Kanumba ndani ya Big Brother House 2009

LOL... Stevieeeeee. nenda British kanseli

Mkuu FP,

Nadhani aanze na TUISHENI pale "perfect vision" ubungo! british kanseli anaweza kushindwa mtihani wa mchujo!

Aibu kubwa kwa wale wote waliomteua Kanumba kutuwakilisha BB..
 
tarehe mon sep 07, 11:06:00 pm, mtoa maoni:
anon16-rounded.gif
anonymous

jamani mbona wa tz hamjiamini? Kwani inglishi ni nini?
Kwa mtu kama kanumba aliye soma jitegee or sijui makongo kwa ujielezaji alio jieleza juzi ni kajitahidi sana , kwakweli nampa hongera sana ka kusingatia inglish ni lugha ya pili na hajasoma hivyo viji accademy vyenu.
Kujua kingereza kama second language ni kitu kiumu haswa unapo sima lugha ukiwa ume shapita miaka 15 , ina bidi uwe mdadisi zaidi ili uweze kuimaster lugha mpya .
Wengi wetu hatuwezi kuwa fluent in inglish sababu shule tulizo soma tume soma kingereza tukiwa akubwa , pale tunapo ingia secondari, elimu ya msingi kwa kingereza peke ni ngumu sana kuweza ku ongea lugha iyo, wengi tuna uwezo mkubwa wa kuisikia ila kuiongea ni ngumu.

Nashnidwa kuwaelewa kanini mnaona ni jambo la aibu kutojua kingereza , mbona mshiriki wa angola alikuwa ana vunja kiingereza vibaya sana na mbaka richard alikuwa ana mcheka live ,lakini hatukusema kitu .

Hongera kanumba , wewe ni a victim wa mfumo wa elimu wa tanzania , sio kosa lako.

haya ndo maoni ya watu wenye akili, hekima na busara. Watu wanaokubali ukweli wa sisi tz.
 
WANAJAMII MMEMUONA KANUMBA NDANI YA NYUMBA? LUGHA INAVYOMSUMBUA NA ANAVYOJITAHIDI KUJIFWAGILIA KUWA YEYE NI CELEBRITY? HEBU MCHAMBUENI KIDOGO.... mfano pale BIG alipowataka waandae mapokezi kwa housemate na akawapa dakika kumi za kufanya hivyo... Celebrity Kanumba akasema " so Big want us to make hurry" eish!

Mdau kanitonya eti alipoulizwa what do you like to eat amejibu "Am closing this month. Am waiting to open in the evening when I will eat my futari food......!"
 
Ina onekana walipewa Nafasi..Nafikiri wengi waliokua na sifaza kwenda huko hawakupewa!!....mmmh sijui!!
 
Wapendwa kwanza hongereni sana kwa maoni,

Kuhusu Kanumba, ametoka jana usiku baada ya kukaa masaa 24 ndani ya nyumba, kazi yake ilikuwa kupokea housemates.

Binafsi simlaumu kanumba ila wale waliompeleka huko, ni kweli tunajivunia kiswahili lakini kinakikomo chake, na hasa kwenye maeneo kama BBA. Unakutana na watu ambao kiswahili hawajawahi kusikia na unahitaji kuwasiliana nao, tusidanganyane, ni kweli tunajivunia kiswahili lakini kunaplatform nyingine huwezi kuzungumza kiswahili na wala huwezi kuwasiliana kama hujui lugha nyingine

sasa BBA lugha ya mawasiliano ni Kingereza tu, tatizo la Kanumba kwa mfano siyo kuongea broken English lakini tatizo pia kuelewa wengine wanaongea nini ili ajibu hata kama ni broken, tusifariaje hapa tukubaliane na ukweli ili mtu aweze kushinda kule lazima aongee ainteract ili watazamaji wavutiwe naye na kisha kumpigia kura, sasa ukiwa kimya kama Kanumba nani anakuona? huwezi kubishana huwezi kujibu maswali, huwezi kuuliza hivi kweli wewe ni mshiriki??

Lakini swali kubwa MNET hawakulijia hili? pamoja kuwa kanumba hakuwa mshiriki, lakini sidhani kama misson yao imekuwa accomplished, mwisho wa yote wanapompeleka mtu huko wajaribu kupeleka mtu anayeweza kuzungumza kuhusu Tanzania, kutetea Tanzania kwa nguvu zote na aeleweke pia, kumbukeni haya ni mashindano na hivyo nchi nyingine watatafuta weak point kukushinda, na si kazi yao kujua kuwa Watanzania kiswahili ndo lugha yetu. Lakini tunajua pia kuna watu wengine wangetuwakilisha vizuri zaidi
Mimi ninahakika ingekuwa ni kutafuta filamu bora, kanumba angefanya vizuri zaidi kwani huko pengine lugha isingekuwa kigezo, lakini hapa tunatafuta kitu kingine kabisa
Pamoja na yote tunamshukuru Kanumba kutuwakilisha lakini somo hili lifike kweto sote watanzania na waandaji pia. Naamini waandaaji watatupelekea mtanzania bora jumapili ambapo washiriki wa kike watatambulishwa. Ikumbukwe kwamba katika shindano hili lugha ndiyo kigezo cha kwanza mengine yatafuata baadaye

heshima mbele
 
Mdau kanitonya eti alipoulizwa what do you like to eat amejibu "Am closing this month. Am waiting to open in the evening when I will eat my futari food......!"

Alikuwa pia akiongea na mshiriki nadhani wa Mozambique au Zimbabwe (dont remember the nationality) ambaye juzi alimfundisha "meditation" au kumeditate kwa kibongo. sasa jana Kanumba akataka wafanye tena hilo zoezi lakini akasahau linaitwaje, basi akamfuata mshkaji na kumwambia "I want to do that exercise that make you travel is it tempatation?" mshkaji akamwambia hapana linaitwa meditation
 
Tatizo lako ni kudharau watu, wewe unaelimu gani ya kujidai nayo? Wewe unaelimu gani mpaka kunidharau hivyo? Ni taarifa yako shule ninayo, tena ya juu sana. Zungumza mengine siyo hizi pumba zako juu yangu, wala hunijui. Yaani suala la Kanumba liwe kipimo cha elimu ya mtu bwa ha ha ha...

Kuhusu Kanumba, yeye amefanya kwa sehemu yake. Acheni kujifanya msivyo, kingereza cha Watanzania wengi ni kibovu mno na kunasababu ya hilo. Ndo maana BBA wanaenda half-castes (Mwisho, Richard, Lutoya).

Kwani mmejua leo kuwa Kanumba anakingereza kibovu? mbona website yake: www.kanumba.com inakingereza kibovu sana (mfano: 'movies i've wrote') sasa si mngeanza kumsahihisha hapa?

Mimi nilichokuwa nimeongea ni juu ya ustaa wake na mchango wake ktk sanaa ya maigizo nchini kwetu. Nchi za wenzetu wala hawahangaiki na kingereza kizuri. Nimetembelea nchi mbalimbali za Ulaya mashariki na Asia nimejionea mwenyewe english inavyowapiga. Lakini wanaongea hivyohivyo na maendeleo yao ni makubwa. Wanatumia lugha zao na english ni second language kama sisi.

Napenda mtu tunae tofautiana huku tukiendelea kuheshimiana siyo kudharauliana.

Sielewi Kanumba amesaidia nini na sanaa yake. Nitarudia hilo baadaye.

Ndugu yangu Mojawapo ya faida ya kwenda shule ni KUELIMIKA. Kwa vipi?, ni kwa kuweza kutambua na kung'amua baya au zuri na kupima na misingi mbali mbali ya zamani ili kuweza kujua yajayo, though sio kwa precision inayotakiwa.

Ikiwa ni hivyo basi, hata uelewa wa Kanumba unaemshabikia ni mmbovu sana, Kama umesoma kweli (minimum Masters kwa kipimo changu) ungeweza kuona kuwa wazungu wa Eastern Europe huwa hawajui Kiingereza vizuri, wao kwa sababu wana UPEO mkubwa na exposure ya kutosha wanatafata MKALIMANI.

