'Kamdomo kamponza Ally Kamwe..' Polisi Tabora yathibitisha kumshikilia

'Kamdomo kamponza Ally Kamwe..' Polisi Tabora yathibitisha kumshikilia

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
9,764
Reaction score
20,456
Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe akamatwa usiku wa manane huko Tabora.

Chanzo cha Kukamatwa kwake ni kutoa Lugha chafu kwa viongozi wa Mkoa.

Ameshikiliwa kwa Mahojiano Maalum.

RPC Tabora amethibitisha

“Nathibitisha tunamshikilia Msemaji wa Yanga, Ali kamwe, tunamshutumu kwa kutoa kauli mbaya dhidi ya viongozi wa Serikali, tunaendelea na mahijiano nae na tutatoa taarifa,” Richard Abwao - Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora.


==================

Polisi Mkoani Tabora imethibitisha kumshikilia Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe.

Kamanda wa Polisi Tabora Richard Abwao amethibitisha kushikiliwa kwa Ali Kamwe na Polisi huku tuhuma zake zikitajwa ni kutoa lugha chafu kwa viongozi wa Serikali.

Kamwe alikuwa na timu yake ya Yanga Tabora kwa mchezo dhidi ya Tabora United ambayo ilimalizika jana kwa Yanga kushinda mabao 3-0.

Kabla ya Mchezo Kamwe anatajwa kuzozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Paul Matiko Chacha katika kile kilichotajwa kuwa alikuwa akijibu alichosema RC huyo kuwa Yanga wamekuja na kiherehere mkoani mwake.

Tabora.jpg

Ali Kamwe kushoto akiwa na RC Tabora​
 
Afisa habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe Akamatwa usiku wa manane huko Tabora.

Chanzo cha Kukamatwa kwake ni kutoa Lugha chafu kwa viongozi wa Mkoa.

Ameshikiriwa kwa Mahojiano Maalum.

RPC Tabora amethibitisha

“Nathibitisha tunamshikilia msemaji wa Yanga Ali kamwe, tunamshutumu kwa kutoa kauli mbaya dhidi ya viongozi wa Serikali, tunaendelea na mahijiano nae na tutatoa taarifa” Richard Abwao - Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora

View attachment 3291826
Ali Kamwe kushoto akiwa na RC Tabora​
Kama mkuu wa mkoa ameamua kuwa shabiki wa soka then avumilie changamoto zake otherwise abakie na majukumu yake ya kiserikali
 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao amethibitisha kukamatwa kwa afisa habari wa Yanga Ally Shabani Kamwe baada ya mchezo wa jana dhidi ya Tabora United kumalizika kwa sababu zinazoelezwa kuwa ametoa lugha chafu kwa viongozi wa serikali kabla ya mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kushinda goli 3-0

Abwao amesema bado Kamwe yuko kizuizini akiendelea na mahojiano juu ya tuhuma hizo ambapo taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
 
😂😂😂😂 wapuuzi tu .... Yaan mkuu wa mkoa atoe shutuma dhidi ya Yanga afu Alli Kamwe amjibu kwa kauli laini?. Wanaopoteza muda wao hao polisi... Wanashindwa kutatua mambo ya msingi kwa jamii anajiingiza kwenye mambo ya mpira usiowahusu?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom