Kanisa katoliki mmekubali kujichafua na pesa za Lowassa?

Uko sahihi sister ila haina maana kuwa kwa kuwa sote ni wakosefu basi tusikemee maovu. Sidhani kama Jesus alimaanisha hilo!!!!
kukemea ni tofauti na kuhukumu, huyu anahukumu kwa nini kanisa limruhusu lowasa na achangie kwenye kanisa lakini kukemea ni kukataza mtu asifanye maovu na kanisa linakemea hilo ila halimhukumu mtu na kumkataza asihudhulie kanisani kisa ni muovu.
 
Ndugu yangu Isango nakujua wewe umepata kusoma seminari, mara hii umesahau kuwa kanisa halimuhukumu mtu kwa kuwa tu wewe unamtuhumu!!! halafu pia mtu hata kama ana dhambi lakini kuna maungamo ambayo ni ya siri..! hakuna dhambi ndogo na kubwa wala sadaka kubwa na ndogo, hebu kumbuka mara ngapi tumezini, mara ngapi tumesengenya, mara ngapi tumedanganya au umetukana na kuwaza mabaya !!!!! bila mie kujua umetubu ama hujatubu lakini bado kanisa linapokea sadaka yako na wakati mwingine kushiriki meza ya Bwana. jamani tusitake kanisa lifanya kazi Kidunia kama mfanyavyo ninyi. hata mamlaka zenyewe zilizopewa haki kisheria kudeclare kuwa somebody is.guilty hazijawahi kufanya hivyo??? Ahhhhh.... hata kama humpendi Mzee EL lakini usilisakame kanisa kwa kuwa lipo kwa ajili ya kila aitwaye binadam

Ndugu yangu hoja ya Isango siyo kwamba Lowasa ni mdhambi hivyo asishiriki huduma za kanisa. Kabla sijaendelea kukujibu naomba nikupe mfano mmoja: Kuna baba mmoja alikuwa akiisaidia sana kanisa katika michango na harambee za kanisa na hata kuwasaidia mapadre binafsi. Baadaye huyo baba akawa amempeleka mtoto wake akasome seminari (huko alikosoma Isango) kwa ajili ya malezi ya kipadre. Seminari hiyo ilikuwa na viwango vyake vya wastani wa kufaulu masomo. Ikatokea mtoto wa huyo baba akashindwa kufikisha wastani na hivyo mtoto akatakiwa kurudia darasa au aondoke seminarini. Huyo baba alianza kumfokea kiongozi wa seminari iweje mtoto wake arudishwe darasa na kwamba yeye amelisaidia sana kanisa.

Lowasa kama muumini (ingawa sidhani kama yeye ni muumini wake) kanisa katoliki halina shida na dhambi zake lakini kuna tatizo katika suala la yeye kuwa mgeni rasmi katika harambee hizo ambazo mwenye akili timamu anajua yana malengo ya kisiasa nyuma yake. Tukirejea nyuma wakati anagombea urais mwaka 1995, tunasikia kuwa Mwalimu Nyerere alimwambia kuwa kijana una fedha nyingi sana ulizipata wapi? Mashaka makubwa waliyonayo watu ni mali zake nyingi alizonazo na kwamba anataka kuzitumia kwa malengo ya kufika Ikulu.

Tukio la Lowasa kuongoza harambee siyo la kwanza katika kanisa katoliki. Aliwahi kuongoza kule Nyakato - Mwanza ambako suala hilo lilihojiwa vile vile na watu. Ninajua kuwa kanisa halijawa na mfumo wa kuhoji madhambi ya watu hadharani lakini vile vile ninajua halipaswi kudadisi mwenendo wa waumini wake hasa ule unaokwaza watu. Kama Lowasa anatajwa na watu kuwa ni fisadi kwa upande mmoja na huko kanisa katoliki linataka kusema kuwa Lowasa ni safi kwa upande mwingine basi kuna haja kuwa na muafaka katika suala hilo.

