Kampeni ya kuikataa Vodacom

Kampeni ya kuikataa Vodacom

Siku zingine jitahidi uwe unatumia vyema Akili zako hasa ukija hapa The Home of Great Thinkers tafadhali. Hilo ambalo unadhani limefanywa tu na huo Mtandao ambalo umekuja nalo kwa Mhemko hapa pia huwa linafanya hata na Mitandao mingine mikubwa kama Tigo na Airtel na Mifano yake ipo wazi isipokuwa tatizo Kubwa la Watanzania si Wafuatiliaji wazuri wa mambo, hamjui Kutunza Kumbukumbu na ni Watu wanaopenda Kukurupuka na si ajabu ndiyo maana huko nje tunadharaulika mno na waliotuzidi Akili.

Ungekuwa unajua ya kwamba haya Makampuni yote ya Simu nchini yapo chini ya Serikali na kwa Msaada mkubwa wa Kiudhibiti kutoka TCRA wala usingekuja na huu Uzi wako ulio na Hoja Nyepesi kama siyo ya Kipuuzi. Halafu msisahau ya kwamba kuna hatua zingine zinaweza zikawa zinachukuliwa dhidi ya Mtu kwa ajili ya Usalama wa Taifa letu na hata Sisi Wananchi wake ila bahati mbaya sasa hivi kila Jambo la Muundo huo kama uliomtokea huyo Mtu likitokea haraka sana lawama zenu mnazielekeza katika Mamlaka ila huwa hamtaki Kujua ya upande wa Pili.

Namalizia tu kwa Kukuambia kuwa KUNA UNAYOYAJUA NA YALE USIYOYAJUA na msije Kuona Watu wanakurupuka tu.
Voda ndio vinara, mwaka huu tu kwa taarifa yao wenyewe kwa msukumo wa dola wamedukua simu za wateja wake mara 1000! Shame on them and you too.
 
Sidhani kama ni voda tu, mitandao yote kwa sasa imeunganishwa kwa ajili ya usalama,na ukitoka toka kimya kimya sio mpaka sisi huku tujue,Me binafsi natumia voda na nitaendelea kutumia kama kawaida na daima tusikubali kuongozwa na hisia fulani,fikiria kabla ya kutenda
 
Voda ndio mtandao namba moja Tanzania acheni kudanganyana nyie vijana.
Sheria inawalazimisha mtandao wowote kuingilia mawasiliano ya mteja kama yanatia shaka kiusalama popote mtapokimbilia mtanyooshwa kama mnaleta upumbavu.
 
Kwa ninayo yasikia ni bora kujihami mapema, hivyo nimeachana kabisa na kutumia laini ya Vodacom na nitatumia mitandao mingine nayo ikishindikana basi nitaanza kutumia Email kuwasiliana.

VODACOM sio salama kwa mawasiliaona kabisa labda tuwaachie Makada waendelee kutumia.
Nilisha wakimbia siku nyingi
 
Mi nawaomba kwa umoja kabisa tuanze kampeni hii ya kukataa kutumia vodacom labda akili itawarejea, haiwezekani sisi kama wateja siri zetu zinatolewa pasipo ruhusa ya mteja na kama haitoshi unafungiwa kupiga simu pasipo kutaarifiwa na kubwa zaidi tabia yao ya kupunguza vifurushi. Tuseme sasa inatosha voda wameota mapembe wakati sisi ndo tumewafikisha hapo.
# TuikataeVoda
# HawatufaiVoda
Voda ya nini sasa! Kwenye vifurushi hawafai na kila sekta hawafai. Me shavunja line kwa ghadhabu kitambo sana.
 
Kwa kitendo chenu cha kudukua mawasiliano ya akna Membe mmejitia KITANZI wenyewe . Watu maelfu wanaendelea kuwaacha, hamfai na mko hovyo.Mimi nimeshaweka chip yenu pembeni.
 
Kwa ninayo yasikia ni bora kujihami mapema, hivyo nimeachana kabisa na kutumia laini ya Vodacom na nitatumia mitandao mingine nayo ikishindikana basi nitaanza kutumia Email kuwasiliana.

VODACOM sio salama kwa mawasiliaona kabisa labda tuwaachie Makada waendelee kutumia.
Kwanza hii ni kampuni ya chama kama alivyosema Cyprian Musiba. Hivyo inafanya kazi za chama kwa maelekezo ya Mwenyekiti.
 
Kwa ninayo yasikia ni bora kujihami mapema, hivyo nimeachana kabisa na kutumia laini ya Vodacom na nitatumia mitandao mingine nayo ikishindikana basi nitaanza kutumia Email kuwasiliana.

VODACOM sio salama kwa mawasiliaona kabisa labda tuwaachie Makada waendelee kutumia.
Mpaka juzi nineshaitupa laini mkr wangu pia nimemshawishi naye kaitupa, hawataona jata senti moja kutumika kupitia laini zangu kule vijijini najipanga kuwashawishi wazazi.na ndugu zangu nao wazitupilie mbali.
 
Umejuaje kama ni voda?
Kwa kitendo chenu cha kudukua mawasiliano ya akna Membe mmejitia KITANZI wenyewe . Watu maelfu wanaendelea kuwaacha, hamfai na mko hovyo.Mimi nimeshaweka chip yenu pembeni.
 
Watanzania wanashangaza sana.

Vodacom inamilikiwa na Ccm kama mwanahisa, kwa hali yoyote, Vodacom haiwezi kukubali mmiliki wake ahenyeshwe wakati wanaweza kutoa taarifa kwa chama kuhusu mambo mbalimbali yanayofanyika kupitia mtandao wa vodacom yanayokidhuru chama.

Binafsi nawapongeza vodacom kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa chama tawala.

Wale wenye nongwa, kuna mitandao mingine wala hamjalazimishwa kubaki vodacom, nendeni mjiunge na mitandao ya mabeberu
 
Back
Top Bottom