Kamlete - akibisha...

Yaani ni kweli mimi nilikuwa na mawazo hayo hayo. Nina imani kabisa alikuwa anatuongopea, kama kaandika yeye vile, kumbe kazi yake yeye ilikuwa ni kubadilisha lugha tu, stori imekuwa ya kwake...
Hehehehe...Kwikwikwi

Hizi ni accusations nzito kuzitoa kwa "imani" tu.Toa jina la kazi yake na kitabu alichokopi.

Thematic resemblance ni kitu cha kawaida katika utunzi (ama sivyo rappers. Robert Ludlum na Frederick Forsyth wasingekuwa na kipya cha kusema kama unaongelea plagiarism tuonyeshe ushahidi.
 
Hapo sasa hao hao wanao kufa kwa ajili ya midege mibovu utaona wanamlinda kwa vile na wao walisha pata 10% yao kwa hiyo mm naona bora ziendelee kuwaua wao wenyewe wao ndo wanao zipanda.
Hapo NO COMENT watajiwajibisha wao wenyewe kwa kulipukiwa tu.
 
nasikia visa vyake vingi vilikuwa vinatokana na James Hadley Chase..

Nope!
nimesoma 100% ya musiba na 70% ya chase, hakuna uelekeo kabisa.
Labda hao waingereza.
Lakini plot zilikaa kinyerere nyerere, wakati huo tuliamini kuwa yeye ni usalama wa taifa.
Huyu Musiba sio huyu wa "Biashara ya nje"?
nimekumbuka yule Nyota ya jaha, na vitabu fulani vya historia ya Zanzibar kabla ya mapinduzi, navitafuta sana, nimevisahau majina lakini stories zake ziko akilini kabisa. Those were good books.
Kwa kweli siwezi kusoma 'novels' za siku hizi, labda nimepitwa na wakati au vipi.
Lakini najitahidi sana kurecomend vitabu vya zamani vya tanzania na kenya kwa watu na wanafurahi sana.
 
bwana Ibambasi kwa nini hiki kitabu cha Rosa Mystica kilipigwa marufuku?.kilikuwa na ishu gani mbaya? by the way mimi nilikisoma pale Tanganyika library, Dar.

Ilidaiwa kwamba theme ya kitabu ilikuwa ni udhalilishaji,kwa mfano ndani ya kitabu msichana huyo alikuwa akifanya mapenzi (ashakum si matusi) na Bwana Maendeleo,mara Mkuu wa Chuo cha Kigurunyembe na mambo mengine...hicho kilikuwa kipindi cha Mzee wetu aliyetangulia mbele ya haki na nadhani unaelewa censorship iliyokuwepo.Kama ulikisoma basi ni kwa vile ilitokea ukakisoma.Mi nilikuwa from III wakati nakisoma mara akatokea Mwalimu akanikuta nacho akataka kuninyang'anya akidai nimweleze nilikokitoa,baadaye ndo akanifafanulia ni kwa nini hakitakiwi kusomwa...
 
Yote tisa, kumi ni "mfululizo wa vijitabu vya Ujinga wa Mwafrika".... inaonekana umbumbu wetu haukuanza jana...
 
Hamuwezi kuwa na kumbukumbu nzuri kama hamkumbuki "Usiku wa Balaa" na yule "Kibibi Gula" na "Mzee Ole".... sijui kama watu wanakumbuka hadithi kama "Dimbwi la Damu" na kisa cha "Helen Jeuri??" Mtasema nini tukiwakumbusha visa vya Lisabeti na Bulicheka katika nchi ya Wagagagigikoko? Hivi hata mnakumbuka mambo ya "Paulo usije kucheza na sisi" au mambo ya "Makari Hodari, katika Safari"....?

Yooote mmeyataja, sijasikia simulizi za Adili na Nduguze, pia kulikuwa na kitabu- Ikibidi kufa nife, pamoja na hadithi za mama na mwana- hadithi ya kijana Akajasembamba
 
Yooote mmeyataja, sijasikia simulizi za Adili na Nduguze, pia kulikuwa na kitabu- Ikibidi kufa nife, pamoja na hadithi za mama na mwana- hadithi ya kijana Akajasembamba

Yaani Bi tarabushi umenikumbusha zamani.Hakuna kitu kilichokua kinaninyima usingizi Usiku kama hadithi ya Akajase Mbamba.Kwa kweli weekend kwangu ilikua ni ni kitu cha thamani hasa pale inapofika saa nane Mama Debora Mwenda anapoanza kutusomea hadithi zile.Ishu ilikua wakati wa kulala ukikumbuka majini kwenye akajase basi usingizi kwisha wote.
 
Whaaaat... mtasema nini tukiwaambbia kuhusu "Ua Jekundu" hasa lile jitu liliposema "Vema Kijana Vema Kijana"?
 
Jamani kumbe watu tumetoka mbali nchi ya wagagagikoko hasa tukicheza gololi au ndude vifuniko vya ndovu halafu tulikuwa hatuchezi na Paulo kwa vile ana mikono michafu....kwa kumalizia nakumbuka kitabu cha Mine Boy...Xuma...sijui kama kumbukumbu yaku sahihi lakini kuna part ya kitabu ....."white sands made by black people"...ina fanana na machimbo yetu ya madini yanawanufaisha kina James Sinclair na share holders wa TRE.

Tusimsahau Shaaban Robert na nchi ya Kusadikika na hivi nani aliandika KIU?
 
duh, MAOKA imenichekesha mpaka machozi, thanks Mwkjj!
Is it possible kupata copy ya hivi vitabu sasa hivi, maana wengine hatukuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu. Mlo wenyewe ulikuwa ishu!
 
umenikumbusha pia marehemu shaaban robert, hivi na yeye alikuwa hatafsiri kazi za watu yule?

maana ukisoma vitabu vyake utakubali kama yule ni nguli
 
Tarehe 6 Disemba mwaka 2007 Helikopta ya Jeshi la Wananchi ilianguka kwenye ziwa Natron huku na kujeruhi watu kadhaa wakiwemo wale ambao walidaiwa kuwa ni "Wageni wa serikali" ambao walikuwa na vifaa vya kupigia picha za filamu katika ziwa hilo na taarifa za awali zilisema pia kupiga picha mlima wa Oldonyo Lengai.

Na jana Helikopta nyingine imeanguka mkoani Arusha na kuua watu wote sita waliokuwemo kwenye chopa hiyo ambayo ilikuwa inatoka Arusha kuelekea Dodoma.

Ndege zote hizo mbili zinaunganishwa na yule dalali maarufu Bw. Shaileth Pragji Vithlani ambaye ndiye aliyeshughulikia mchakato wa kuzipata ndege hizo na kuwaunganisha JWTZ huku yeye mwenyewe akiwa mabilioni ya shilingi mfukoni kama gharama yake ya udalali. Bw. Vithlani ndiye dalali huyo huyo aliyeshiriki katika ununuzi wa rada ambako inadaiwa kuwa alikatiwa karibu Shs. Bilioni 21 kama malipo yake ya udalali wa kazi yake.

vithlani2.JPG

Kwa vile sasa inaonekana helikopta zake hizo zote zina matatizo, jambo la kwanza ambalo tunapenda kutoa wito.

a. Kusitisha kuruka kwa helikopta zote za Jeshi hadi uchunguzi huru wa kitaalamu wa airworthness ufanywe na kuona kama zinafaa kuendelea na huduma.

b. Endapo helikopta hizo zilizoanguka na zile zilizopo bado zilionekana zina defects zozote za msingi basi Bw. Vithlani pia afunguliwe mashtaka ya manslaughter au criminal negligence kutokana na kuchangia vifo vya watanzania hao na pia kulisababisha Taifa hasara.

c. Maafisa waliohusika na ununuzi wa helikopta hizi wachukuliwe hatua mara moja ikiwemo kufunguliwa mashtaka ya kijeshi.

d. Serikali imtafute huyo dalali kabla na yeye hajafa na kuzikwa huko huko Uswisi siku chache zijazo na mwili wake kuteketezwa kwa moto kwa desturi za kwao!!

Vinginevyo kama kina Rashid Othman wanauwezo wa kukifanya kile Waisrael walikifanya baada ya mauaji ya Munich ya 1972 ambapo maafisa wake wa Usalama waliwafanyizia wale wote waliohusika na mauaji hayo bila kujali nchi walizopo. Ni wakati wa kutuma kikosi chetu (kama hakipo kianzishwe) cha kuwashughulikia watu kama hawa ambao wanafanya uhalifu Tanzania halafu wanakimbilia nje ya nchi.

Tuwatume waende "wakamlete.. akibisha... "


Mkono mrefu wa sirikali si kwa mambo kama haya .Mkono mrefu unatumika kama kule Pemba kwa wale wazee wenyewe wanaotaka haki sawa lakini si kwa wanao kula nao .
 
jamani kuna novel moja inaitwa "BURIANI",ni nani aliisoma hii na je iliandikwa na nani?

GLN, Buriani iliandikwa na bwana mmoja kutoka Tabora (samahani jina limenitoka na inanibother kutokumkumbuka). Alikuwa mwandishi mzuri sana na aliandika kitabu kingine kiitwacho "Simu ya Kifo"
 
Agoro Anduru umenikumbusha nadhani ndiyo alikuwa na ile "Rosa Mystica" siyo?
Mzee MwanaKijiji,
Kwanza nai-miss sana ile picha yako ya zamani. Ilikuwa Mswano sana. Ukija kwenye Agoro Anduru kwa ukweli sikumbuki aliandika kitabu gani ila hicho cha ROSA MYSTICA na GAMBA LA NYOKA kwa kumbukumbu zangu za ki-ufundi mchundo zinaniambia kuwa aliandika Ezekiel Kezilahabi- Professor kutoka Ukerewe kweli ya Ziwa Victoria. Katika hizo ongeza na mtani wangu Nico ya Mbajo na ile mimama minene na wowowo kubwa aliyokuwa akichora ndani ya vitabu vyake. Pia tusimsahau HOMEBOY wangu wa kutoka pale Igalula Railway Station na vitabu vyake kama Simu ya kifo na Pili Pilipili akienda na jina Hassan Katalambula.
 