Hawajipeleki kichwa kichwa kama Kanumba. Kama wanajua hawata FIT wanakataa mwaliko. Kanumba amefadhaisha kila mmbongo, maana sio tu kuwa ni kibovu (hata prez alichemsha lakini angalau alieleweka) Kanumba hawezi kuongea sentensi mbili kwa kiingereza kilichonyooka.

Sasa mkuu kama na shule yako (unayosema unayo) hujaona haya basi nasema ulifuata cheti kwa kukariri tu na HUKUELEWA AU HUKUELIMIKA (no matusi intended, just a general thinking bro)
 
hivi nyie....kwani KIINGEREZA ni nini zaidi ya kuwa lugha ya mawasilianao???...dogo kama hajui kiingereza kwanini asitumie kiswahili???...shauri yake kwa kukurupuka na milugha ya watu hata asiyoifahamu....

haya KANUMBA TISA...KUMI BABA YETU alivyokuja BUSH....kwani baba alikuwa anaongea kiingereza safi???....KWELI NIMEEAMINI MITANZANIA NDIVYO TULIVYO...tunajikweza na kufanya mambo makubwaa tusiyoyaweza na kuishia kuaibika....

KISWAHILI NDO LUGHA ILOPITISHWA KUWA LUGHA YA AFRIKA ...ndiooo...MNAKUMBUKA RAISI CHISANO WA MSUMBIJI ALIWAHI KUHUTUBIA OAU/AU KWA KISWAHILI.....

sasa kwanini kanumba asitumie kiswahili hapo BBA tena kwenye shoo za kitoto hizo...au baba kwann asitumie kiswahili alipokuja bush....
mbona PUTIN HUWA ANATUMIA KI-RUSIA kwenye mikutano na waheshimiwa wenzake wa magharibi...

TUHESHIMU CHETU TUTAHESHIMIKA...pole kanumba kwa kukidharau kiswahili kilichokufikisha hapo ulipo na kuparamia kizungu kilichotuvua ngu watanzania wote...NI MAONI TUU
 
Wapendwa kwanza hongereni sana kwa maoni,

Kuhusu Kanumba, ametoka jana usiku baada ya kukaa masaa 24 ndani ya nyumba, kazi yake ilikuwa kupokea housemates.

Binafsi simlaumu kanumba ila wale waliompeleka huko, ni kweli tunajivunia kiswahili lakini kinakikomo chake, na hasa kwenye maeneo kama BBA. Unakutana na watu ambao kiswahili hawajawahi kusikia na unahitaji kuwasiliana nao, tusidanganyane, ni kweli tunajivunia kiswahili lakini kunaplatform nyingine huwezi kuzungumza kiswahili na wala huwezi kuwasiliana kama hujui lugha nyingine

sasa BBA lugha ya mawasiliano ni Kingereza tu, tatizo la Kanumba kwa mfano siyo kuongea broken English lakini tatizo pia kuelewa wengine wanaongea nini ili ajibu hata kama ni broken, tusifariaje hapa tukubaliane na ukweli ili mtu aweze kushinda kule lazima aongee ainteract ili watazamaji wavutiwe naye na kisha kumpigia kura, sasa ukiwa kimya kama Kanumba nani anakuona? huwezi kubishana huwezi kujibu maswali, huwezi kuuliza hivi kweli wewe ni mshiriki??

