Kanisa katoliki mmekubali kujichafua na pesa za Lowassa?

Tunaliheshimu sana Kanisa Katoliki, Tunawaheshimu sana viongozi wake. Kanisa Katoliki angalau mpaka ninapoandika uzii huu ni Kanisa tajiri sana, linamiliki Taasisi muhimu sana, Hospitali, Zahanati, vituo vya Afya, Shule za chekechea, msingi Sekondari, Vyuo, na vyuo vikuu, Bahati mbaya sana kanisa Katoliki linamiliki hadi Mkombozi Benk. Kanisa Katoliki linapata sadaka na michango mbalimbali toka kwa waumini wake, ni kanisa ambalo kweli halipaswi kulia njaa, hadi kiwango cha kukimbilia Pesa ambazo zinazua maswali mengi. Walioandaa Chakula cha Hisani kwa ajili ya uanzishwaji wa Jimbo Katoliki Ifakara, walikosa mtu mwingine hadi wamwite Lowassa tu? Wameenda wapi viongozi wa dini wenye maadili mazuri, mfano Balozi wa baba mtakatifu, mwadhama Kardinali, Maaskofu wakuu, Wakuu wa Mashirika au watu wengine? CCM walitamka wao kwa kinywa chao kuwa Lowassa ni FISADI. Nimejisikia vibaya sana kuona Kanisa limeamua kutoangalia upandaji wa maisha ya watanzania wa sasa kwa sababu ya gharama za Umeme amabazo chanzo chake kimekuwa Richmond, Dowans. Kweli mmeamua kuyaishi yale mliyoyalaani?. Angalau kwa ajili ya wenye dhamiri changa mngeacha hili. Mihi Vivere Christus est......................
Mimi naomba niiangalia hoja hii kwa upande mwingine. Kanisa Katoliki (mimi ni muumini wake) siku hizi limegeuka kuwa mjasiriamali zaidi kuliko kazi ya kuhubiri neno la Mungu
 
Kinachohitajika yule aliyemdhambi kumrudia mungu

Wakati ule Yesu aliwambia wale waliomleta yule mwanamke aliyezini ili ahukumiwe kwa kupigwa mawe na Yesu aliwambia kuwa asiyekuwa na dhambi ya zinaa na awe wa kwanza kupiga jiwe mwanamke huyu na Yesu akainama chini alivyoinua macho hakumkuta hata mmoja wao ispokuwa yule mwanamke.

Kwa maana hiyo kanisa lisibebeshwe dhambi za watu na wala kanisa haliwezi kumtenga mtu kwa sababu dhambi zake bali kumleta karibu ili atubu.Pia kanisa halina taratibu za kuandaa viongozi wa kisiasa kazi ya kani sa ni kurudisha wale wote waliopotea
 
Kuna kitu cha siri ambacho kanisa katoliki linajua kuhusu Lowassa na kwa utamaduni wa katoliki halitasema siri hiyo litafanya vitendo tu matokeo yake tutayaona mbele.

Kuna watu wanafikiri wataweza kuiangusha dola ya kikatoliki. Dola hii ipo tangu enzi ya Roma empire ni moja ya dola za kale na kongwe duniani.

Nobo tatu (75%) ya wakristo wote duniani ni wakatoliki.

Kuhatarisha uhai wa dola ya ukatoliki yenye watu wenye akili ya hali ya juu na fedha nene kumesababisha kuanguka kwa tawala nyingi duniani.

kwa suala la Lowassa Wakatoliki wanajua wanafanya nini na kwa nini wamegeuka kumuunga mkono.

Tunatakiwa kufukua ukweli ni nini kimesababisha wakatoliki kumuunga mkono muumini wa KKKT kinyume na Mila zao.
 
Kwani Lowasa anaenda makanisani kutubu? Ni ili akatubu lazima aarikwe?


Makanisa yote yaliyoingia kwenye mtego wa Lowasa yamepotoka na yanajichimbia makaburi yake.....!

Babu DC!!
We kinakuwasha nn? Ulitaka ualikwe wewe?
 
Kweli nimekubali kwamba kufikia 2015 tutaona mengi,

Kwa hiyo EL amekuwa mtu wa Mungu na kwa hiyo mambo yake ya siasa nayo yamekuwa ya Mungu...Sasa ya Kaisari ni yapi tena?

Babu DC!!
kaisari ni mambo ya nchi yani ya kidunia, kama mahakama, polisi na mengineyo. yani ya mungu yaache kwa mungu na ya dunia yaachie dunia.
 
Mimi naomba niiangalia hoja hii kwa upande mwingine. Kanisa Katoliki (mimi ni muumini wake) siku hizi limegeuka kuwa mjasiriamali zaidi kuliko kazi ya kuhubiri neno la Mungu
kivipi?, elezea ujasiliamali wake kwa vielelezo.
 