Katika mashaka ya kuwa Lowasa ni fisadi au la kanisa linapaswa kuwa salama kwa lolote litakalothibitika kati ya hayo. Lowasa alijiuzulu kwa kashfa ya Richmond huku wengine wanasema alijiuzulu kuokoa serikali na hata wale mawaziri aliojiuzulu nao wakasemakana wametolewa kafara. Kama tunakubalina kwamba kulikuwa na kashfa ya Richmond na kuwa ukweli katika hilo na hayo yalitendeka chini ya serikali ambayo yeye alikuwa waziri mkuu wake, Je? yeye kama waziri mkuu alikuwa na mchango katika kushiriki hayo yatokee au yasitokee? Yeye anakuwaje safi hivi hivi? Lowasa anasema alikuwa akimshirikisha rais kila kitu kilichokuwa kikitendeka, ina maana alikuwa akimshirikisha hatua zote za ufisadi ili utendeke? kama hakupenda ufisadi usitokee kwanini hakujiuzulu kwa sababu ya hilo?

Kama kanisa katoliki linataka kumtangaza Lowasa kuwa mtakatifu kwa sababu anatoa michango mikubwa mikubwa hakika ninaona sasa viongozi wa kanisa wanataka kuliondoa kanisa toka mikononi mwa Kristu aliye mwanzilishi wake. Kanisa la asili la Kristu lilikuwa la wanyonge lakini watu wanopenda na kutetea haki. Hata kama halina nguvu za kiuchumi halipaswi kununuliwa na wenye fedha kwa malengo yake. kanisa linawapa watu sakramenti ili wapate wokovu bila gharama yoyote. leo linakimbilia fedha za Lowasa kwa ajili ya nini?

Nina mashaka makubwa sana kama viongozi wa kanisa wakakwepa kumpigia kampeni Lowasa wakati atakapoitisha harambee ya kuwania uongozi. Huo ndio mwelekeo wa ushirikiano wa viongozi hao wa kanisa na Lowasa. kama sasa hivi wamefungua milango ya ushirikiano wataweza kufunga wakati Lowasa atakapowapelekea ombi lake?
 
kukemea ni tofauti na kuhukumu, huyu anahukumu kwa nini kanisa limruhusu lowasa na achangie kwenye kanisa lakini kukemea ni kukataza mtu asifanye maovu na kanisa linakemea hilo ila halimhukumu mtu na kumkataza asihudhulie kanisani kisa ni muovu.
Sister fafanua vizuri! Kanisa ndio linamwomba El akawasaidie kukusanya fedha!
 
Sister fafanua vizuri! Kanisa ndio linamwomba El akawasaidie kukusanya fedha!
hapana sijamaanisha hvyo , ni kwamba yeye alialikwa tu kama kiongozi na kama kawaida inavyofanyika viongozi wanaalikwaga.
 
Umesema mengi juu ya mali za Kanisa Catholic ila umesahau kubwa kuwa vile vile wana watu ambao ni wasomi waliobbobea na wenye kujua mambo kwa undani akiwemo Balozi wa Papa na hivyo wanavyoamua au wanavyofanya maamuzi wanajua wanachoamua; bado hawajakosea hata kidogo kwa kumpa Edward jukumu hilo huku nje ndio tunaokosea........ Edward kafanye kazi ya Bwana naye yupo tayari kufungua mapito yako imeandikwa kila ulimi na kila silaha itakayo nyanyuka juu yako atauhesabu kuwa mkosa............
 
Ebu tuondolee siasa za majitaka za CCM ktk kanisa letu. Sioni tatizo lolote kualikwa kwa Lowassa ktk harambee. Tuache kushabikia viongozi wanaopenda umasikini ndiyo maana nchi yetu licha ya utajiri mkubwa ilionao bado ni masikini.
 
Huwa wenye Dhambi Milango ya Kanisa Huwa Wazi Kwa ajili yao!! Nadhan Hata Kwenye Bibilia kuna mtoza ushuru mmoja alitakiwa na Yesu arudishe Kila alichochukua kwa Dhuluma awarudishie Wahitaji!! Sasa Muheshimiwa amechagua Njia Hiyo!! Mimi sioni Kama kuna Tatizo!!
 
Wazazi kumuita mtu mwizi bila kusema alichoiba tunachuma zambi tu ;na kuna ubaya gani kama mtu pochi nzito akiamua kupunguza au tatizo ni kupunguzia makanisa? huenda Edo anaprogramu mzuri kwa mwadau wote maana 2015 mbali kimtindo.Mtu mzima Pengo vuta huo mpunga upesi ikibidi kabla ya tarehe ya harambee maanake wachawi washaanza kuwanga.
 
