Jaman hapa kinachotakiwa kwangu ni ushauri wenu tu baaaaaaasi.
Nikirejea nyuma kdg....kuna yule mdada niliyewahi kuwapa story zake hapa kuwa nilimlipia nauli kwny daladala then jamaa yake akanirudishia sh elfu 5, baada ya cku kadhaa tukaonana tena akaninunulia na bua moja ya kucndikiza lunch, baadae akanitambulisha tena kwa jamaa yake, jamaa akaniangalia kwa dharau sana hadi nikatamani kumnasa makofi baadae nikagundua kumbe dharau zake ni kwa sababu anamiliki bastola.
Hiyo sio habar niliyokuja nayo leo...hapo nilikuwa najaribu kuwarudisha nyuma ili muelewe ninachotaka kukiuliza kwenu, kama mtakumbuka yule mdafada alinipa simu yake nikaandika namba za simu yangu.
Sasa leo kwny saa 5 hivi asubuhi kanipigia na kuniomba kuwa nifanye niwezavyo lakin nihakikishe kesho tunaonana....... sasa hicho ndo ninachoomba ushauri kwenu wakuu, hivi niende au nisiende maana nahofia isijekuwa naingizwa kwny mtego mbaya.