Lugha sio kiingereza tu. Gadaffi hajui kiingereza vizuri lakini anaweza kukufundisha kiarabu. Viongozi wengine wanajua vizuri kireno,kijapani,kirusi,kihispania,kijerumani, kifaransa,nk, kuliko wanavyojua kiingereza.Amejitahidi sana! Muammar Gaddafi hajui hata kuandika barua ya kuomba kazi kwa kiingereza ingawa ni kiongozi wa nchi.
Mkuu are you serious.., hio sentensi ipo awkward..
Ni bora angeandika...
From an early age I have always wanted to be an actor au..
I have always wanted to be an actor from an early age
Mkuu. Sentensi ya Kanumba na hizo za kwako zote si sahihi. Ila hiyo 'an' ikitolewa ikawa mfano ' from early age' au 'from my early age' zitakuwa sawa.
Mkuu from early age is not correct hapo unahitaji article the au an
Kwahiyo from an early is correct from early does not sound correct
Wengi hatuwezi lakini hakuna mtu anaeshindwa kumuomba mwingine amuandikie.. professionalism
Amejitahidi sana! Muammar Gaddafi hajui hata kuandika barua ya kuomba kazi kwa kiingereza ingawa ni kiongozi wa nchi.
("Hello and welcome,
I've been blessed to live my dream, for quite a while now. From an early age I've wanted to be an actor and to make a difference in people's outlook on life by way of the art of acting.
I've had the priviledge and opportunity to work with some of the best actors on the continent, making movies that in some way or the other influence peoples' lives and outlooks. That being said there are still more movies to be made and many talented people to work with all over the world.
I hope that this site will be a window through which you may take a peek at my life and career. This is the best place to find out about what I'm working on, with whom and a whole lot of other fun stuff I get up to.
Enjoy!")
Wadau mimi sio mtaalamu wa kiingereza kwa sana, ila naomba mnisaidie hapo kwenye rangi nyekundu labda mimi ndiye nisiyeelewa. Hii iko kwenye ukurasa wa mbele wa website ya kanumba.
Kanumba, The Great
Yeeeeees! Wataalam wa kimombo wakiwa kazini........... mpaka nione mshindi leo!
Ni bora angeandika Kiswahili tu ama kuajiri wataalamu wa lugha kumuandalia hayo aliyotaka kuyaandika.....
Mkubwa ukumbuke Kiingereza ni lugha yetu ya pili, tatu au kwa wengine hataya tatu.
Wachina, Warusi na Wajapan hata Wajerumani na Wafaransa, kwao kutokuzungumza Kiingereza hakuwakoseshi usingizi, nina maana Kiingereza ni lugha, ila sio kipimo cha elimu ya mtu.
Kanumba mie naona kajitahidi kukiongea hata kama kakivunja ile mbaya. Sioni tatizo hapo, ila kama akiongeakiswahili chetu ovyo naukamponda, hapo ntakuelewa.
Ndugu yangu hapa TZ kwenyewe ni wangapi wanaoweza kuandika kwa kiwango hicho unachosema cha professionalism? Hapo kwenyewe ameandikiwa na mtu ambaye alimwamini kwamba atafanya kazi hiyo kwa uhakika sasa kimombo chenyewe ndo hicho, jamani tuache tu hiyo ni lugha ya wenyewe, sisi tukomae na Kiswahili chetu tu!!
Ila kama ameandika mwenyewe hatuna budi kumpa hongera, amejitahidi huwezi linganisha na alivyofanya kwenye Big Brother! Grammar yenyewe ni janga la Kitaifa! hamkumsikia Mh. mmoja wakati wa kuomba kura za Bunge la Africa? na huyo sasa ni msomi mwenye Masters sembuse na Kanumba aliyesoma shule zetu za Kata!!!!
Hahahahaha mkuu umenivunja mbavu asee.....khaa! Former Prime Minister an Edward Lowasa......... LOLMkuu hata mie nimejiweka kando maana haya mambo magumu sana yanataka wito.
Wanatwambia a, e, i, o, u na h zinakwenda na "An", hivyo ni sawa kusema An Edward Lowasa in an house.
Wallah wazungu kiboko!