Hata JK anajua wazi ya kuwa AMANI ya Taifa hili kwa sasa imeshikiliwa na maaskofu. Nadhani kiongozi huyu anachokionesha ni hali ya juu ya busara alizonazo.
 
HOJA NZURI SANA, ILA Shida yangu na hoja ya MMM ni moja tu, kusema staafu... binafsi naona umeleta siasa. Kinachotakiwa ni sisi kumdai Pengo ahadi aliyotuahidi ya kulinda, kuongoza na kuwakilisha.

Pengo anatakiwa kusimama na kuwajibika, alipewa daraja lile kwa kuwa na sifa na vipawa fulani, basi atuonyeshe.... Dini, wajibu, busara na haki hazina mbadala... hazina blahblah.

TUNAMUOMBEA KILA SIKU NA KWENYE KILA SALA, SIDHANI KAMA HUWA TUNAMUOMBEA AWE BUBU, MPOLE NA MWENYE KUGUBIKA KOMBE
Binafsi nisingependa kuweka hisia binafsi kama Mzee Mwanakijiji alivyofanya bila kufanya utafiti, labda amebuni au kuambiwa na pengine kuyachukua ya vijiweni.
Kanisa haliendeshi shughuli zake kisiasa bali kiimani na kwa busara ya hali ya juu kwa kufuata kanuni zake.


Nina mashaka kama Mzee Mwanakijiji anajua utaratibu wa Kanisa Katoliki, kama hujui bora angeuliza kwa wanaofahamu wamfahamishe.

Anavyoropoka Aux. Bishop of Bukoba, Rt Rv. Methodius Kilaini ni kinyume cha taratibu za kanisa. Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa kauli iliyoakisiwa na balaza la Maaskofu Katoliki pale Tanzania Episcopal Conference, ni kauli ya pamoja chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Baraza hilo la TEC ambalo Cardinal ni member. Mwadhama Pengo hana na pengine kila askofu au Cardinal kuibuka na kutoa matamko katika mambo mazito kama haya. Naona umeteleza
Mzee Mwanakijiji.

Tamko lolote litolewalo na Askofu linaeleweka kama tamko la Kanisa Katoliki, ndio maana wana utaratibu wa kutulia kwanza, kusoma na kupata vyanzo mbalimbali vya habari, na tamko linapotolewa linakuwa limesheheni ukweli na hali halisi, si mampo kama ya kisiasa ya papo kwa papo halafu kesho unajutia sikujua.

Wakatoliki hawakurupuki tu kutoa kauli, wanatulia, wanakutana kushauriana na kupima cha kuzungumza na ndipo kauli inayotolea inaeleweka kwa kila mmoja wao kwa msimamo wa pamoja si mtindo wa wengine kusikia kwenye vyombo vya habari.

Canon Law ndio msingi wa uongozi si cheo cha mtu katika ukatoliki
 
unataka afe padre gan ndo ujue sio mapema? Achen ushabik kwenye ishu za msingi
​Usiwe unakurupuka kama kuku anayeatamia! Ushauri niliyoutoa una ushabiki gani?! Tumia ubongo kufikiri siyo kinyesi!
 
Inawezekana naye ni 'dhaifu'. Kuna mambo hayatakiwi kuwa. Msipoangalia convent ya watawa itavamiwa watu watachinjwa halafu atakuja mtu kutupa hotuba ya 'jamani udini kitu kibaya'. Ngoja tumwone atakavyoanza kumuita Nyerere "Baba wa Taifa"...

Nasita kuamini kama ni kweli umeandika uzi huu....kuna mdau aliwai kusema anashaka na identity ya MM kwa siku za hivi karibuni.Hata mimi napata shaka hiyo sasa.

Kama ungefanya utafiti wa kutosha hasa kuhusu misingi ya kanisa katoliki naamini usingefikia uamuzi wa kutaka matamko ya kiongozi kama pengo.

Je ,unatambua kuwa kanisa katoliki limejengwa katika amri kuu mbili nazo ni Mpende Mungu wako kwa moyo,uwezo na akili yako yote na pia Mpende jilani yako kama nafsi yako mwenyewe. Je Unatambua kuwa Msamaha ni nguzo kuu ya kanisa katoloki, na hukumu hutolewa na Mungu pekee kwa mujibu wa imani katoliki.

Katika misingi hii Pengo hawezi kutoa tamko lolote zaidi ya kuwaagiza mapadri wote kuendelea kuhuburi msamaha kwa wote wanao hujum kanisa pia kuwaomba waumini kuendelea kuishi kwa upendo na watu hawa kwani Mungu atawahesabia hukumu yao siku ya mwisho.Kwa taarifa yako matamko haya hutolewa kila jumapili kanisani.