Mi naona kama sasa hivi kuna vita kali juu ya ni dini gani inatakiwa imsimamishe mgombea urais ambaye atakuwa na mafanikio kwenye uchaguzi ujao wa 2015.Sasa makanisa yote naona wameona hakuna mkristo yeyote ndani ya CCM ambaye anaweza kuwa na mafanikio akipambanishwa na kundi la waislamu hivyo wameona ni bora huyu(Edward) kwa kuwa tu anaamini kuwa Bwana Yesu ni mwana wa Mungu(hata kama haishi kwenye imani yake).Na ndio maana wameamua kumualika kwenye harambee zao
 
Natafuta website ya TEC au kanisa katoliki tanzania niwamwagie hasira zangu kwa kuruhusu ujinga na sarakasi za EL zifanyike kanisani.
Mwenye kujua hii site please aimwage hapa!
 
Ndugu yangu Isango nakujua wewe umepata kusoma seminari, mara hii umesahau kuwa kanisa halimuhukumu mtu kwa kuwa tu wewe unamtuhumu!!! halafu pia mtu hata kama ana dhambi lakini kuna maungamo ambayo ni ya siri..! hakuna dhambi ndogo na kubwa wala sadaka kubwa na ndogo, hebu kumbuka mara ngapi tumezini, mara ngapi tumesengenya, mara ngapi tumedanganya au umetukana na kuwaza mabaya !!!!! bila mie kujua umetubu ama hujatubu lakini bado kanisa linapokea sadaka yako na wakati mwingine kushiriki meza ya Bwana. jamani tusitake kanisa lifanya kazi Kidunia kama mfanyavyo ninyi. hata mamlaka zenyewe zilizopewa haki kisheria kudeclare kuwa somebody is.guilty hazijawahi kufanya hivyo??? Ahhhhh.... hata kama humpendi Mzee EL lakini usilisakame kanisa kwa kuwa lipo kwa ajili ya kila aitwaye binadam

Natumia kasimu ka mchina kamanda sioni pa kukugongea like. well worded!
 
Je hamuiamini "INTELLIGENCE UNIT" ya KANISA? Mjadala uanzie hapo

Nadhani hiyo intelligence unit ya kanisa kama ipo basi imeshambuliwa na virus na sasa iko corrupted kama ile taasisi kuu ya nchi!!

Kanisa ambalo limekuwa likipaza sauti kupinga maovu likiwemo suala la ufisadi, haliwezi kusamehewa kwa kushirikiana na mtuhumiwa muhimu wa ufisadi ambaye hajasafishwa na walio mchafua!!


Kwanza Nape afute kauli yake kuwa EL ni gamba kabla hatujamtatifuza...Vinginevyo kanisa limejichafua na kupoteza moral authority ya kukemea maovu!!

Huo ndio ukweli unaosemwa bila motivation ya bahasa nyuma yake!

Babu DC!!
 
Nadhani hiyo intelligence unit ya kanisa kama ipo basi imeshambuliwa na virus na sasa iko corrupted kama ile taasisi kuu ya nchi!!

Kanisa ambalo limekuwa likipaza sauti kupinga maovu likiwemo suala la ufisadi, haliwezi kusamehewa kwa kushirikiana na mtuhumiwa muhimu wa ufisadi ambaye hajasafishwa na walio mchafua!!


Kwanza Nape afute kauli yake kuwa EL ni gamba kabla hatujamtatifuza...Vinginevyo kanisa limejichafua na kupoteza moral authority ya kukemea maovu!!

Huo ndio ukweli unaosemwa bila motivation ya bahasa nyuma yake!

Babu DC!!

Wewe ni msafi? Naona umekuwa Farisayo wa kizazi kipya?
 
Hapa USA
Kanisa katoliki lina kesi kibao Mahakamani za kuwalinda Mapadre walio wala witi vijana wadogo kibao.
Padri anakula witi kwa nguvu kijana akienda kutoa taarifa Padri anahamishwa.
Hapa kwa wenzetu sheria hufuata mkondo na inakata kama msumeno mahakam imeamuru kanisa kulipa vijana hao fidia za mamilioni.
Sakata hilo bado linaendelea.
Yesu alikula nawenyedhambi meza moja huku akiwakata injili siyo kuwaomba mchango wa ujenzi wa himaya yake.
Yesu alikaribishwa numbani kwa wenye dhambi na hakusita kuwaambia ukweli.
Kama wewe ni mtoza ushuru toza kiwango kilicho halali.
kama wewe ni askari usichukue mali isiyo yako kwa nguvu, tenda haki.

