Kamishna wa Kudhibiti dawa za Kulevya: Bangi ya Tanzania haifai kwenye Masoko ya Kimataifa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,100
49,795
Swali.

Hivi wenzangu mnamuelewa huyu Jamaa?

Yaani bangi ingekuwa haifai watu wangekuwa wanalima na kuisha Kwa Wingi kwenye black market?

Waache ujinga walete sheria ya Kilimo rasmi Cha Bangi na Mirungi Ili Mashamba yawe monitored badala ya kuongea pumba hapa 😆😆.

---
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Nchi zilizohalalisha bangi zina utaratibu thabiti ikiwemo kulima bangi hizo kwenye maeneo maalum na kuna kiwango kinachotakiwa ambapo amesema bangi ya Tanzania inayolimwa kwenye mashamba yasiyo rasmi kiholela haifai na haiwezi kukubalika kwenye masoko halali ya nje ya Nchi.

Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam baada ya Mwandishi wa @AyoTV_ kumuuliza mtazamo wake kuhusu maoni ya Watu wakiwemo Wabunge kwamba bangi ianze kuuzwa nje ya Nchi ili iongeze pato la Taifa badala ya kuwa inateketezwa.

“Nchi zilizohalalisha bangi wana bangi yao inalimwa kwenye green house inatakiwa iwe na kiwango fulani, tusichukulie tu jambo la rahisi tu kwamba tutachukua tuweke kwenye kiroba kwenda kuwauzuia nje mfano Kenya, Kenya wenyewe bangi haijahalalishwa”

“Hii bangi yetu haifai kwenye kwenye masoko halali hata huko nje, kule wenzetu wametengeneza sehemu maalum za kuuza, kiwango cha kununua na hata umri wa Mtu wa kumuuzia, ukisema uruhusu ya kwetu haiwezi kukubalika, mfano halisi ni miwa, hivi miwa yote inaruhusiwa kutengenezea sukari?, jibu ni hapana, na bangi pia ipo hivyo sio kila bangi inafaa kwa matumizi halali”

Chanzo: Millard Ayo

Bangi ihalalishwe, Sheria zinazotumika kuhusu Bangi. Ziende kudhibiti Ushoga

Kassim Majaliwa: Bangi ya 'Cha Arusha' pamoja na 'Skanka' inafanya watumiaji kuwa vichaa

Serikali iruhusu kilimo cha bangi na ipunguze masharti ya uingizaji wa fedha nchini ili kukabili uhaba wa dola
 
Swali.

Hivi wenzangu mnamuelewa huyu Jamaa?

Yaani bangi ingekuwa haifai watu wangekuwa wanalima na kuisha Kwa Wingi kwenye black market?

Waache ujinga walete sheria ya Kilimo rasmi Cha Bangi na Mirungi Ili Mashamba yawe monitored badala ya kuongea pumba hapa 😆😆.

---
Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dkt. Peter Mfisi amesema Nchi zilizohalalisha bangi zina utaratibu thabiti ikiwemo kulima bangi hizo kwenye maeneo maalum na kuna kiwango kinachotakiwa ambapo amesema bangi ya Tanzania inayolimwa kwenye mashamba yasiyo rasmi kiholela haifai na haiwezi kukubalika kwenye masoko halali ya nje ya Nchi.

Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam baada ya Mwandishi wa @AyoTV_ kumuuliza mtazamo wake kuhusu maoni ya Watu wakiwemo Wabunge kwamba bangi ianze kuuzwa nje ya Nchi ili iongeze pato la Taifa badala ya kuwa inateketezwa.

“Nchi zilizohalalisha bangi wana bangi yao inalimwa kwenye green house inatakiwa iwe na kiwango fulani, tusichukulie tu jambo la rahisi tu kwamba tutachukua tuweke kwenye kiroba kwenda kuwauzuia nje mfano Kenya, Kenya wenyewe bangi haijahalalishwa”

“Hii bangi yetu haifai kwenye kwenye masoko halali hata huko nje, kule wenzetu wametengeneza sehemu maalum za kuuza, kiwango cha kununua na hata umri wa Mtu wa kumuuzia, ukisema uruhusu ya kwetu haiwezi kukubalika, mfano halisi ni miwa, hivi miwa yote inaruhusiwa kutengenezea sukari?, jibu ni hapana, na bangi pia ipo hivyo sio kila bangi inafaa kwa matumizi halali”

Chanzo: Millard Ayo
Na Wamejuaje kama Haina ubora wakati wakiichukuaga wanaichoma au wameshaenda kuuza na kuipima ubora
 
hana jipya anabwabwaja tu wanakuja watu toka us ukimpa cha arusha anasizi tena anakuambia hii kitu bomba sana iko soomth tatizo kubwa ni bhange ambazo hazijakomaa zinaletwa town kwa biashara ila ukapata kitu from orkokolo ukila kete moja ukatafute sehemu uskilizie stimu
 
Back
Top Bottom