Kamati za Lowassa na Zitto zavunjwa

Kamati za Lowassa na Zitto zavunjwa

Kipengele a ndio kinahusika, kwani kamAti za Bunge zinaundwa kwa mujibu wa kanuni na huwa zinaundwa upya kila baada ya miaka miwili na nusu ya uhai wa Bunge, so zilipaswa kuundwa upya , ila la kuifuta kamati ya POAC hoja ya spika leo ilikuwa hakuna bunge lolote duniani ambalo lina kamati kama hiyo, ila kamati ya hesabu za serikali ndio ipo na inakagua pamoja na mashirika ya umma kwani ni sehemu ya serikali hayo mashirika.

Ila kiuhalisia Spika amevunja kanuni kwani kamati ya POAC imeundwa kwa mujibu wa kanuni, yaani imetajwa na kanuni kuwa itakuwepo, hivyo alipaswa kuleta hoja ya kurekebisha kanuni kwanza ili Bunge liamue ndipo aweze kuifuta hiyo kamati , na sio kama alivyofanya.

Kamati nyingine hazijatajwa kwenye kanuni kama zilivyo za POAC, PAC NA LAAC , ndio maana Spika amepewa uhuru wa kuunda kamati kadiri atakavyoona inafaa kwa mujibu wa kanuni.

Asante Mkuu kwa ufafanuzi uliotoa. At least umenipa mwanga sasa.

Kwa hiyo, POAC ilikuwa siyo kamati ya kudumu?

Umesema kiuhalisia Spika amevunja kanuni kwani POAC imeundwa kwa mujibu wa kanuni, so alitakiwa kwanza hiyo kanuni ibadilishwe kabla ya kuivunja POAC.

Unaweza kuiweka hiyo kanuni hapa kama ilivyo?

Pili section 38 of the Public Audit 2008 inaongelea kuhusu
Parliamentary Oversight Committees.

Section 38(1) says that "The Public Accounts Committee, Local Authorities Accounts Committee and Parastatal Organisations Accounts Committee shall discuss the reports of the Controller and Auditor-General after they have been tabled in the National Assembly."

Najua Mwanasheria Mkuu alileta Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Mwaka 2013 (The Written Laws Miscellaneous Amendments Bill 2013)

Je, huu mswada unafanya pia marekebisho kwenye hiki kifungu kwa kuindoa POAC kama moja ya Parliamentary Oversight Committees?

Kama haufanyi marekebisho, hata kama hiyo kanuni ya Bunge ingebadilishwa kwanza kabla ya kuivunja POAC, maamuzi ya kamati ya kanuni ya kuivunja POAC yangekuwa halali?
 
Zitto atapata wapi jukwaa la kueneza uongo wake

Zitto kesha tajirika.

Namwonea huruma Bw William Erio Mkapa, DG wa PPF maana alimweka Zitto kama mungu wake kumsaidia kuzima hoja za ubadhirifu wake pale PPF na wakurugenzi wake. Kweli Mungu kaona na kusikia kilio cha waja wake. Cheyo si mwepesi kama Zitto

Zitto alilichukulia suala la group Endowment ya PPF kama mtaji wa kuikomba PPF, na ameikomba kweli!
 
Taarifa zako ni za zamani sana , soma kanuni ya 113 , ujue kuwa mawaziri na manaibu sio wajumbe wa kamati za Bunge, hivyo Simbachawene na Kairuki sio wajumbe.

Pili , ukisoma hiyo kanuni utajua nani mwenye mamlaka ya kuunda , kamati kazi yake ni kumshauri na sio kuunda , mamlaka ya kuunda ni ya Spika.

Aidha , ukisoma kanuni hiyo ya 113 kifungu cha 11 utaona kuwa kamati zilizotajwa kwa majina kwenye kanuni ni tatu nyingine anapanga Spika kadiri atakavyoona inafaa..........

mkuu,
Nimekupata.
Hebu tujaribu kupambanua hili neno KUMSHAURI. Hudhani hata kuunda kamati hizi lazima kuna ushauri aliopata kutoka kwa hawa wajumbe wa kamati ya kanuni. Na kama sivyo, kwa nini hajitokezi hata mjumbe mmoja katika kamati hiyo na kutoa dukuduku lake kuhusiana na hilo.
 
