Kampuni sita zasaini mkataba wa awali kununua korosho nchini Tanzania

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Serikali imesaini mkataba wa awali na kampuni sita ya kununua korosho kati ya zilizoomba kununua korosho hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 16, 2019 Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema baada ya Kampuni ya Indo Power ya nchini Kenya kushindwa kununua korosho wameendelea kusaini mikataba ya awali.

“Tumeendelea kusaini mikataba ya awali na kampuni nyingine hadi sasa tumesaini na kampuni sita,” amesema.

Amesema asingependa kuzitaja kampuni hizo kwa sababu ya hali halisi ya biashara ya korosho duniani ambayo kwa sasa watu wanafuatiliana na kuharibiana biashara.

Kakunda amesema Novemba 13 mwaka jana hadi juzi, Serikali imenunua tani 225,000 za korosho na kwamba kati ya hizo 2,200 zinaendelea kubanguliwa na viwanda vya ndani kwa mkataba maalumu.

Amesema tani 222,800 za korosho zimebaika katika maghala na zina ubora wake.

Chanzo: Mwananchi
 
Hapo kwenye bold pana-suggest kuwa hakuna cha mkataba wala photocopy ya mkataba. Eti watu wanafuatiliana ili kuharibiana biashara; yaani mtu aache kufanya core business yake ili amfuatilie mwenziwe anaetaka kununua korosho za watani zake jiwe?!
 
Sijui mkataba na serikali maana yake nini wakati fedha ni za makampuni hayo na korosho ni za wakulima. Nilidhani ilitosha makampuni haya yakasajiliwa na kulipa kodi zinazostahiki kwa serikali. Unless mkataba unazungumzia kiwango cha bei cha chini ambacho kambuni haitarihusiwa kununua - urasimu mwingine ndio huu.
 
Sababu iliyotolewa kuzuia kuzitaja kampuni zilizoingia mkataba wa manunuzi ni za kimangumashi. Haziingii akilini na inaonyesha kuwa wanaogopa kuzitaja isitokee yale ya kampuni ya Kenya ambayo watu waliiambia serikali kampuni hiyo haina uwezo.

Haya ya serikali kujiingiza katika zao hili inaenda kuliua. Serikali inabidi ijiondoe sasa na kuacha mfumo huria wa kibiashara kuendesha ununuzi wa zao la korosho.
 
Inawezekana wanatuliza mzuka bungeni
Sababu iliyotokewa kuzuia kuzitaja kampuni zilizoingia mkataba wa manunuzi ni za kimangumashi. Haziingii akilini na inaonyesha kuwa wanaogopa kuzitaja isitokee yale ya kampuni ya Kenya ambayo watu waliiambia serikali kampuni hiyo haina uwezo.

Haya ya serikali kujiingiza katika zao hili inaenda kuliua. Serikali inabidi ijiondoe sasa na kuacha mfumo huria wa kibiashara kuendesha ununuzi wa zao la korosho.
 
wamepungukiwa busara pakubwa hawa watu, kwa aibu ilipofikia wangefanya hayo mambo kimyakimya tu
 
Hivi mtu kwenda kununua korosho ya mkulima paka kuwepo na mikataba kweli, kwanini wanaweka urasimu usio na ulazima, thats why hizo kampuni zinaingia mitini.
 
Back
Top Bottom