Mie najua huwezi kutubu na kupokelewa kabla hujapatana na ndugu zako...
...Mbona sijasikia akituomba msamaha?
Mkuu, kwani kupatana lazima yeye akuombe msamaha? Inawezekana katika kupatana huko, wewe ndio ukatakiwa umuombe msamaha.
 
Kwa hakika yale yote ayafanyayo mwanadam ambayo ni chukizo kwa Mungu,matokeo yake ni hapa hapa! Najisikia vibaya sana kuskia au kuona Lowasa, Fisadi na Tapeli asiyeshiba bado kunawatu wanamnyenyekea na kumlamba miguu!! Wakatoliki tumekosa nini mpaka kushirikiana na wanyang'anyi kulijenga kanisa?? Yesu siku moja akiwa kwenye sinagogi aliikubali sadaka ndogo ya mama mjane kwa sababu aliitoa kutoka moyoni kuliko sadaka za wale matajiri!! Hata kama ufisadi wa Lowasa bado ni tuhuma, bado haitoshi kuona kwamba ni msafi! Kwa vile alituhumiwa hadharan hana budi kusimama hadharani na kutubu na kuweka mambo yote yanayomuhusu hadharan kama kweli anataka kuwa mtakatifu! Kinyume na hapo niwasihi na kuwaomba kutomualika tena na hata akiomba tumkatalie kwa nguvu zote! NI AIBU NA TUTAONEKANA WAVIVU WA KUFIKIRI NA WAPUMBAVU KWA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MATAPELI,WANYANG'ANYI NA MAFISADI ETI TUNAJEGA KANISA! KWELI HUYU TAPELI AKIWA RAIS TUTAPONA?????
 
Nimeangalia hapa chini nimeona Mh Dr Slaa naye kapaki anasoma huu mjadala kiaina.

Edward Lowassa ni mwizi, piga ua.

Edward Lowassa hakuiba London ameiba hapa Tanzania kwa kutumia mabenki yetu na udhaifu wa serikali ya CCM.
Pia katumia watanzania wenzetu kuiba.
Hatulipwi kusema yote haya kama wengi wanao tetea face valuee ya ED wanavyotegemea some kind of reward.

Edward Lowassa alitia ubabe kuileta Richmonduli,piga ua.
Edward Lowassa kama walivyo wezi wengi wa Kitaifa wenye kujikweza na kuwa juu ya sheria ya nchi hajashitakiwa.

Uliwahikuona wapi fisi akatamani nyama ya fisi mwenzake??
Hata Fisi na Uroho wake haramu yake ni nyama ya fisi mwenza. That is a number 1 Rule of CCM government.
Fisadi wa CCM hawezi kushitakiwa na Mafisadi wenzie, sisi tulio nje ya wigo wa mafisadi ndio wenye uwezo wa kumtia lupango yeye Edward Lowassa na mashoga zake.

Harakati za Edward Lowassa ni za kuisave nafsi yake na za Mafisadi wenzake.
Anajua kitakacho mpata yeye na wenzake nguvu ya umma ikirudisha heshima ya nchi.
Si mnajuaFani ya Lowasa pale UDSM ilikuwa ni Thamthiria??
Usanii wa Edward Lowassa ni wa Cheti siyo wa kubabaishia.

Kutoshitakiwa kwake Edward Lowassa hakumfanyi asiwe mwizi.
Kutoa Mabilioni kwenye Harambee za makanisa ni kujaribu kujiosha lakini hakumfanyi asiwe mwizi.
Kuwa mgeni Rasmi kwenye Harambee za Kanisa Katoliki kuna zusha maswali makubwa na yenye Utata.
Huyu Mlutheri kawapa nini Makasisi wa Kikatoliki hadi kumfanya awe mgeni rasmi.

