Kamishna Jenerali wa Kudhibiti dawa za kulevya nchini Ndugu Aretas Lyimo namwona kama kiongozi serious na anayeweza kulisaidia Taifa; hongera

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Huyu Bwana anahitaji pongezi kubwa sana. Anapambana na dawa za kulevya proffesionally siyo kisiasa kama watangulizi wake.

Amebiresha mambo mengi kwenye taasisi hii kwa muda mfupi. Ameondoa Tambo za vyombo vya habari, amepiga marufuku kuchafua watu kisa siasa na sasa anakamata na kuchunguza akimaliza anakuja kwenye jamii mtuhumiwa akielekea Mahakamani.

Kwa umakini alionao na endapo atapewa uhuru wakupambana na mapapa naamini atawamaliza madawa za kulevya zitaisha nchini. Changamoto aliyonayo kubwa ni ushirikiano wake na polisi ambapo polisi wanavyoratibu kesi ya dawa za kulevya naamini wanakosa utaalamu na wanakimbilia sana kwenye vyombo vya habari kabla hata yakufanya uchunguzi.

Akiweza kudhibiti wakuu wa polisi kutangaza issue za dawa za kulevya hadi majalada yakamilike itamsaidia sana kudhibiti wahalifu kutoroka. Vinginevyo nimtakie afya njema na zaidi amtegemee Mungu katika majukumu haya magumu aliyopewa.
 
Back
Top Bottom