Kiwi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 1,054
- 995
Habari zenu wanajamvi,
Ninaomba mtu yeyote mwenye kulifahamu kanisa linaloitwa Mlima wa Matumaini linaloongozwa na Apostle Lutumba kutoka Congo na mkewe kutoka Zambia. Kanisa hili linasemekana lilianzia Tabata, na sasa limehamishiwa Mbagala/Toa Ngoma.
Mimi binafsi sio muumini wa kanisa hilo wala sifahamu lilipo. Ila cha kusikitisha ni kuwa wazazi wangu wamekuwa wakitapeliwa sana na viongozi wa kanisa hilo. Niliwahi kuwaona siku moja tu hao "wachungaji/manabii", na sikuamini macho yangu kuona jinsi walivyokuwa na majivuno ya ajabu sana. Walidiriki kuniambia unaona sisi tuna magari manne kwa nini huwasaidii wazazi wako kwa kuwanunulia gari? Wakati huo hao wachungaji hawafahamu kuwa gari wanalotumia wazee wangu hadi leo hii limeanza kuchakaa nililinunua mimi.
Sasa kinachonitia uchungu zaidi ni kuwa wazazi walikuwa na nyumba mbili, moja imeuzwa mwaka jana, na mama mzazi amekiri kuwa amemuuzia mtoto wa huyo mchungaji. Kumuuliza aliiuza kwa kiasi gani, jibu lake likawa nyumba ni yangu haikuhusu, nikanyamaza. Sasa jana nimepata tena taarifa kuwa nyumba ya pili iko njiani kuuzwa, mama anataka waiuze halafu wao wahamie kanisani.
Wandugu naomba msaada wenu, nimechanganyikiwa sana. Mimi niko ughaibuni. Nina hakika mama ameshachotwa akili na hawa watu wa hilo kanisa. Kila senti anayoipata anaipeleka kanisani. Mwaka jana mwezi wa sita alipeleka shilingi milioni moja na laki saba kanisani. Mwezi wa kumi na mbili akanipigia simu kuwa anaumwa anahitaji shilingi laki tatu aende hospitali. Kweli mtu kama huyu tumsaidieje jamani?
Ndiyo sababu nimeona niombe msaada kwanza nijue hilo kanisa kweli lipo, limesajiliwa kihalai na linafanya kazi gani, kama sio kudanganya watu hasa wazee na kwa kufanya hivyo kutupa matatizo sisi watoto ambao ndiyo tunaowatunza wazee wetu? Kama kuna yeyote anayefahamu hilo kanisa hata kwa mbali tu naomba anijulishe, ninataka kufuatilia hili suala la utapeli kutumia dini.
Natanguliza shukrani.