Maana yake kwako hata utawala wa kijeshi ni sawa tu.
Sasa hivi nchi ipo vitani. Maadui wa Tanzania ni Genge linaloongoza. Maadui wapo ndani ya nchi wameshika mifumo yote, nafasi zote za uongozi na kuziba njia zote za kidemokrasia za kuwaondoa madarakani.
Hawa maadui ni hatari kuliko hata Idd Amin, maadui wa nje. Wanauza nchi, bandari, misitu, mbuga, rasilimali za nchi kiholela na zingine kuchukua wenyewe kwa ubabe. Wanaua, kuteka,kutesa Watanganyika ukiwa na maoni tofauti na yao.
Wanatumia jasho, nguvu, kodi za Watanzania hovyo kwa manufaa yao binafsi na manufaa ya genge lao, sio kwa maslahi ya Taifa.
Wanafurahi kufungia mitandao ambayo inawapa kipato wananchi wengi. Maji, umeme, matibabu, usafiri ni shida, ajali kila siku, rushwa, ufisadi umekuwa kitu cha kawaida.
Hili genge linafanya haya maovu yote wakilindwa na Polisi, Mahakama, Bunge, TISS.
Hata jeshi likilinda mipaka ni kazi bure sababu nchi inauzwa na maadui wa ndani, hili genge linashambulia raia kila siku.
Jeshi halitakiwi kubaki neutral kwenye hali kama hii. Inabidi liwadhibiti hawa maadui wa ndani, kuwalinda raia, wazalendo ili kutoa nafasi kujenga nchi upya, mifumo mipya yenye manufaa, kuwalinda, kutoa haki kwa kila raia wa Tanzania. Hii ni moja ya kazi majukumu ya jeshi linalojitambua.