Kanisa katoliki mmekubali kujichafua na pesa za Lowassa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa katoliki mmekubali kujichafua na pesa za Lowassa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Isango, Feb 27, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tunaliheshimu sana Kanisa Katoliki, Tunawaheshimu sana viongozi wake. Kanisa Katoliki angalau mpaka ninapoandika uzii huu ni Kanisa tajiri sana, linamiliki Taasisi muhimu sana, Hospitali, Zahanati, vituo vya Afya, Shule za chekechea, msingi Sekondari, Vyuo, na vyuo vikuu, Bahati mbaya sana kanisa Katoliki linamiliki hadi Mkombozi Benk.

  Kanisa Katoliki linapata sadaka na michango mbalimbali toka kwa waumini wake, ni kanisa ambalo kweli halipaswi kulia njaa, hadi kiwango cha kukimbilia Pesa ambazo zinazua maswali mengi. Walioandaa Chakula cha Hisani kwa ajili ya uanzishwaji wa Jimbo Katoliki Ifakara, walikosa mtu mwingine hadi wamwite Lowassa tu?

  Wameenda wapi viongozi wa dini wenye maadili mazuri, mfano Balozi wa baba mtakatifu, mwadhama Kardinali, Maaskofu wakuu, Wakuu wa Mashirika au watu wengine? CCM walitamka wao kwa kinywa chao kuwa Lowassa ni FISADI. Nimejisikia vibaya sana kuona Kanisa limeamua kutoangalia upandaji wa maisha ya watanzania wa sasa kwa sababu ya gharama za Umeme amabazo chanzo chake kimekuwa Richmond, Dowans.

  Kweli mmeamua kuyaishi yale mliyoyalaani?. Angalau kwa ajili ya wenye dhamiri changa mngeacha hili. Mihi Vivere Christus est......................
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Dini ipo kwa ajili ya wenye dhambi na sio watakatifu,fikiria upya,acha wenye dhambi wakatubu na kutoa walichochukuwa,hakuna mahala pengine pa kufanya kitubio zaidi ya kwenda huko kanisani..
   
 3. sister

  sister JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  unajua nini hatupaswi kumuhukumu mtu bali mtoa hukumu ni mungu pekee, na hata kwenye biblia Yesu alisema ambaye hana dhambi na achukue jiwe mrushie huyu mama akuna aliyefanya hivyo unajua kwa nini? kwa sababu no one is perfect in this world, na pia Yesu aliandaa kalamu na wenye dhambi wale wanojihisi ni wasafi wakakasirika lakini Yesu akasema sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu.
   
 4. sister

  sister JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa. LIKE
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kwani Lowasa anaenda makanisani kutubu? Na ili akatubu lazima aarikwe?


  Makanisa yote yaliyoingia kwenye mtego wa Lowasa yamepotoka na yanajichimbia makaburi yake.....!

  Babu DC!!
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Aliye mzima hahitaji tabibu, kumbuka hata Yesu alikula na kunywa na watoza ushuru na wenye dhambi kama Zakayo, Lawi na wengineo, lengo lake ni kuwahubiria ili watubu hivo hawa wenye pesa chafu (ambao wewe umeshawahumu pamoja na kuwa biblia inatukataza tusihukumu tusije kuhukumiwa) kama wanakuja kanisa acha waje ili wapate kutubu na kuokoka.

  Paulo hapo awali akijulikana kama Saulo alikuwa mtu mbaya sana akiwaua na kuwatesa waliomuabudu kristo lakini Yesu mwenyewe alimuita akamfanya chombo chake kitakatifu so hawa uliowahukumu wewe acha nao wapate fursa ya kuongoka kama mtakatifu Paul
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Are you serious?

  Kama ni hivyo, mahakama na polisi vinafanya kazi gani? Kwa nini tunapoteza pesa nyingi sana za walipa kodi kughalimia vyombo hivi?

  Babu DC!!
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  EL haendi kanisani mwenyewe bali anaitwa na kupokelewa kwa mikono miwili na wachunga kondoo wenye tamaa ya pesa zake....Can't you see that difference?

  Babu DC!!
   
 9. sister

  sister JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  I am very serious, ila kumbuka ya kaisari mwachie kaisari, na ya mungu mwambie mungu. na biblia inasema heshimuni taratibu na sheria za nchi zenu.
   