Kanisa katoliki kwa kawaida ni very Conservative, haitwi mtu kuwa mgeni rasmi hivi hivi tu.
Angekwenda kama mualikwa wakawaida hizi kelele zote zisingekuwepo.
Hilo Jopo la maaskofu na mapadre waliomualika mimi binafsi nina wasi wasi nalo ningependa kujua ni akina nani.
 
tuimbe "Toa ndugu toa ndugu ulichonacho wewe bwana anakuona mpaka rohoni mwako x 1000 Kanisa katoliki vuteni mpunga wenu makahesabie pembeni mpishe wengine mijadala baadae MASHEHE WASHA NAWA
 
Tunaliheshimu sana Kanisa Katoliki, Tunawaheshimu sana viongozi wake. Kanisa Katoliki angalau mpaka ninapoandika uzii huu ni Kanisa tajiri sana, linamiliki Taasisi muhimu sana, Hospitali, Zahanati, vituo vya Afya, Shule za chekechea, msingi Sekondari, Vyuo, na vyuo vikuu, Bahati mbaya sana kanisa Katoliki linamiliki hadi Mkombozi Benk. Kanisa Katoliki linapata sadaka na michango mbalimbali toka kwa waumini wake, ni kanisa ambalo kweli halipaswi kulia njaa, hadi kiwango cha kukimbilia Pesa ambazo zinazua maswali mengi. Walioandaa Chakula cha Hisani kwa ajili ya uanzishwaji wa Jimbo Katoliki Ifakara, walikosa mtu mwingine hadi wamwite Lowassa tu? Wameenda wapi viongozi wa dini wenye maadili mazuri, mfano Balozi wa baba mtakatifu, mwadhama Kardinali, Maaskofu wakuu, Wakuu wa Mashirika au watu wengine? CCM walitamka wao kwa kinywa chao kuwa Lowassa ni FISADI. Nimejisikia vibaya sana kuona Kanisa limeamua kutoangalia upandaji wa maisha ya watanzania wa sasa kwa sababu ya gharama za Umeme amabazo chanzo chake kimekuwa Richmond, Dowans. Kweli mmeamua kuyaishi yale mliyoyalaani?. Angalau kwa ajili ya wenye dhamiri changa mngeacha hili. Mihi Vivere Christus est......................

Kwenye red



Ni kweli Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume linamiliki hivyo ulivyooredhesha; swali Jee mahosipitali na mashule ni huduma au ni biashara? Serikali ya Tanzania inamiliki vyuo vingi sana, mashule mengi sana na hospitali, vituo vya afya na zahanati nchi nzima....kama kwa huu ni utajiri mbona tunaendelea kulipa kodi na serikali inaendelea kuomba misaada nchi za nje?

Acheni kukashifu, huduma za jamii ni kwa ajili ya watu wote na zinagharamiwa na watu wote wazuri na wabaya (kwa mtazamo wako?
 
Sidhani kama kuna kanisa hapa duniani lenye utaratibu wa kuhoji muumini ni wapi alipozitoa sadaka anazotoa kanisani, hii ndio nitakuwa naisikia mara ya kwanza. Hata Yesu alipomuona Zakayo mtoza kodi, alimwambia ateremke kwenye mti, ili waende nyumbani kwake Zakayo kula karamu pamoja. Zakayo mwenyewe binafsi aliamua kuchukua fedha zake na kuzigawa kwa maskini. Mbona Yesu hakuzuia hela ya Zakayo kugaiwa kwa maskini?
 
Mkuu, kwani kupatana lazima yeye akuombe msamaha? Inawezekana katika kupatana huko, wewe ndio ukatakiwa umuombe msamaha.

EL hana sababu ya kuniomba msamaha mimi binafsi bali watanzania ambao alishiriki kuwasababishia madhara makubwa ikiwemo vifo kwa sababu ya dili lao la Richimond na madili mengine ya kitapeli.

Mie nimwombe msamaha nimemkosea nini?

Ila kwa vile anamwaga pesa...may be kabla ya 2015 nitamwomba msamaha!

Babu DC!!
 
mimi ni mkatoliki lakini mambo ambayo yanayofanywa na kanisa langu yananitia kichefu chefu. wewe angalia tuu kwa mfano, mambo yote ambayo nyerere aliwaudhi watanganyika katika operesheni vijiji, kuwaweka detention tumtemeke sanga, mapalala, fundikila saidi na kasanga tumbo na kuuwa erikali za mitaa lakini bado wakatoliki wanamwita mtakatifu!

Lowassa ni paulo ana mikono michafu hawezi kucheza na sisi lakini wakatoliki wanamuita mwenye busara na wanamualika katika fund rising! hivi maaskofu wa kanisa katoliki ni raia kweli wa nchi hii?
 
Back
Top Bottom