Lakini swali kubwa MNET hawakulijia hili? pamoja kuwa kanumba hakuwa mshiriki, lakini sidhani kama misson yao imekuwa accomplished, mwisho wa yote wanapompeleka mtu huko wajaribu kupeleka mtu anayeweza kuzungumza kuhusu Tanzania, kutetea Tanzania kwa nguvu zote na aeleweke pia, kumbukeni haya ni mashindano na hivyo nchi nyingine watatafuta weak point kukushinda, na si kazi yao kujua kuwa Watanzania kiswahili ndo lugha yetu. Lakini tunajua pia kuna watu wengine wangetuwakilisha vizuri zaidi
Mimi ninahakika ingekuwa ni kutafuta filamu bora, kanumba angefanya vizuri zaidi kwani huko pengine lugha isingekuwa kigezo, lakini hapa tunatafuta kitu kingine kabisa
Pamoja na yote tunamshukuru Kanumba kutuwakilisha lakini somo hili lifike kweto sote watanzania na waandaji pia. Naamini waandaaji watatupelekea mtanzania bora jumapili ambapo washiriki wa kike watatambulishwa. Ikumbukwe kwamba katika shindano hili lugha ndiyo kigezo cha kwanza mengine yatafuata baadaye

heshima mbele

Mkuu umemaliza yooote. Asante sana ubarikiwe. Mtu mwenye busara huwa anaona kilicho mbele yake na kukiepuka na sio kukivamia.

Tanzania tunajua tatizo letu kwanini ukaonyeshe tatizo lako badala ya kulificha?

Ni afadhali watu wakadhania kuwa u mjinga kuliko kufunua mdomo na kuwathibitishia.
 
FairPlay, suala la kuelimika hulielewi wewe. Ninashindwa kukuelewa unavyokomalia suala la shule ktk kutoa maoni tu juu ya suala hili. Mara nyingi watu wenye arguement kama zako ni wale waliosoma kidogo au waliopata nafasi ya kusoma kibahati tu.

Back to Kanumba, niseme wazi kwamba ni kawaida yangu kumuunga mkono Mtanzania yeyote anayefanya jambo lenye kuonekana. Ninapompima Kanumba siwezi kutumia kipimo cha akina Will Smith au ice cube. Ninampima ktk level yake.

Ninakiri uwezo mkubwa wa Kanumba ktk fani ya maigizo Tanzania. Mchango wake ni mkubwa, wewe huuoni kwasababu either hupo Tanzania na huna ukaraibu na mambo ya huko au hutaki kukubali kwa sababu zako.

Sasa hivi kuna soko la movie za bongo (mimi sipo bongo lakini nazipata omba watu wawe wanakutumia kwa DHL nk kwani ninahisi hupo bongo). Kanumba amechangia sana kuinua soko hilo. Nilisema ktk post ya kwanza kuwa ninawakubali Kanumba, Ray na Magali. Wengine wanachipukia tu au wanasaidiwa na hawa jamaa.

Ni vema kutambua kwamba Taifa letu bado linakuwa ktk kila kitu, siyo demokrasia na uchumi tu, hata sanaa. Ni bora kitu kuliko pasipo kitu. Sasa kama tunawakatisha tamaa hawa wanaojenga msingi ukuta hautajengwa. Jamaa ni kweli ameonyesha udhaifu lakini si suala la kila mmoja kumshambulia eti ametia aibu taifa. Kama BBA alitaka kijana wa kiume, msanii maarufu mlitaka aende nani? Richard tena? Kikubwa ni kwamba tunakuwa, hatujafika huko mnakodhani tupo.
 
Tanzania tunajua tatizo letu kwanini ukaonyeshe tatizo lako badala ya kulificha?

Ni afadhali watu wakadhania kuwa u mjinga kuliko kufunua mdomo na kuwathibitishia.

Sasa mkuu kama na shule yako (unayosema unayo) hujaona haya basi nasema ulifuata cheti kwa kukariri tu na HUKUELEWA AU HUKUELIMIKA (no matusi intended, just a general thinking bro)

Huko ndo unakoita wewe kuelimika, kuficha ulivyo sababu ni english Bwa ha ha ha....
 
FairPlay, suala la kuelimika hulielewi wewe. Ninashindwa kukuelewa unavyokomalia suala la shule ktk kutoa maoni tu juu ya suala hili. Mara nyingi watu wenye arguement kama zako ni wale waliosoma kidogo au waliopata nafasi ya kusoma kibahati tu.

