Karantini na changamoto zake

Karantini na changamoto zake

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
18,684
Reaction score
45,616
Nawasalimu wooote wote kwa jina la yeye mwenye mamlaka mbinguni na duniani. Baada ya salamu hiyo naomba nicheke kidogo japo kwa majonzi😃😢😃😢😢😂😂😤 Corona imebadili baadhi ya mifumo yetu ya kimaisha na sijui mwisho wa janga hili la kidunia ni lini maana watu wanayoyafanya Mh! Mungu aturehemu tuu kwakweli😔😔😓

Leo kuna changamoto niliyoguswa nayo na hii ni hasa kwa wanandoa na wale sogea tukae😩 sio siri kukaa "Karantini" hasa ya nyumbani sio mchezo kwa wale wenye hii changamoto. Kuna baadhi ya wanandoa au wale sogea tukae wanaweza kuelewa. Matumizi na usafi wa Maliwatoni/Msalani hivi unawezaje kumvumilia mtu mume au mke ambae akiiingia hilo eneo lazima aache udambwidambwi hawezi kuacha eneo hilo kama alivyolikuta likiwa safi?

Hii nimesikia ni kwa Wanaume sana sana hawajali haya masuala ya usafi wa haya maeneo kabisaaa, LOL. Sasa wakati huu wa kujifungia ni balaa watu wananuna jomonii mpaka basii. Hebu wababa jitahidini kutunza yale maeneo wengine mnatumia "self contained" lakini unakuta Maliwatoni haivutii kabisaa na mama/mke asipokuwepo uuwwiii unaweza hisi ni chumba kidogo cha mizimu😧


Hivi huwa mnawaambiaga au mnamezea tuu mnaingia kuclean wenyewe maisha mengine yaendelee? Maana wote tunajua umuhimu wa lile eneo na raha yake😉hasa likiwa safi na kavu.

Muwe na karantini njema, tuendelee kujilinda na kuwalinda wengine,.

~MC~
 
Umetusingizia kwanza wanaume hatuingiagi chooni wala hatujisaidii hiyo nikazi ya mama mwenye Nyumba
 
Naona umeamua kumsema mume wako kwa kutuvisha lawama hata sisi tusiohusika ila poa tu

GunFire
 
Back
Top Bottom