Leo Wakatoliki wanamwalika Lowassa kuwa mgeni Rasmi katika kuchangia kanisa ili zile pesa za Giza nene la Richmonduli nao wapate mgao wake
Sijui kwa vile wamesikia jamaa anajianda kuingia Ikulu 2015 wasije wakakosa utukufu wa hapa duniani??

Hii si mara ya kwanza Mussolin na Hitler nao pia waliwahi kuwa watu muhimu kwao.
 
Kama CHADEMA wasipojipanga vizuri sioni ni kitu gani kitakachomzuia Lowasa kuwa Rais wa Tano wa nchi hii, sababu za msingi ni hizi hapa:
1. Kumekuwa na upumbavu wa kila siku kuliandika jina la Lowasa humu mitandaoni uku watu wakidhani wanazidi kumtia dosari kumbe bila kujuwa ndio wanampigia Promo ya uhakika.

2. Lowasa tayari ana sifa muhimu ya Rais ajaye, yaani lazima awe ni mkristo na hii ni karata muhimu ambayo Lowasa anaifahamu na kwa upande wa kanisa lake la Lutheran kazi imeshakamilika na ndio maana sasa anahamia upande wa kanisa katoliki.

3. Lowasa alishasema hakuna alilokuwa amelifanya ambalo halina baraka za JK, sasa ufisadi wa Lowasa hapa ni nini? kwa nini mnamuogopa JK? hapa watetezi wa Lowasa watasema anachukiwa kutokana na dini yake na kwa sababu anatoka kaskazini.

Ushauri: kama umpendi Lowasa ni busara zaidi kumpotezea tu kuliko kumuanzishia thread hapa JF, ni kwamba unazidi kumjenga zaidi kuliko kumbomoa. kwa CCM dhaifu ya JK hakuna wa kumzuiya Lowasa kuwa mgombea na akishinda ugombea ndani ya CCM Lowasa ni kwamba tumeumia hakuna chama chochote cha upinzani chenye jeuri ya kushindana na mtandao wa Lowasa.
 
We kinakuwasha nn? Ulitaka ualikwe wewe?


Pole sana ndugu yangu,

Anyway...Siku huyo EL atakapokuwa rais mtarudi tu hapa kuyakumbuka maneno yetu.

Sumaye alisema kuwa mtu anayetumia media kumaliza wenzake kabla ya kuingia ikulu, basi akiingia atatumia risasi za moto...Hamjayaona?

Haya bwana endeleeni na kampeni zenu.....Laiti madhara ya uchafu wenu yangeishia kwenu na yasituguse wengine!!
 
kanisa linapokea kila m2 awe fisadi,jambazi,mchawi na nk.hakuna wa kumhukumu mwanadamu.bali ni Mungu pekee.walete hayo mahela 2jenge makanisa shule hospital na nk.akili ku mkichwa
 
Natafuta website ya TEC au kanisa katoliki tanzania niwamwagie hasira zangu kwa kuruhusu ujinga na sarakasi za EL zifanyike kanisani.
Mwenye kujua hii site please aimwage hapa!
Wakati wanasema Kikwete ni chaguo la Mungu wewe ulikuwa wapi? Nadhani kwa wenye kujuwa namna ya kuwasiliana na Lowasa hata mimi nahitaji mawasiliano yake aje kutusaidia harambee mtaani kwetu, maana hata Biblia kwenye Mithali inasema Pesa ndio jibu la yote. wewe mwenzangu sijui unasoma Biblia gani!!
 
kivipi?, elezea ujasiliamali wake kwa vielelezo.
kama wewe ni muumini utakubaliana na mimi kuwa siku hizi kanisani masuala kuhusu fedha yanapewa kipaumbele sana kuliko kuhubiri neno la Mungu. Suala la kulifanya kanisa lijitegemeze limegeuka kuwa msingi wa imani. Michango ya fedha kwa ajili ya shughuli za kanisa ndicho kipaumbele, uanzishwajiw a miradi unachukua nafasi ya mahubiri nk.nk.nk
 
wewe kila jimbo linajengwa kutokana na michango ya waumini, tuna harambee za kila mwezi kwa ajili ya kujenga hayo makisa na hizo dawa za kulevya labda wewe ndo mnunuzi wa hizo dawa ndo mana unahisi tunauza dawa za kulevya, pesa za waumini ndo zinazojenga makanisa, shule na hospital. amia katoliki ndo utaelewa kinachofanyika.

Kwamba hizo pesa za harambee atakayowasaidia Lowassa zitatumika kujenga jimbo jipya la Ifakara sio maneno yangu bali ya mwenyekiti wa shuhuri hiyo ambaye pia ni mpiga chapa mkuu wa serikali!!
 
Back
Top Bottom