Kampuni sita zasaini mkataba wa awali kununua korosho nchini Tanzania

Serikali imesaini mkataba wa awali na kampuni sita ya kununua korosho kati ya zilizoomba kununua korosho hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 16, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema baada ya Kampuni ya Indo Power ya nchini Kenya kushindwa kununua korosho wameendelea kusaini mikataba ya awali.

“Tumeendelea kusaini mikataba ya awali na kampuni nyingine hadi sasa tumesaini na kampuni sita,” amesema.

Amesema asingependa kuzitaja kampuni hizo kwa sababu ya hali halisi ya biashara ya korosho duniani ambayo kwa sasa watu wanafuatiliana na kuharibiana biashara.

Kakunda amesema Novemba 13 mwaka jana hadi juzi, Serikali imenunua tani 225,000 za korosho na kwamba kati ya hizo 2,200 zinaendelea kubanguliwa na viwanda vya ndani kwa mkataba maalumu.

Amesema tani 222,800 za korosho zimebaika katika maghala na zina ubora wake.

Chanzo: Mwananchi
kufuatiliana na kuharibia biashara..! Gademiti

Tusubiri kilo mbili tu hapa.
 
Je makampuni hayo sita yaliyojitokeza wakati huu pia hayatachunguzwa?

Maana Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji , Joseph George Kakunda alisema ile kampuni ya Indo Power ya Kenya haikupaswa kuchunguzwa. Msikilize Mh. Waziri kuhusu Indo Power alipojitokeza kufanya biashara :
 
Kwa nini korosho hizo tani 222,000 zisiuzwe hata kwa bei ya hasara ili tupate fedha za kigeni. Tunaingia msimu mwingine baadaye zitakuja kushuka daraja zikikaa kwenye maghala muda mrefu.
 
Serikali imesaini mkataba wa awali na kampuni sita ya kununua korosho kati ya zilizoomba kununua korosho hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 16, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema baada ya Kampuni ya Indo Power ya nchini Kenya kushindwa kununua korosho wameendelea kusaini mikataba ya awali.

“Tumeendelea kusaini mikataba ya awali na kampuni nyingine hadi sasa tumesaini na kampuni sita,” amesema.

Amesema asingependa kuzitaja kampuni hizo kwa sababu ya hali halisi ya biashara ya korosho duniani ambayo kwa sasa watu wanafuatiliana na kuharibiana biashara.

Kakunda amesema Novemba 13 mwaka jana hadi juzi, Serikali imenunua tani 225,000 za korosho na kwamba kati ya hizo 2,200 zinaendelea kubanguliwa na viwanda vya ndani kwa mkataba maalumu.

Amesema tani 222,800 za korosho zimebaika katika maghala na zina ubora wake.

Chanzo: Mwananchi
Wameleta "Indo Power" zingine?

Hii serikali kweli ni sikio la kufa, mtu akipita tu akawatishia nataka kununua korosho yenu yote wanakimbilia TBC kututangazia, pumbavu😅
 
May 16, 2019

“WATANZANIA KULENI MAISHA/ INAONGEZA RUTUBA KUMPA MIMBA MWANAMKE”-WAZIRI KAKUNDA

Source: Millard Ayo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wanahofia kuyataja majina ya kampuni husika maana Wabongo wataingia mitaani kufanya research ili kujua undani wa kampuni hizo kama ni za kweli au FAKE NEWS.

Serikali imesaini mkataba wa awali na kampuni sita ya kununua korosho kati ya zilizoomba kununua korosho hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 16, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema baada ya Kampuni ya Indo Power ya nchini Kenya kushindwa kununua korosho wameendelea kusaini mikataba ya awali.

“Tumeendelea kusaini mikataba ya awali na kampuni nyingine hadi sasa tumesaini na kampuni sita,” amesema.

Amesema asingependa kuzitaja kampuni hizo kwa sababu ya hali halisi ya biashara ya korosho duniani ambayo kwa sasa watu wanafuatiliana na kuharibiana biashara.

Kakunda amesema Novemba 13 mwaka jana hadi juzi, Serikali imenunua tani 225,000 za korosho na kwamba kati ya hizo 2,200 zinaendelea kubanguliwa na viwanda vya ndani kwa mkataba maalumu.

Amesema tani 222,800 za korosho zimebaika katika maghala na zina ubora wake.

Chanzo: Mwananchi
 
yani katika tani laki mbili ni tani elfu mbili tu zimebanguliwa they are not serious
Tena hizo tumejitahidi sana, ubanguaji wa korosho unahitaji kujipanga kwani si kubangua tu, ni pamoja na method ya ubanguaji, kuhakikisha ubora (grading) na pia packing and packaging. Ni process inayobidi ujipange.

Korosho baada ya kuzibangua inabidi ziwe "properly packed" bila hivyo zinaweza ku "stale" ukala hasara.
 
Biashara ni taaluma na inahitaji akili. Huwezi kutengeneza pesa halali bila akili.

Ni rahisi kuwa mwanasiasa kuliko kuwa tajiri. Mtazunguka sana lakini mwisho wa yote mtawarudia wafanyabiashara tajiri maana wana akili na uelewa mkubwa zaidi kuliko wanasiasa.
 
Sababu iliyotolewa kuzuia kuzitaja kampuni zilizoingia mkataba wa manunuzi ni za kimangumashi. Haziingii akilini na inaonyesha kuwa wanaogopa kuzitaja isitokee yale ya kampuni ya Kenya ambayo watu waliiambia serikali kampuni hiyo haina uwezo.

Haya ya serikali kujiingiza katika zao hili inaenda kuliua. Serikali inabidi ijiondoe sasa na kuacha mfumo huria wa kibiashara kuendesha ununuzi wa zao la korosho.

Roho ya koroshow anaeleji Na Pesa zote ataka ziwe zake
 
Hawa hawajifunzi, kwanini wasiwe wanafanya kimya kimya tu, wakimaliza watoe matokeo!
 
Tena hizo tumejitahidi sana, ubanguaji wa korosho unahitaji kujipanga kwani si kubangua tu, ni pamoja na method ya ubanguaji, kuhakikisha ubora (grading) na pia packing and packaging. Ni process inayobidi ujipange.

Korosho baada ya kuzibangua inabidi ziwe "properly packed" bila hivyo zinaweza ku "stale" ukala hasara.
Mkuu hivi kwani inatakiwa korosho zibanguliwe baada ndani muda gani toka kuvunwa ili kulinda ubora.....
 
Back
Top Bottom