Halafu unakumbuka mipira iliyokuwa inatengenezwa na manailoni halafu unaifuma na kamba? Hii ndo ilikuwa alternative yetu ya magozi kwa vile yalikuwa adimu sana. Mdingi akienda kiwanja akikuletea gozi kama zawadi basi mwenyewe unataaamba...Lol.
Mipira ya manailoni tena nisahau ndugu yangu?
Mpira wa Gozi, huko unaenda mbaaaali mno. Kitenesi tu ishu!
Kuna vile vi gofu vile, vya Tiger Woods vile. Ukikipata kile dili. Ndio kinakuwa cha ndimu mpaka kipotee!
Tulikuwa tunaambiwa kigofu ndani kimejaa raba bendi. Me and my brother tukawa tunatamani tukipasue tupate raba bendi (mwanangu, raba bendi nazo iiiiiishuu!) Sasa tulikuwa tunapenda mpira kupindukia. Tukaona tukipasua kigofu, hatuna cha ndimu. Tukibaki nacho kigofu, we'll never find out ndani kuna nini. Big dilemma!
We never cracked the golf ball or the puzzle!
angalau wenzetu mlikuwa na vitu vya kuchezea.. wenzenu kijijini.. mkono mmoja umeshika kaputula isidondoke huku kwapani umeweka daftari za "Mazoezi"; mkono mwingine una bonge la kijiti na ringi la baiskeli unakimbizana nalo kuwahi shule... uzuri wake jinsi ulivyokuwa unakatisha nayo kona mtu akikuambia uendeshe pikipiki hutaki!!
hapo sijakuambia kuhusu manati inayoning'inia shingoni for "after school activity"...
Mwanakijiji, naamini kuwa katika umri huo, ndio nilikuwa na raha kuliko wakati wote. Hakuna wajibu (responsibilities) wowote, hakuna kujali unaonekanaje au una hatari ya kuumia na wazazi wetu walitusupport. Walituruhusu tucheze vita vya makungu au madongo bila hofu. Siku hizi, kila kitu lazima kiwe kimethibitishwa na chombo flani cha dola. Hivi ni nani aliyegundua mchezo wa, ashakum, mama na baba?
... Walituruhusu tucheze vita vya makungu au madongo bila hofu.
On a serious note though, speaking of vita vya makungu, hivi kwa nini sisi ndio tuna chakula mpaka tunachezea lakini bado tunakufa njaa?
Kiwanja toka lini ukakuta mpera au mpapai umejiotea otea barabarani!
Nani atakupa tunda la bure Marekani? Is it the land of milk and honey kweli?
...this is what I figured out.. nikienda Kroger au Meijers..... this is the land of milk and honey.. at least ukienda kwenye grocery stores...
Je ukipewa nafasi ya kuurudia umri huo utakubali?
Zaidi ya vitabu vya upelelezi na mapenzi... kuna kulikuwa na vitabu kama Machimbo ya Mfalme Suleiman.. akina Umplomagasi na msemo wake wa Pigo moja tu, pigo lenye nguvu pigo takatifu
Zaidi ya vitabu vya upelelezi na mapenzi... kuna kulikuwa na vitabu kama Machimbo ya Mfalme Suleiman.. akina Umplomagasi na msemo wake wa Pigo moja tu, pigo lenye nguvu pigo takatifu