Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,269
- 675
Wana Jamvi
Niko jimboni Karagwe kama mwangalizi wa Uchaguzi (TEMCO).
Hivi sasa kikosi cha FFU kutoka Bukoba kimeingia na kuanza kurusha mabomu ya machozi mengi.
Kuna watu wapatao kama elfu kumi wamezingira ofisi ya tume wakidai itangaze matokeo ya ubunge.
Mabomu yameisha na sasa polisi wanatumia risasi za moto hewani. Watu wameumizwa na wengine wanakimbizwa hopsitalini.
Kuna tetesi kuwa Mgombea wa Chadema DEUSDEDITH JOVIN KAHANGWA amemshinda BLANDES GOSBERT wa CCM, lakini wakubwa wanakataa asitangazwe, bali Blandes ndiye atangazwe. Msimamizi wa Uchaguzi amejitahidi kukataa pressure kutoka kwa wakubwa lakini yaelekea sasa ananyonya mikono ili atangaze ushindi bandia kwa CCM. Hapahitajiki mabomu kumtangaza mgombea Chadema hapa maana maelefu ya watu wamekodi mafuso kuja kumlaki mbunge wao waliyemchagua.
Asante mkuu