 10. sister

  sister JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  kuitikia wito kwanza ni jambo la busara mana anaweza kuitwa na asiende vile vile au akawakatalia, hivi wale wote wanaotoa michango unajua hela wametoa wapi?
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kweli nimekubali kwamba kufikia 2015 tutaona mengi,

  Kwa hiyo EL amekuwa mtu wa Mungu na kwa hiyo mambo yake ya siasa nayo yamekuwa ya Mungu...Sasa ya Kaisari ni yapi tena?

  Babu DC!!
   
 12. sister

  sister JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo akitubu unataka atangaze kama ametubu?
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naomba tuanze na EL,

  Hizo milion 20, 30 anazota anazipata wapi?

  Tunamjua hajawahi kuwa mfanyabiashara maarufu..Amekuwa kwenye utumishi wa umma toka akiwa kijana....Kwa sasa ni mbunge ambaye mshahara wake ni less than 10mil.

  Hizo za kutoa sadaka amezipata wapi?

  Babu DC!!
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwani keshatubu?

  Mie najua huwezi kutubu na kupokelewa kabla hujapatana na ndugu zako...

  Yeye alitukosea kwa kutuingiza kwenye madudu ya Rich...Mbona sijasikia akituomba msamaha?

  Au kwa kuwa anatoa dau, kanisa limeamua kumpa kitubuo cha short cut?

  Babu DC!!
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama makanisa yanakubali fedha kutoka kwa mafisadi, kitu gani kitawazuia kufanya biashara ya madawa ya kulevya yanayoingiza pesa nyingi zinazoweza kutumika kujenga jimbo jipya?The Roman Catholic church is indicting itself!!
   
 16. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Mwadhama Pengo , usiandike historia chafu nyuma yako. Lowasa watu wana wasiwasi na usafi wake. Hata baba wa taifa alikuwa na mashaka nae na aliacha amemfuta kwa watu wa kuaminiwa.

  Kwa nini mnakuwa karibu naye? Mtu hataingia mbinguni kwa vile alikuwa na fedha bali usafi wa roho.Heri maskini wa wa mali maana watauona ufalme wa Mungu
   
 17. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bado narudia,

  Kanisa katoliki hawajakurupuka, ni watu walio makini sana. Waamuacha sio Aamuacho, ni jopo linaamua. Hivyo naamini kabisa Kanisa Katoliki limejishibisha juu ya tuhuma zote juu ya Lowassa, linajua anahusikaje au hahusikaje.
  Kanisa Katoliki linaye waziri mkuu aliye madarakani ambaye ni muumini wake, je halikumuona na kumualika aende pale na ving'ora na wapambe lukuki?

  Hawa jamaa naamini fika WANAJUA WAFANYALO, NA WAKIAMUA KUYAWEKA BAYANA JUU YA SAKATA LA KUCHAFULIWA EL...nchi itayumba. Hawajakurupuka RC, ndio maana tangu sakata la EL lilipoanza jamii haijawahi kupokea karipio lao kupitia kwa Ruzoka etc.
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kama Lowassa angekuwa na makosa ambayo tunataka ahukumiwe basi asingekuwa Bunge, asingekuwa mjumbe wa NEC - CCM, asingekuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya bunge. Lowassa angefunguliwa mashitaka tungejua kweli ana makosa.

  hapa ni kulionea kanisa kwa kumtumia Lowassa wakati chama chake hakijathibitisha hilo ama kwa kumfungulia mashitaka au kumpokonya uanachama. Kwa nini tunataka kanisa ndilo limuadhibu Lowassa wakati kisiasa haijawekwa wazi kama ni fisadi/si muadilifu?

  Kama si mwadilifu angeendelea kukitumikia chama chake?
   
 19. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kwanza akubali dhambi aende kuonana na pilato kama anataka kutubu akatubu kuleeee kwa walutheri
  siyo kila kwenyemnuso wa kanisani namsikitini yeye anasogeza pua kisiasa.
  Hata Adolf Hitler alitumia mistari ya biblia kuuza sela zake.
  Ibilisi naye alitumia mistari ya Torati kutaka kumdanya Yesu na kumwingiza majaribuni.

  Lowassa anatubu kwa kumwaga pochi nene pale wapiga kula watakapo sikia nguvu yake.

  Renpeting Lowassa style.

   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Lowassa ni muumini wa dini hiyo, kanisa si chombo cha uchunguzi kama ilivyo kwa PCCB iweje litoe hukumu kwa Lowassa wakati hakuna chombo cha uchunguzi kilichotangaza hukumu kwake Lowassa.
   
Loading...