Sijasoma post zote. Mhhh, hii ya Paulo usije cheza na sisi na Wagagagigigoko, kahhh!!
Nakumbuka na ile Mr. Kapufi is a veterinary officer, Mbishi and the Goat, Umsuke umsuke, twahelela .... Hadithi za Malimwengu (alifu lela u lela?), Huyu ni Juma, juma ana dada, dada yake Juma ni Rosa, Rosa ana Kiu, Kunywa maziwa Rosa ..... Mzee Mwaura na Joka lake (Kenya). Vitabu vya Erotic kama yule mwandishi Mkenya alieandika My Dear Bottle. Na cha Tz kinaeleza msichana ambaye mama alikuwa Changu Doa na yeye akawa anamendewa na Mzee Magege ambaye baada ya kupata mimba wakaenda kuitowa ... kuna wimbo "Hilo kapu hata taka laingiza ...ohhh kapu hilo ." Duu, kweli tumetoka mbali. Na ilikuwa ukifika secondary basi unaanza kusoma James Hadley Chase......
 
Katika wachoraji umenikumbusha yule Ndunguru.. alikuwaga Sani. Na kwenye makala siwezi kumsahau "Kaka Miye"...
 
kuna sani moja ilikuwa na stori ya lilian seuya, mwanadada aliyemkataa jamaa kwenye altare baada ya kutonywa na dada fulani kwamba jamaa alikuwa mpenzi wake na walishapanga kuoana na kila kitu, kutokana na guilty conscious, lilian akamtosa jamaa mbele ya altare.
kutokana na uchungu alioupata jamaa akaamua kula njama na rafiki yake fulani ambaye lilian alikuwa hamjui ili walipize kisasi kwa lilian, wakapanga yule rafiki wa jamii amtongoze lilian kwa udi na uvumba , kweli yule msela akafanikiwa kumpata lilian na wakapanga ndoa,kufika kwenye Altare padri anauliza kama msela yuko tayari kumfanya lilian kuwa mke, jamaa akatosa.kwa hiyo lilian naye akafanyiwa yale yale aliyomfanyia rafiki wa huyu msela. ila baade kitambo huyu msela alipokuja kujua kwa nini lilian alimtosa rafikiye ikawa imeshakuwa too late tena
msela akawa hawezi tena kumconvice Lilian..... Hayo ni mambo ya Sani enzi hizoooo
 
angalau wenzetu mlikuwa na vitu vya kuchezea.. wenzenu kijijini.. mkono mmoja umeshika kaputula isidondoke huku kwapani umeweka daftari za "Mazoezi"; mkono mwingine una bonge la kijiti na ringi la baiskeli unakimbizana nalo kuwahi shule... uzuri wake jinsi ulivyokuwa unakatisha nayo kona mtu akikuambia uendeshe pikipiki hutaki!!

hapo sijakuambia kuhusu manati inayoning'inia shingoni for "after school activity"...

Mwana Kijiji, (Usisome kama unakichefuchefu au wala)
umenikumbusha miaka hiyo nilipotoka Dar na kwenda Kijijini. Kufika huko nikaona binamu zangu wakijisaidia na nikashangaa hakuwa kajiandaa kwa toilet paper yoyote walau majani ya miti laini. Baada ya kumaliza nikamuona anakaa chini na kuanza kucheza Sikinde (ngoma ya ukae). Nikamuuliza sasa unafanya nini hapo? Akajibu kuwa anachamba. Sikuamini na ilibidi nihakikishe. Nilijaribia na nikashindwa na hadi leo nawanyenyulia mikono wenye uwezo huu. MMK kweli umenirudisha mbali saaana na kunikumbusha marehemu wengi saana ukichanganya wazazi wangu. Nakumbuka daftari langu la kwanza jarada lililiwa na ndama, hee ilikuwa kasheshe maana likijaa sintaweza badilisha. Nilipata ujanja wa kuweka cover la gazeti (nalo kupata ni shida) na nikabadilishiwa....... Juu ya magari kule kwetu walikuwa wakitengeneza ya mabua ya mahindi. Yalikuwa mazuri saana hasa LANDROVER na yale mabasi ya LEYLAND (SABENA, Tanganyika Buss,.....).
 
Kati ya magari yote ya kuchezea hakuna yaliyokuwa yanapendeza kama yale ya waya halafu yamezungushiwa tule tuwaya twa rangi rangi... mzee hadi yananesa halafu kijiti kimepita katikati.. halafu ukitaka kuzinguka ni vile vikaragosi vinavyoendesha basikeli...
 
Back
Top Bottom