Yesu alisema ufalme wake ungekuwa wa dunia hii angekuwa na jeshi la kumlinda, kwa misingi hii kanisa katoliki halina ufalme katika dunia hii na pia Pengo hayuko kimya kwani anaendelea Kuhubili neno la Mungu akisisitiza upendo na amani kila jumapili.

Je wakati saul(POUL) alipokuwa anachinja wakristo kama kuku PETRO kama mkuu wa kanisa alitoa TAMKO? au wakati Kaisari NERO alipoua wakristo zaidi ya laki moja umewai soma popote kuwa kuna tamko lilitolewa? ya kaisari Pengo anamwachia kaisari na Ya Mungu atawasisitiza waumini kwa matamko tena makubwa wampe Mungu.

Ukristo si dini ya visasi, uchichezi na malipizi hivyo usitegemee tamko la papa,kadinari au paroko pia ungemuomba msamaha kwa kusema anakula na kunywa na wakubwa, kwani si makosa kufanya hivyo..Hata YESU alikula na kunywa na wakubwa..akiwemo ZAKAYO mtoza kodi aliyemuandalia sherehe kubwa tuu.
 
inawezekana naye ni 'dhaifu'. Kuna mambo hayatakiwi kuwa. Msipoangalia convent ya watawa itavamiwa watu watachinjwa halafu atakuja mtu kutupa hotuba ya 'jamani udini kitu kibaya'. Ngoja tumwone atakavyoanza kumuita nyerere "baba wa taifa"...

pengo naye dhaifu tuu ndo maana alimpiga vita msaidizi wake kilaini!
 
Nasita kuamini kama ni kweli umeandika uzi huu....kuna mdau aliwai kusema anashaka na identity ya MM kwa siku za hivi karibuni.Hata mimi napata shaka hiyo sasa.
Kama ungefanya utafiti wa kutosha hasa kuhusu misingi ya kanisa katoliki naamini usingefikia uamuzi wa kutaka matamko ya kiongozi kama pengo.
Je ,unatambua kuwa kanisa katoliki limejengwa katika amri kuu mbili nazo ni Mpende Mungu wako kwa moyo,uwezo na akili yako yote na pia Mpende jilani yako kama nafsi yako mwenyewe. Je Unatambua kuwa Msamaha ni nguzo kuu ya kanisa katoloki, na hukumu hutolewa na Mungu pekee kwa mujibu wa imani katoliki.....
mKUU VYOVYOTE UTAKAVYOSEMA MBONA HAONGEI LOLOTE ANATAKA MASS IAMUE YENYEWE, TUMECHOKA KUONEWA!
 
Binafsi nisingependa kuweka hisia binafsi kama Mzee Mwanakijiji alivyofanya bila kufanya utafiti, labda amebuni au kuambiwa na pengine kuyachukua ya vijiweni.
Kanisa haliendeshi shughuli zake kisiasa bali kiimani na kwa busara ya hali ya juu kwa kufuata kanuni zake.


Nina mashaka kama Mzee Mwanakijiji anajua utaratibu wa Kanisa Katoliki, kama hujui bora angeuliza kwa wanaofahamu wamfahamishe....

mKUU NAKUBALIANA NA WEWE LAKINI WALIKUWA WANASUBIRI PADRI MUSHI AUWAWE?
ALIKOSWAKOSWA PADRE AKAVUNJWA TAYA MBONA HAWAKUSEMA LOLOTE?
KUWA MWEMA SANA NI HATARI MKUU! LABDA TUSEME NAO NI DHAIFU TUU!
 
Napenda kutanguliza shukrani zangu sana kwa wana JF wote na kutoa Pole zangu sana kwa ndugu zetu wakatoliki wote ambao wamempoteza askofu wao zanzibar.

Kwa kweli nasikitika sana kwa baba yetu Mhadhamu askofu polycarp pengo kushindwa kutoa tamko na maelekezo kwa serikali ya ccm kuhusu mauaji yanayoendelea zanzibar.

Tumeona hivi karibuni askofu wa anglikani na lutherani wakitoa matamko yao katika kulaani mauji ya kidini yanayoendela lakini baba askofu pengo yupo nyuma katika kutoa tamko.

Principal wanasema kimya kingi kina mshindo kwa mapendekezo yangu binafsi napenda kusikia kauli ya baba askofu kwa serikali ili tusije ona mauji ya kidini yakiendelea.

Asanteni sana
 
naogopa sana tunapoelekea, inaninyima haki yangu ya msingi yakuabudu napokuwa Zanzibar coz sijui ni lini watachoma kanisa likiwa na waumini ndani yake, kiukweli Tanzania ya sasa wakiamka wazee wetu waliofariki miaka kumi na tano iliyopita na kuona hali yrtu ya sasa nahisi swali la kwanza watamuuliza Mungu mbona kawafufulia SOMALIA???
 
Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.

Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..

Pengo... utafanya nini....


Kanisa katoliki lili crash liberation theology kwa kuwa ilichanganyika na marxism na political activism na hivyo ndivyo ilivyo leo...Pengo hawezi kujiuzulu.....
 
Kauli na Matamko haya yamesaidia nini?...Mimi naona kama yanaweka petroli kwenye moto!
Mbagala walitoa matamko, umeona jipya?
 
sure kama kiongozi lazima awe imara tena madhubuti....maana awa jamaa watazoea
 
kiukweli tumechoka kuona teki na pengo wapo kimya tunataka tamko na utekelezaji wa matamko kama wameshindwa watwambie tuingie barabarani make hatuwezi kukubali viongozi wetu wa kidini wanauwawa kila siku

mkuu nakuunga mkono nimechoka na hii tec yao! Mpaka wafe wao!
 
kauli na matamko haya yamesaidia nini?...mimi naona kama yanaweka petroli kwenye moto!
Mbagala walitoa matamko, umeona jipya?
mkuu mbona mauaji hayazimwi!?
Hapa nikuonyesha kuwa tumechoka na mimi kama mimi nimecha na uovu huu!
 
Cardianl pengo kama umeshindwa hiyo kazi mpe fr.baptist mampunda,ruwaichi sasa ndio najua kwa nini ulimhamisha askofu methodius kilaini alikuwa anakufunika kiutendaji,baraza la maskofu mko wapi mnataka tuingie kanisani na bullet proof????
 
Kweli! Something has to be done. Ila tumefika hapa tulipo kutokana na mafundisho tunayoyapata katika nyumba za ibada. Wahubiri/Mashehe badala watangaze mazuri ya dini zao wao wanatumia muda mwingi kusema dini zenye msimamo kinyume na wao. Kila dini inajiona bora kuliko nyingine. Hali ni mbaya zaidi kwa wenzetu wa kiislamu, kwa kweli wanakosa uvumilivu. Huwa napenda kusikiliza radio Imani na haya yanayotokea ni reflection ya ninachokisikia. Huwezi amini radio ni ya waislamu lakini huenda wanataja ukristo mara nyingi kuliko wanavyotaja uislamu! Mpaka nikajiuliza, hivi kama serikli ilifungia gazeti la mwanaHalisi kwa sababu za uchochezi (kama wasemavyo), serikali hiyo inasubiri nini kuifungia radio imani kwa sababu hizo hizo?

Nina uhakika angelikuwa Shehe kauwawa hapa, sasa hivi pengine tungekuwa tunazungumza mengine.
Vitendo hivi vinapaswa kukemewa na watanzania wote
.

hapo kwenye nyekundu panaonesha kuwa ama umri wako ni mdogo au huwa hufatilii matukio yanayotukia hapa nchini.
waislamu wameshauawa sana na bunduki za serikali ya tanzania. waliwahi uwawa mwembechai. zaidi ya watu 10 walipigwa risasi na wengine kusababishiwa ulemavu hadi leo. kule znz katika maandamano ya cuf waliuawa zaidi ya waislamu 70 tena wengine walifuatwa misikitini. naomba uwe na kumbukumbu nzuri za kihistoria. kipindi cha mwalimu aliwafukuza masheikh wengi hapa nchini wakaishi wanakokujua. sheikh hassan bin amiri, sheikh abdallah saleh farsy na wengineo.

kuhusu suala la mauaji ya padre jana kule znz, kila mpenda amani LAZIMA alaani jambo hili. padre ameuawa bila hatia! waislamu walipigwa risasi waziwazi na askari wa JWTZ pamoja na polisi. kuhusu padre hatujajua mhusika hadi muda huu. serikali ifanye uchunguzi wa kina kubaini wahusika. niliwahi sikia kuwa miji yetu imewekewa street security cameras. sijui zipo au yalikua maneno. ktk nchi zilizoendelea, kamera za mtaani husaidia sana kubaini wahusika wa vitendo vya uhalifu. ni muda muafaka sasa, tuingie gharama ya kufunga vifaa vya ulinzi katika mitaa yetu.

kubwa zaidi ni kwa viongozi wetu wa dini kuhubiri upendo na umoja. serikali pia ijaribu kusikiliza wananchi kuhusu malalamiko mbali mbali. kama wa znz hawataki muungano, basi tuuvunje. kama kuna malalamiko ya waislamu kuhusu mambo mbalimbali, serikali ikae nao meza moja na kuyazungumza. kupuuzia matatizo ya kundi mojawapo katika jamii ni kupalilia uhalifu na ugaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom