Kanali Muammari Gadafi katika kitabu cha kijani- kuhusu Bunge na chama

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
images (5).jpeg
BUNGE

BUNGE ni uti wa mgongo wa demokrasia ya uongo iliyopo kwenye ulimwengu wa sasa. Bunge sio uwakilishi wa watu na mfumo wa mabunge sio suluhu katika matatizo ya demokrasia.
Bunge kwa asili liliundwa kuwakilisha watu lakini kitendo hiki chenyewe si cha kidemokrasia kwakuwa demokrasia maana yake ni mamlaka ya watu na sio mamlaka kwa niaba ya watu. Kuwepo kwa bunge maana yake ni kutokuwepo kwa watu. Demokrasia ya kweli inakuwepo pale tu panapo kuwepo na ushiriki wa moja kwa moja wa watu na sio kwa shughuli za wawakilishi wao.

Kama bunge litaundwa kwa wawakilishi wanao tokana na chama kutokana na kushinda kwake katika uchaguzi basi litabaki kuwa bunge la chama kilicho shinda na sio bunge la watu kwa hiyo litawakilisha chama na sio watu.

Hali kadharika kwa bunge lililoundwa kwa uwakilishi sawa wa vyama ambapo kila chama kina viti kutokana na ushindi wao katikanuchaguzi bado wabunge watawakilisha vyama vyao na sio watu na nguvu yao ni nguvu ya vyao na sio ya wananchi.

Pia kama bunge litatokana na propaganda katika kushinda kura, kura zinaweza kutengenezwa kwa udanganyifu, watu masikini hawawezi kushindania uongozi na matajiri tu ndio wanao chaguliwa. Mabunge yanayo undwa kwa kuteuliwa kuingia kwa nyadhfa zao hayaingii katika aina yoyote ya demokrasia.

Baada ya kufanikiwa kuunda mfumo wa jamuhuri na kuanza kwa tawala za wengi si jambo la kufikilika kuwa demokrasia ni kuchagua wawakilishi wachache kutenda kwa niaba ya wengi. Huu ni mtindo wa kizamani. Mamlaka yafaa yawe katika mikono ya watu wote. Kiwango cha juu cha udikteta hivi sasa kimekuwepo katika kivuli cha mabunge.

Tiba
Kwakuwa mabunge yamekuwa namna ya kunyonya na kunyakua mamlaka ya watu. Ni haki ya watu kupambana kupitia mapinduzi ya wengi kuharibu chombo kiitwacho BUNGE kinacho nyakua demokrasia na nguvu ya madola na kukandamiza hiali ya wengi.
Wengi wanapaswa kudai pasipo kuchoka kanuni mpya yaani " hakuna uwakilishi badala "in lieu" ya watu.

CHAMA
CHAMA ni mfumo mwingine wa kisasa wa kidikteta ni chombo cha kisasa cha serikali za kidikteta. Chama ni mamlaka ya chama dhidi ya wengi. Chama sio chombo cha kidemokrasia kwa kuwa ni watu wenye maslahi sawa, mtazamo sawa wanaweza kuwa na utamaduni mmoja hata dini na imani moja. Wanaunda chama kutimiza hatma zao. Kutekeleza matakwa yao au kukuza imani yao thamani na maslahi katika jamii kwa ujumla.

Kidemokrasia chama hakiwezi kutawala watu wenye maslahi tofauti, dhana tofauti, dini tofauti na imani tofauti.

Mfumo wa kichama ni mfumo wa kisasa wa kikabila au kidhehebu. Jamii inayotawaliwa na chama ni sawa tuu na ile inayotawaliwa na kabila au dhehebu. Chama huwasilisha mtazamo wa watu furani au maslahi ya kundi furani katika jamii au kwa niaba ya ukanda mmoja.

Pengine ni damu inaweza kutofautisha kati ya kabila na dhehebu. Mapambano ya chama kutawala watu kama yalivyo mapambano ya kabila kutawala au dini hayawezi kukubalika.
 

Attachments

  • gaddafi-green-book.pdf
    278.7 KB · Views: 7
Back
Top Bottom