Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 115
- 258
1. Mikataba ya uwekezaji iliyosainiwa kati ya Nchi ya Tanzania na mamlaka ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World imesainiwa kuzingatia kifungu cha 2 cha sheria ya Ubia Na. 6 ya mwaka 2023 na kifungu cha 2 cha sheria ya ununuzi wa Umma Na. 5 ya Mwaka 2023.
2. Hapo awali serikali ilikuwa inatumia takriban asilimia 90 ya mapato yaliyokusanywa katika uendeshaji wa maeneo hayo yaliyokodishwa na kubakiwa na asilimia 10 tu ya mapato yote, lakini kupitia hili la mkataba, Serikali itaweza kubaki na asilimia 60 ya mapato yote kutokana na gharama zote za uendeshaji kubakia kwa kampuni ya DP World
3. TRA itakusanya mapato kutoka shilingi Trilioni 7.8 za Mwaka 2021-2022 hadi shilingi Trilioni 26.7 kwa mwaka ifikapo mwaka 2032/33.
4. Kampuni ya DP World kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake Ahmed Bin Sulayem inakwenda kuanza na uwekezaji wa Dola za Marekani milioni 250 sawa na shilingi bilioni 623.75 za kitanzania.