Back to Kanumba, niseme wazi kwamba ni kawaida yangu kumuunga mkono Mtanzania yeyote anayefanya jambo lenye kuonekana. Ninapompima Kanumba siwezi kutumia kipimo cha akina Will Smith au ice cube. Ninampima ktk level yake.

Ninakiri uwezo mkubwa wa Kanumba ktk fani ya maigizo Tanzania. Mchango wake ni mkubwa, wewe huuoni kwasababu either hupo Tanzania na huna ukaraibu na mambo ya huko au hutaki kukubali kwa sababu zako.

Sasa hivi kuna soko la movie za bongo (mimi sipo bongo lakini nazipata omba watu wawe wanakutumia kwa DHL nk kwani ninahisi hupo bongo). Kanumba amechangia sana kuinua soko hilo. Nilisema ktk post ya kwanza kuwa ninawakubali Kanumba, Ray na Magali. Wengine wanachipukia tu au wanasaidiwa na hawa jamaa.

Ni vema kutambua kwamba Taifa letu bado linakuwa ktk kila kitu, siyo demokrasia na uchumi tu, hata sanaa. Ni bora kitu kuliko pasipo kitu. Sasa kama tunawakatisha tamaa hawa wanaojenga msingi ukuta hautajengwa. Jamaa ni kweli ameonyesha udhaifu lakini si suala la kila mmoja kumshambulia eti ametia aibu taifa. Kama BBA alitaka kijana wa kiume, msanii maarufu mlitaka aende nani? Richard tena? Kikubwa ni kwamba tunakuwa, hatujafika huko mnakodhani tupo.

So Kanumba was a better choice among the worst?, Is that what you are trying to tell us?

Anyway, shule, sipo bongo achana nazo. Nimesema tuanzishe topic ya Sanaa ya movies bongo nikwambie kwanini ninaishi Mbagala na wala sizitazami. Nani anataka dakika ishirini iwe inaonyeshwa gari linatoka Mbagala mpaka mjini?, ili mradi tu wawe na CD mbili (part one and two). Labda wee mzee sio mimi.

Achana na Usanii unaouita sanaa. Kanumba kama alikuwa anajijua kuwa hawezi kuwasiliana kwanini hakumtafuta Mkalimani?, rejea post yangu niliyojibu hoja ya wazungu kutojua kiingereza, na acha na hoja ya shule jibu subject matter.
 
Huko ndo unakoita wewe kuelimika, kuficha ulivyo sababu ni english Bwa ha ha ha....

Mkuu achana na ya shule nimeshakujua uwezo wako..........najaribu tu hapa kukuelimisha, nitajitahidi tu najua Mabox yanachosha sometimes.

Hoja ninayoijenga hapo juu ni kuwa kama unajua hujui kwanini uende ukahaibike?, kwanini husikatae kwenda?. Yaani tumia busara yako kupima ya mbeleni.

Kama hujaelemika nitaendelea kukuelimisha tu kaka karibu
 
So Kanumba was a better choice among the worst?, Is that what you are trying to tell us?

Anyway, shule, sipo bongo achana nazo. Nimesema tuanzishe topic ya Sanaa ya movies bongo nikwambie kwanini ninaishi Mbagala na wala sizitazami. Nani anataka dakika ishirini iwe inaonyeshwa gari linatoka Mbagala mpaka mjini?, ili mradi tu wawe na CD mbili (part one and two). Labda wee mzee sio mimi.

Achana na Usanii unaouita sanaa. Kanumba kama alikuwa anajijua kuwa hawezi kuwasiliana kwanini hakumtafuta Mkalimani?, rejea post yangu niliyojibu hoja ya wazungu kutojua kiingereza, na acha na hoja ya shule jibu subject matter.

well, you are there! unakubaliana na hilo swali au unakataa? mimi nasema YES. Na ndo msingi wangu i'm optimistic about future whatever of bongo movies/art works in general.
 
Mkuu achana na ya shule nimeshakujua uwezo wako..........najaribu tu hapa kukuelimisha, nitajitahidi tu najua Mabox yanachosha sometimes.

