GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Mwanza, Shinyanga, Kahama, Geita, Kagera, na Kigoma! Kote huko sijawahi kukutana na ndizi mshare. Ndizi zinazopikwa maeneo tajwa ni ndizi ambazo kwa Arusha na Kilimanjaro, ukikuta mtu kazipika, ujue ni amekosa kabisa cha kupika. Si matumizi yake.
Nilikula ndizi kwa mara ya kwanza jijini Mwanza mwaka 2010. Nilishangaa nilipokuta ni ndizi ambazo kwa Arusha na Kilimanjaro zinatumika kwa kupikia mtori au kuvundikwa kwa ajili ya kutengenezea pombe. Nilikula kwa kuwa sikuwa na namna, isitoshe, nilikuwa ugenini na ziliandaliwa kwa ajili yangu.
Tokea nikiwa mdogo, nilikuwa nikijua kuwa ndizi zinazotumika kupikia "ndizi" ni NDIZI MSHARE, KIMALINDI, n.k., lakini si ndizi ng'ombe.
Ni kwa nini hizo ndizi hazipatikani Kanda ya Ziwa?