pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 11,644
- 14,810
Habari za wakati huu mashabiki na wapenzi wa soka,
Leo tumshauri ndugu yetu ambaye ni msemaji wa wananchi kwa sasa yaani DAR ES SALAM YOUNG AFRICAN.
Msemaji wa YANGA kwa siku za hivi karibuni amekuwa anafanya vitu vya kitoto sana, Kwanza anajibu kila hoja kutoka kwa wapinzani labda anadhani kufanya hivyo ndio usemaji wenyewe ila ukizoea kujibu hoja siku ukikaa kimya juu ya jambo Fulani watu wataona kuna ukweli.
Yaani hata ukiangalia post zake anaweza akaweka emoji 20 za kucheka tu bila caption. Lakini jingine ni kwamba siku wakati YANGA wanazindua jezi aliacha kufanya promotion ya jezi za yanga akadandia kuvuja kwa jezi simba bila kujua kwamba ule ulikuwa mtego matokeo yake jezi zimedoda na promotion imemshinda. Lakini ukiachana na yote matukio haya yalitosha kumuondoa Ali Kamwe kwenye usemaji:-
1.Tukio la Ali Kamwe na Juma Mgunda alimtukana na kumkejeli kwa kusema akiwekewa Mgunda na andazi yeye anachagua andazi licha ya kuomba msamaha baadae lakini hii haikuwa kauli nzuri kutoka kwake na alikuja kuirudia kwa kumuita mama yake Feisal andazi wakati wana mgogoro naYANGA.
2.Hivi karibuni wakati YANGA ilipoenda kucheza mechi ya NBC Premier League mkoani Tabora alimtukana na kumkejeli mkuu wa mkoa na akawekwa ndani ila baadae alitoka kwa dhamana msemaji unatakiwa uangalie kinachotoka kinywani mwako.
3.Hii ndio ilinishangaza sana msimu uliopita YANGA walichagua kutumia uwanja wa chamazi complex ila ya kaibuka madai ya kwamba wachezaji wa YANGA wanapigwa sindano baada ya kuonekana bomba za sindano chumba walichokuwa wanatumia baadae wakahamia KMC Complex, ila Ali Kamwe alitoa kauli za dharau kwa uwanja huo akidai viti vyake vilikuwa vidogo na pitch mbovu na hauna hadhi ya kutumiwa na team kama YANGA wakati huo ambayo haina hata kiwanja cha mazoezi .
4.Ali Kamwe kwenye Sakata la dana dana za derby alikataa kuhojiwa na CLOUDS FM na aliwakataza pia kulitaja jina la YANGA kwenye uchambuzi wao hata mechi hyo ilipopangiwa tarehe nyingine mpaka leo CLOUDS anapaona kituo cha polisi .
5.Mkataba wa kagoma na YANGA yaani hapa ndio walifanaya utoto wa hali ya juu na wenzake kina abdul aziz Pamoja na privadinyo walipoonekana wameshika nakala za mkataba unaodaiwa ulikuwa wa YANGA na Kagoma wakiwa na mwanasheria wao feki wakati wanajua taratibu haziruhusu walichofanya.
6.Ali Kamwe huyu huyu wakati YANGA wanaenda kucheza na Al hilal ya ibenge alisema wanaenda kuwapiga kama ngoma matokeo yake walifungwa goli moja na kutolewa kwenye mashindano.
7.YANGA kuichangia CCM yaani yeye alitakiwa ajishushe waombe msamaha ila yeye ndio alikuja kuharibu kabisa akidai kwamba CCM haijaanza kusaidiwa leo na YANGA wameanza zamani wakati huo anaodai chama kilikuwa kimoja na sasa ni vyama vingi kama sasa.
8.Ali kamwe hawezi promotion yeye anaweza propaganda licha ya YANGA kufanya vizuri misimu minne mfululizo lakini ameshindwa kuwashawishi mashabiki waende kujaza uwanja kwenye mechi muhimu na kununua jezi za msimu huu ambazo zimedoda sokoni.
9.kudandia kila jambo la SIMBA bila kujua kwamba mengine ni mtego ili team yake itolewe kwenye reli mara anajiita Ali mpanzu yaani kiufupi Ali Kamwe ana utoto mwingi sana na wale wenzake waliokuwa wanalia siku ya harusi yake.
10.kujificha kwenye kivuli cha derby YANGA licha kuchukua ubingwa back to back ila mafanikio yake kwenye caf champions league ni ya kusua sua cha ajabu wanajificha kwenye kivuli cha derby yaani team isajili wachezaji kutoka nje halafu iishie mtoano kila mwaka ukiwagusa wanasema derby tumemfunga mtani.
Alamsik.
Wananchi mkanunue jezi yaliyopita si ndwele.
Ila aliyekaribu na Ali Kamwe amshauri aache kuropoka maana maadui zake ni wengi kuliko marafiki wanamtafutia angle na mmoja ni diwani mtarajiwa.