Kapuya Matatani: Adhibitiwa na kitoto kinachodai alikibaka, akakiambukiza virusi

AKUDO IMPACT+

7515210_orig.jpg

 
hamna kesi hapo, mlalamikaji amejipeleka/anajipeleka mwenyewe. Pamoja na kuwa ni yatima.. matatizo yake yasimfanye kuwa mtumwa.

hii imekaa kama black mail.. kwanini hawakulalamika baada ya tukio la kwanza?? kinacholalamikiwa hapa sio ubakaji bali kusitishwa kwa huduma.
 
Hawa wasichana nao,
Kwanini mara ya kwanza hakusema;
Hapa kilichomfanya achanganyikiwe ni ile kuambiwa kuwa mzee ana maradhi;

Haya ndo watoto tuliowazaa sisi wenyewe lakini;
Sijui hata maneno ya kusema hapa.
 
kwa habari ilivyo wote wana shida kabsaaaa!waziri wa zamani na huyo binti!mimi ni mzazi lakini nachoona hapo ni upuuzi kabisa,alipobakwa (kwa maelezo yake on which sikubaliani nae kwani inaonyesha alireact alipoambiwa baba huyo ana HIV),alipaswa kushtaki kitu ambacho anadai alifanya na walipofika polisi wakakubaliana jambo ambalo alilitekeleza,aliposema wauze gari ili amalizie shule hao mabinti walitaka huyo baba awahudumie mpaka kufa kwao?WOTE WAPUUZI KABISA.

Yes wanamfanyia Mzee "blackmail" ya nguvu. Mtu ulibakwa 2011 halafu kelele unaanza kupiga 2013. Huyu binti kuna mtu yuko nyuma yake sio siri. Kwa kusema hivi haina maana kwamba naunga mkono alichokifanya huyo Bwana mkubwa.

Tiba
 
MMOJA wa mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tatu na mbunge anayetoka Mkoa wa Tabora, anatuhumiwa kumbaka na kisha kutishia kumuua msichana yatima mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa) anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo (jina lake linahifadhiwa kwa sasa), ametoa tishio hilo la mauaji kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia namba iliyosajiliwa kwa jina lake kwa kile alichodai kukaidi amri ya kutaka wasifichue uchafu wake kwa waandishi wa habari.

Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili, mwanafunzi huyo alisema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012.

Mwanafunzi huyo alisema alifikwa na ukatili huo alipoitwa na kiongozi huyo kwenda kuchukua fedha za ada na matumizi mengine, ambapo mara ya kwanza alimpa sh 700,000 na mara ya pili sh 350,000.

Yatima huyo anayeishi na dada yake, alikutanishwa na waziri huyo wa zamani na baba wa mwanafunzi mwenzake, kutokana na msaada mkubwa aliompa akiwa mgonjwa, ili aweze kumsaidia fedha za ada kama ishara ya shukurani.

Mwanafunzi huyo alisema baada ya kutambulishwa, aliitwa katika hoteli hiyo ambako baada ya kufika mapokezi wafanyakazi walimkataza kuingia chumbani kutokana na umri wake kuwa mdogo (mwaka 2011 alikuwa na miaka 14), lakini waziri huyo wa zamani aliamrisha aruhusiwe.

Akiwa chumbani, mwanafunzi huyo alilazimishwa kulala naye kisha kumpa sh 700,000, badala ya shilingi 67,000 alizohitaji kwa ajili ya ada.

Mwanafunzi huyo alisema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na kiongozi huyo katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012, ambapo pia alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha kumpa sh 350,000.

Mwanafunzi huyo alisimulia kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa wahudumu alimuuliza sababu ya huzuni yake na akalazimika kumweleza kisa hicho, ndipo mhudumu alitokwa machozi huku akimwambia kwamba, atakufa kwa sababu “baba huyo ni muathirika wa ukimwi”.

Aliongeza kuwa baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi, hadi alipokamatwa na walinzi, kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa mashitaka.

Hata hivyo, alisema polisi waliposimuliwa kisa chote, walilazimika kumwita waziri huyo wa zamani na alipofika alikiri na kuomba mambo yaishie hapo.

“Alikubali na akaahidi kunilipia ada na pesa za matumizi kiasi cha sh 300,000 kila mwezi, jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi (namba za simu tunazo),” alisema.

Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, Januari 24, mwaka huu walitishiwa maisha na kiongozi huyo, lakini mwezi uliofuata, mtu asiyefahamika alienda nyumbani kwao na kuacha gari (namba tunazo) aina ya Mercedes Benz yenye rangi ya bluu wakati akiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa maelekezo kuwa akifika apewe.

Wamesema baadaye kiongozi huyo aliwapigia simu kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa ajili ya matumizi, na wanaruhusiwa kuliuza ili wapate pesa za mahitaji yake siku zilizosalia, kwani baada ya uchaguzi mkuu 2015, atakuwa Waziri Mkuu, hivyo itakuwa ngumu yeye kumtumia huyo binti pesa kama alivyoelekezwa na Jeshi la Polisi kituo cha Oysterbay.

Hata hivyo, wasichana hao walishindwa kulitumia gari hilo hivyo kutoa taarifa polisi ili kesi ipelekwe mahakamani.

Wamedai kuwa polisi walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa katibu wa Bunge, ambaye alimwita mwanafunzi huyo na nduguye Dodoma kukutana na Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge.

Hata hivyo, walipofika Dodoma hawakuweza kupata ufumbuzi kwa maelezo kuwa waziri huyo wa zamani hakuwepo hadi Bunge lilipoisha. Kwa muda wote, wasichana hao walisema waligharimiwa kila kitu na Ofisi ya Bunge.

Kabla ya kurudi Dar es Salaam, mabinti hao walisema waliitwa na kiongozi mmoja wa juu wa CCM aliyewalekeza kwenda kumwona Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula.

Kwa mujibu wa mawasiliano, kiongozi mwingine (jina tunalo) alimpigia binti huyo simu majira ya asubuhi, akimtaka aende ofisi za CCM, lakini hakupata msaada wowote zaidi ya kuombwa asubiri hadi wakati wa kipindi cha Bunge ili apate msaada kwa kuwa ni suala binafsi.

Hata hivyo, wakati akiwa njiani kuelekea katika kituo kimoja cha runinga kwa ajili ya kutoa kilio chake, mwanafunzi huyo na dada yake walifuatiliwa na watu wasiowajua, jambo lililowalazimisha kuomba msaada wa wapita njia.

Hata alipofika katika ofisi za kituo hicho cha runinga, watu watatu akiwemo mwanamke mmoja walifika wakidai kuwa ndugu wa wasichana hao na kuwakataza waandishi wasikubali kusikiliza neno lolote, wakati sio kweli.

Chanzo cha habari,"Tanzania Daima", Eti waziri abaka! Ukisoma ooh,ni waziri wa awamu ya tatu! Scraaaap! Hilo ni gazeti au karatasi za kufungia vitumbua!
 
Lakini ilani ya chama si inaruhusu. Ongera Mh. Waziri wa zamani kwa kutekeleza ilani ya chama.

Ibara ya nane ya katiba Chadema inaruhusu kupora mke/mme wa mtu na kama mke/mme atahoji kimbiza yeye na watoto.
 
Back
Top Bottom