Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,591
- 134,264
Kuna neno limemisi, "Kanisa ni Moja Tuu, Takatifu Katoliki La Mitume!'.Kuna kanisa moja tu Katoliki la mitume.
Kuna kanisa moja tu Katoliki la mitume.Ukiniuliza kwanini tembelea kanuni ya imani ambayo madhehebu yote yakikristu hukiri.Kwa maana nyingine hao wanaprotest agaist the church(Catholic) though kwenye kanunu zao za imani wanasadiki kwa kanisa Katoliko(Catholic)kwa maneno.
.
Kuna neno limemisi, "Kanisa ni Moja Tuu, Takatifu Katoliki La Mitume!'.
Alianza TB Joshua, sasa yanafuatia makanisa haya madogo madogo, itafuatia misikiti, the by 2014 lifuatia Anglican, Mid 2015 Lutheran, October, 2015 ndipo itakuwa zamu ya lile Kanisa ni Moja Tuu, Takatifu Katoliki La Mitume!.
Japo yeye ni sauti tuu ya mtu aliye nyikani, Mungu Baba ataudhihirisha utukufu wake kupitia kwayo, kwa "jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!", na litatimie lile neno "Wewe ni mwamba, na juu ya mwamba huu nitalijenga taifa langu!".
Kwa wale ambao ni wabishi kuliko Tomaso wakidhani kuna mambo ambayo hayawezekani!, nawahakikishia "nothing is impossible under the sun!" na "lisilowezekana kwa binadamu, kwa Mungu, linawezekana!".
Pasco.
...Tafadhali tupe ufafanuzi wa mkanganyiko huo kwenye red.KANISA la Overcomers lililopo mkoani Iringa, limeandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kumtunuku Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kutokana na mchango wake alioutoa katika jamii.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Boaz Sollo, alisema jamii ya wakazi wa Mkoa wa Iringa inatambua mchango wa Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli.
Dk. Sollo alisema kuwa tuzo hiyo itampa moyo wa kuendelea kushiriki zaidi katika shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuiendeleza injili kama ambavyo amekuwa akifanya.
"Hii tuzo itamuongezea ujasiri wa kujituma katika kuisaidia jamii, sambamba na kuchangia ujenzi wa makanisa katika mikoa mbalimbali bila kujali wanaomkatisha tamaa ili kumrudisha nyuma.
"Tumeandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kiongozi huyu ambaye haipiti wiki moja anasikika akifanya kazi za kijamii, habagui, hachagui na wala hana upendeleo," alisema Dk. Sollo.
Aliongeza kuwa tangu alipojiuzulu uwaziri mkuu, hajawahi kuutembelea mkoa huo jambo linalowafanya wakazi wa mkoa huo kuwa na hamu ya kumuona kutokana na jitihada zake za kujihusisha katika masuala ya kijamii.
Alisema tuzo hiyo itatolewa mwezi ujao wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo na kituo cha redio ya dini ya Overcomers, ambayo ni maarufu kwa mikoa ya kusini.
Wakizungumza na MTANZANIA kuhusu tuzo hiyo, baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wamelipongeza kanisa hilo kwa kuandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kutambua mchango wa kiongozi huyo.
CHANZO: Mtanzania
alikaa kimya na leo tunawalipa mabilioni ambayo bila shaka ndiyo anayotamba nayo makanisani na misikitini. Angekuwa na mapenzi na watanzania angeelezea umma dili zima la RICHMOND na wahusika wake ili umma uwaadhibu.Usichokijua nini? nilitaka kuvunja mkataba ukanikataza ! ukasema unasubiri ushauri wa makatibu wakuu,hawa watoto wadogo wananitukana zaidi ya miezi 7 wanazunguka nchi nzima,sasa ndio mumegundua kufwata sheria na kanuni?MKAPA akatikisakichwa(kukubali).chezea Lowasa wewe.
Wanafukuzia mshiko tu hapo, wanajua hiyo tuzo haiendi bure.
KANISA la Overcomers lililopo mkoani Iringa, limeandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kumtunuku Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kutokana na mchango wake alioutoa katika jamii.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Boaz Sollo, alisema jamii ya wakazi wa Mkoa wa Iringa inatambua mchango wa Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli.
Dk. Sollo alisema kuwa tuzo hiyo itampa moyo wa kuendelea kushiriki zaidi katika shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuiendeleza injili kama ambavyo amekuwa akifanya.
Hii tuzo itamuongezea ujasiri wa kujituma katika kuisaidia jamii, sambamba na kuchangia ujenzi wa makanisa katika mikoa mbalimbali bila kujali wanaomkatisha tamaa ili kumrudisha nyuma.
Tumeandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kiongozi huyu ambaye haipiti wiki moja anasikika akifanya kazi za kijamii, habagui, hachagui na wala hana upendeleo, alisema Dk. Sollo.
Aliongeza kuwa tangu alipojiuzulu uwaziri mkuu, hajawahi kuutembelea mkoa huo jambo linalowafanya wakazi wa mkoa huo kuwa na hamu ya kumuona kutokana na jitihada zake za kujihusisha katika masuala ya kijamii.
Alisema tuzo hiyo itatolewa mwezi ujao wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo na kituo cha redio ya dini ya Overcomers, ambayo ni maarufu kwa mikoa ya kusini.
Wakizungumza na MTANZANIA kuhusu tuzo hiyo, baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wamelipongeza kanisa hilo kwa kuandaa tuzo maalumu kwa ajili ya kutambua mchango wa kiongozi huyo.
CHANZO: Mtanzania
kuna tofauti gani kati ya kanisa na dhehebu???
Pamoja shem king'asi.Asante. Yaani Yesu nadhani anajishangaa huko alipo manake sasa kanisa limekuwa kitu tofauti kabisa na kazi aliyotumwaga yeye duniani. Kanisa imekuwa biashara na mahala pa kuganga njaa. Im feel so ashamed! Nilifurahi sana bishop dr malasusa hakumualika lowassa wala maselebriti wengine kwenye kuchangia marekebisho ya kanisa lililochomwa mbagala.