Rais Samia, ukiongezea Kanisa misamaha ya kodi, Wananchi na watumishi tupewe misamaha pia ili tumudu huduma za Kanisa

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,208
42,068
Nakusalimu Mhe. Rais,

Kwanza ni ukweli ulio wazi kuwa kanisa hasa la Katoliki limekuwa likitoa huduma nyingi sana kwa jamii hasa katika elimu na afya na wamekuwa wakitoa msaada mkubwa sana kwa jamii na serikali kwani wamekuwa wakichagiza maendeleo kwa ujumla na hutoaji huduma.

Ukweli ni kwamba pamoja na hutoaji huduma huo bado kanisa linatoa huduma hizo kwa bei ya juu sana na ghali ambazo wanaozimudu ni matajiri na kama huna bima hasa kwenye mahospitali yao uwezi kupata huduma kwani utaweza kulipa cash kutokana na gharama kubwa ya huduma.

Ni wazi kwa sasa ni ngumu kutofautisha kabisa huduma na baishara hasa kwenye hospitali za makanisa na mashule yao.

Hata kwenye shule zao bado gharama kubwa sana ni vigumu kuelewa mtu anayetaka kusamehewa kodi huku anatoza ada ya 10million wakati kuna wenzao wanatoza hiyo hiyo ten million kama ada na hawana msamaha wa kodi.

Inatia shaka sana kumsikiliza Nyaisonga akitaka msamaha wa kodi wakati msamaha huo haumgusi kabisa mwanachi wa kawaida na wengi hawamudu huduma zinazotolewa na makanisa.

Makanisa mengi yamekuwa yakifanya baishara kama wafanyabiashara wengine ambao nao wanastahili huruma ya kodi kama kanisa
Kanisa linamiliki biashara za maduka, mashule, guest house, dispensary na hospitali nyingi lakini ni ngumu kutofautisha biashara hizi za kanisa na biashara za watu wengine, kwa hiyo ukiniuliza nani anastahili msamaha wa kodi basi ni kila mfanya biashara ana stahili msamaha wa kodi kama kanisa maana hawana tofauti kabisa kwenye huduma zao.

Mh Rais, Padri Nyaisonga ameshindwa kukuambia jinsi huduma zinazotolewa na kanisa ni za bei rahisi kuliko wengine ili astahili msamaha wa kodi ameshindwa kuonesha hilo kwakuwa halipo na kanisa linafanya biashara kama wafanya biashara wengine na wanashindana na wafanya biashara wengine na lazima walipe kodi kama watanzania wengine wote.

Mh Rais kila mtanzania ana stahili msamaha wa kodi na kila Mtanzania anatakiwa kulipa kodi nanayo stahili na hii ndio haki yenyewe lakini sio wengine wapewe msamaha wengine wasipewe halafu bado kwenye gharama hawana tofauti.

Kanisa linapewa misamha mingi sana lakini ukweli ni kwamba bado misahama hiyo haigusi wananchi bali ni wao kutengeneza faida tu waingiza magari kwa mlango wa kanisa na vitu vingine halafu yanakuwa ya biashara kama wafanya biashara wengine.

Kama ni msamaha wa kodi basi hata wafanyakazi wanastahili zaidi msamaha wa kodi ikiwezekana makato ya kodi yashuke hadi 3% hii itasaidia kumudu gaharama za huduma zinazotolewa na kanisa.

Pia na wafanya biashara wote nao wapewe misamaha ya kodi hasa wanao miliki mashule na mahospitali hii ndio itakuwa haki kwa wote.

Kwako Mh Rais
 
Kodi waSamehewe 7X70
Huduma nzuri bei ghali
unakuta hz hospital zina good service yaan unakuta chumba kina mgonjwa mmoja / hawazidi 10.
Tena madaktari wanafanya kazi zao 24/7
Wanavifaa bora na vya kisasa

So wache watoe huduma kwa bei ghali.
 
Ashushe msamaha kwa msanii kama Gwaji boy?

Hii hapana, ataje kabisa aina ya makanisa, si hawa matapeli wa kukanyaga mafuta, mara sijui nabii kitu gani, mashimo, apana aisee.
 
ashushe msamaha kwa msanii kama Gwaji boy?
hii hapana, ataje kabisa aina ya makanisa, si hawa matapeli wa kukanyaga mafuta, mara sijui nabii kitu gani, mashimo, apana aisee.
hahahahaha
 
Kodi waSamehewe 7X70
Huduma nzuri bei ghali
unakuta hz hospital zina good service yaan unakuta chumba kina mgonjwa mmoja / hawazidi 10.
Tena madaktari wanafanya kazi zao 24/7
Wanavifaa bora na vya kisasa

So wache watoe huduma kwa bei ghali.
Sasa hii si biashara na wanaofanya hivyo si makanisa pekee hata hospitali binafsi wanatoa huduma hivyo basi na wao wasamehewe
 
Mama alishasema yeye ni kama hayati. Hayati hajawahi kusikika akitaka kusamehe kodi. Hapana walipe kodi kama wananchi wengine nchi bado inahitaji kujengwa.

Huduma zao zina bei ghali sana na wanaozimudu ni wenye kipato kikubwa kwa hiyo naunga mkono hoja kwamba walipe kodi stahiki.
 
Mama alishasema yeye ni kama hayati. Hayati hajawahi kusikika akitaka kusamehe kodi. Hapana walipe kodi kama wananchi wengine nchi bado inahitaji kujengwa.

Huduma zao zina bei ghali sana na wanaozimudu ni wenye kipato kikubwa kwa hiyo naunga mkono hoja kwamba walipe kodi stahiki.

Umeanza vizuri halafu ukaharibu mwishoni. Unachokitaka kiko duniani kote na hasa afrika. Huduma ambazo ni kwa maslahi ya umma husamehewa baadhi ya kodi - nia ni huduma kupatikana (sio gharama ya huduma). Gharama ya huduma huendana na ubora (watumishi, miundombinu na vifaa). Ndio maana unaona hospitali binafasi zina vitu vyote hivo ya kutosha wakati huduma za bei za chini ziko katika hospitali za serikali huku zikiandamana na ukosefu wa madaktari, miundombinu na vifaa tiba na madawa!!

Ungejua kodi wanayotozwa ni kidogo usingewaza unayowaza. Ni kidi ya forodha tu. Kodi nyingine kama za mapato, VAT, property tax na huduma wanalipa. Serikali inawapunguzia kama shukrani kwa kuleta huduma za kijamii. Unajua kwamba hospitali zao kuna wafanyakazi wanaolipwa sehemu ya mishahara na serikali??

Umekiri kuwa huduma za bei aghali kuna wanaozimudu. Acha hao wawe na sehemu yao, ukitaka waje huku chini, kutakuwa na mkanganyiko!!
 
Back
Top Bottom