Kamishna Jenerali Aretas James Lyimo atangaza vita mpya dhidi ya dawa za kulevya nchini. Kuanza na vijiwe vyote

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
KAMISHINA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Aretas James Lyimo ametaja malengo yake ambayo ameingia nayo ili kuhakikisha mamlaka hiyo inadhibiti kabisa biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.
msg167566-99242.jpg
Ameyasema hayo leo Aprili Mosi, 2023 mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambapo mamlaka hiyo inashiriki kikamilifu katika mbio za mwenge huku akiweka wazi mipango yake ya kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo.

"Mimi kama Kamishna mpya wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, malengo yangu ambayo nimeingia nayo ni kuhakikisha tunadhibiti kabisa usambaaji wa dawa za kulevya, lakini pia kuhakikisha kwamba tudhibiti na kupambana na uingizaji wa dawa za kulevya nchini.

"Kwa hiyo nitoe wito kwa watumiaji wa dawa za kulevya kuacha wenyewe kutumia dawa za kulevya, lakini pia kwa wale wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya kuacha kabisa hiyo biashara ya dawa za kulevya, kwani kuanzia sasa tunafanya operesheni kabambe nchi nzima, lakini tutahakikisha vijiwe vyote vya wauzaji, na watumiaji wa dawa za kulevya tunavisambaratisha,"amefafanua Kamishna Jenerali Lyimo.

Pia amefafanua kuwa, "Na tutafanya opereheni kabambe nchi nzima na tutakamata wote wanaofanya biashara ya dawa za kulevya. Lakini pia tutafanya operesheni kila kijiji, mikoa yote kuhakikisha kwamba wale wote ambao wanalima bangi na mirungi tutahakikisha kwamba tunawakamata na kuteketeza mashamba yao, kwa hiyo nitoe wito kwa jamii nzima, mashirika ya dini, na Serikali kwa ujumla kuhakikisha kwamba tunatoa taarifa kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ili kuweza kufanikisha operesheni mbalimbali tutakazofanya nchini kudhibiti dawa za kulevya.

"Kwa hiyo, niiombe jamii na nitoe wito kwao kutambua kuwa,ushirikiano wao utaiwezesha hii nchi ikuwa salama bila ya dawa za kulevya, kwani dawa za kulevya zina madhara makubwa sana, yanapoteza nguvu kazi ya taifa. Kwa hiyo tukisaidiana wote kama jamii, tutahakikisha kwamba tunadhibiti dawa za kulevya nchini.

"Lakini cha kwanza tutakachoanza nacho ni kudhibiti vijiwe vyote vya dawa za kulevya nchini,Lengo tunapunguza uhitaji wa dawa za kulevya, lakini pia tutapambana sambamba na wale wote waletaji wa dawa za kulevya kutoka nje ya nchi, nje ya mipaka na ndani ya Tanzania, lakini pia tutaimarisha ushirikiano wa Tanzania, kikada pamoja na Kimataifa kuhakikisha kwamba tunadhibiti dawa za kulevya nchini,"amefafanua Kamishna Jenerali Lyimo.

Mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2023 katika uwanja wa CCM Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara leo Aprili Mosi , 2023 zimezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Aidha,Kamishana Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Aretas James Lyimo amesema, ushiriki wao katika mbio hizo una umuhimu mkubwa.

"Tupo hapa Mtwara katika tukio hili la uwashaji wa Mwenge, kwa sababu Mwenge unatembea nchi nzima kwa ajili ya kukemea maovu, kuhakikisha kwamba, maovu yanaondoka kwenye jamii nchini, na sisi kama Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya,dawa za kulevya ni sehemu moja wapo ya maovu ambayo yanakemewa na Mwenge.

"Kwa hiyo sisi ni sehemu ya Mwenge, na tuko hapa kwa ajili ya kuitaka jamii kuhakikisha inaachana na matumzi ya dawa za kulevya, inaachana na biashara ya dawa za kulevya,na mwisho wa siku katika mikakati yetu ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama bila dawa za kulevya.

"Na kuhakikisha Tanzania nzima, watu wote na wananchi wote tutahakikisha kwamba hakuna matumizi ya dawa za kulevya. Na ndiyo dira na ndiyo lengo letu na ndiyo mapambano yetu dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya,"amefafanua Kamishna Jenerali huyo.
 
Je ana kikosi chenye maadili na ataweza kuvunja ngome ya vibopa vya ngada!? Aanze kwa kukusanya mateja wote kwenye vituo vya daladala hasa pale Ilala.

Kisha aongee na yule walisemaga alikamatwa China sijui mpaka baba yake akaenda kumtoa. Binadamu wana maneno sana.
 
Wale vijana wa Europe,kama wanataka madawa ya kulevya kulevya,wapelekee. Kwa sababu usipowapelekea,watanunua madawa ya kulevya kwa mwendo wa kuruka.
Nasikia Magufuli alipotangazwa kuwa rais,vijana walifurahi sana,wakasema ,Bora Kikwete ameondoka na hiana zake,sasa tutapata tena.
Kwa sababu alizuia upelekaji wa madawa ya kulevya Europe.
Ukitaka kudukuliwa moyo ubishane na hao Drug Lords. Magufuli alikuwa na sera ya "Tanzania Kwanza". Alikuwa hajali Ulaya wanafanya nini.
 
Wale vijana wa Europe,kama wanataka madawa ya kulevya kulevya,wapelekee. Kwa sababu usipowapelekea,watanunua madawa ya kulevya kwa mwendo wa kuruka.
Nasikia Magufuli alipotangazwa kuwa raise,vijana walifurahi sana,wakasema ,Bora Kikwete ameondoka na hiana zake,sasa tutapata tena.
Kwa sababu alizuia upelekaji wa madawa ya kulevya Europe.
Kodi imekaa kinyumenyume au kwangu tuu.
 
Back
Top Bottom