Hoja ninayoijenga hapo juu ni kuwa kama unajua hujui kwanini uende ukahaibike?, kwanini husikatae kwenda?. Yaani tumia busara yako kupima ya mbeleni.

Kama hujaelemika nitaendelea kukuelimisha tu kaka karibu

we dogo mimi sibebi mabox aise, ninakazi yangu ya maana sana, pole siwezi kukusaidia.
 
well, you are there! unakubaliana na hilo swali au unakataa? mimi nasema YES. Na ndo msingi wangu i'm optimistic about future whatever of bongo movies/art works in general.

Now you are talking. Yap could be bro.

Ila for the future of Bongo movies......smart pipo need to enter in the industry so as to change the status quo and make some quality movies.

Hali ya movies za kibongo interms ya quality na story ni MBOVU MNNNOOOOOOOOOO. Mfano ni story chache sana unaweza kushindwa kujua inaishaje.

Waigizaji wapo POA SANA, ila waongozaji wanahitaji shule.

Kwa sasa fani ya movies bongo ni ya watu waliofeli form four, six na darasa la saba. Inatakiwa watu wenye nia ya kibiashara na upeo waichukue hii fani.

Anyway nimekuelewa kuhusu Kanumba na wewe unakubali kuwa hakutumia busara kwenda?
 
we dogo mimi sibebi mabox aise, ninakazi yangu ya maana sana, pole siwezi kukusaidia.

Haya bwana , mabox ilikuwa ni utani tu. Mie nakula vumbi hapa Mbagala, karibu saana ukirudi, ukikosa nauli mwaka huu niambie nikutumie ticket. LOL
 
First priority kwa Kanumba ni kujichubua uso na si kujiendeleza kielimu ili walau aweze kujua kingereza ambacho kingemfanya aweze kushiriki katika film za kimataifa.
 
Sielewi Kanumba amesaidia nini na sanaa yake. Nitarudia hilo baadaye.

Ndugu yangu Mojawapo ya faida ya kwenda shule ni KUELIMIKA. Kwa vipi?, ni kwa kuweza kutambua na kung'amua baya au zuri na kupima na misingi mbali mbali ya zamani ili kuweza kujua yajayo, though sio kwa precision inayotakiwa.

Ikiwa ni hivyo basi, hata uelewa wa Kanumba unaemshabikia ni mmbovu sana, Kama umesoma kweli (minimum Masters kwa kipimo changu) ungeweza kuona kuwa wazungu wa Eastern Europe huwa hawajui Kiingereza vizuri, wao kwa sababu wana UPEO mkubwa na exposure ya kutosha wanatafata MKALIMANI.

Hawajipeleki kichwa kichwa kama Kanumba. Kama wanajua hawata FIT wanakataa mwaliko. Kanumba amefadhaisha kila mmbongo, maana sio tu kuwa ni kibovu (hata prez alichemsha lakini angalau alieleweka) Kanumba hawezi kuongea sentensi mbili kwa kiingereza kilichonyooka.

Sasa mkuu kama na shule yako (unayosema unayo) hujaona haya basi nasema ulifuata cheti kwa kukariri tu na HUKUELEWA AU HUKUELIMIKA (no matusi intended, just a general thinking bro)
Lugha ni mfereji wa maarifa. Siamini kama Kanumba hajaelimika. Ana maarifa. Isipokuwa mfereji aliopatia hayo maarifa ni Kiswahili zaidi na wala si Kiingereza. Kumbe kama ingekuwa ni kuongea Kiswahili sidhani kama angeshindawa. Shida ni kuparamia huo umombo. Alipaswa kujua udhaifu wake na kukataa mwaliko huo
 
mkuu ndo najaribu kumuelimisha Nemesis atambue kuwa Kanumba:

Alipaswa kujua udhaifu wake na kukataa mwaliko huo.

Lakini hakutambua kwasababu ya uwezo mdogo wa uelewa wa mambo.

Tupo pamoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom