Tanzania yavunja mkataba wa kuiuzia korosho kampuni ya Kenya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,968
Serikali ya Tanzania imesema mkataba wake na kampuni ya Kenya ya kununua korosho tani laki moja umesitishwa.
Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Joseph Kakunda , wakati akihojiwa na gazeti la Tanzania la "The CITIZEN" na kusema kuwa kampuni hiyo ya Indo Power wameshindwa kufuata masharti yaliyokuepo katika mkataba kwa wakati.
Mwezi Januari tarehe 30, serikali ya Tanzania kupitia Cereals na bodi nyingine ambazo ni ndogo zilizosainiwa na kampuni zinazofahamika chini ya kampuni hiyo ambayo ilikuwa kununua tani 100,000 za korosho ambazo zina thamani ya dola milioni 180.2.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Indo Power, Brian Mutembei alisema kuwa wakati wa kusaini mkataba hiyo ilikuwa ilipe moja kwa moja kupitia benki ya Tanzania kwa ajili ya kulipia korosho, na kuongeza kuwa biashara hiyo ingeanza mapema mwezi Februari.
Waziri Kakunda alisema kuwa licha ya kuwa kampuni ilishindwa kumalizia hatua muhimu za kisheria za mkataba huo. Na kuongeza kuwa serikali ilisaini mkataba na viwanda vingine sita ambao wanaweza kununua korosho hizo.

- Serikali yafunguka utata wa kampuni ya kununua korosho

Serikali iliufuta mkataba wake na kampuni ya Indo Power Solutions uliokuwa na thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 400. Mwezi Februari 2019 Serikali iliweka wazi kuwa imeingia mkataba na Kampuni ya kutoka nchini Kenya ya Indo Power Solutions Ltd iliyojinasibu kuwa na uwezo wa kununua Korosho tani 100,000

Serikali kupitia Waziri wa Biashara, Joseph Kakunda imesema kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza sehemu ya makubaliano ya zabuni hiyo na hivyo walisitisha mkataba na kampuni hiyo.

Aidha kampuni iliyoshinda zabuni hiyo ilikuwa na kashfa ya kutokuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo kwa kuwa walikuwa ni kampuni ya udalali na sio kampuni ya ununuzi kama inavyojinasibisha.

1658210737149.png
 
Back
Top Bottom