EMT, bahati mbaya device ninayotumia kwa sasa haiwezi kukopy na kupaste, ila naomba mwenye kanuni za Bunge aweke kanuni yote ya 113 , itasaidia sana wengi kupata mwanga , hada wale ambao wana nia ya kujifunza.

Pili, POAC ilikuwa kamati ya kudumu ila maisha yake ni miaka miwili na nusu na inaundwa upya kama zilivyo kamati nyingine, ila ninachosema ni kuwa kamati tatu za mahesabu zimeundwa kwa kutajwa majina na kanuni, sasa kuziondoa ni lazima ufute kwenye kanuni kwanza, pili hata kifungu cha sheria ulichonakili hapo ndio ambacho kimefutwa leo na kubadilishwa, hivyo serikali na Spika walishakubaliana kuifuta POAC ndio maana kifungu kipya hakikutaja tena hizo kamati, so huu ni mkakati wa serikali kwa kushirikiana n Spika.

Wabunge wanapaswa kumbana huyu mama hapo, kuwa sheria ilitangulia na yeye baadae kaja kutamka tuu...
 
  • Thanks
Reactions: EMT

Ushauri unaweza kupokelewa ama kukataliwa.....

Naomba uweke hiyo kanuni ya 113 yote kama ilivyo li kusaidia kupanua wigo wa mjadala...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ushauri unaweza kupokelewa ama kukataliwa.....

Naomba uweke hiyo kanuni ya 113 yote kama ilivyo li kusaidia kupanua wigo wa mjadala...

Mkuu,
Hii ndiyo kanuni ya 113 kwa wadadavuzi.

113.-(1) Mbunge yeyote ambaye si Waziri au Mwanasheria Mkuu
wa Serikali anaweza kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge yoyote ambayo inahusika na Kanuni hii na Waziri mwenye
dhamana ya jambo lolote linalopelekwa au kujadiliwa na Kamati,
pamoja na Naibu Waziri aliyeteuliwa kumsaidia Waziri huyo,
watakuwa wajumbe wa Kamati wakati Kamati itakapokuwa
inashughulikia jambo hilo.
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya (1) ya Kanuni hii, Mbunge
Muundo
wa
Kamati
za
Kudumu
za
Bunge70
yeyote ambaye ni Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya
hatachaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali,
Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Hesabu za
Mashirika ya Umma.
(3) Wajumbe wa Kamati zote watateuliwa na Spika kwa namna
ambayo itawezesha kila Mbunge kuwekwa kwenye Kamati
mojawapo.
(4) Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge,
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na Kamati ya
Masuala ya Ukimwi, wanaweza pia kuteuliwa kwenye Kamati
nyingine.
(5) Wakati wa kuteua Wabunge kuwa Wajumbe wa Kamati
mbalimbali, Spika:-
(a) atateua idadi ya Wabunge inayolingana kwa
kila Kamati, isipokuwa kama imeelekezwa
vinginevyo katika Kanuni hizi;
(b) atazingatia aina zote za Wabunge na kuwateua
Wabunge wa aina mbalimbali kwa kila Kamati,
akiongozwa na kigezo cha asilimia ya kila aina
ya Wabunge hao ilivyo Bungeni;
(c) kwa kadri inavyowezekana, atayapa kipaumbele
matakwa ya Wabunge wenyewe, lakini
hatalazimika kutosheleza kila takwa au ombi;
(d) atazingatia haja kwa kila Kamati kuwa na
Wabunge wenye uzoefu au ujuzi maalumu kuhusu
kazi za Kamati hiyo.
(6) Katibu atahakikisha kuwa Wabunge wote wanapewa orodha
inayoonesha jinsi walivyoteuliwa katika Kamati mbalimbali.
(7) Ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka
mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza
ya maisha ya Bunge.
(8) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (7) ya Kanuni hii, Mbunge
yeyote anaweza kuteuliwa tena katika Kamati aliyokuwa
anaitumikia katika nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge.71
(9) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (7) ya Kanuni hii, Mbunge
atakoma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge endapo
atateuliwa kuwa Waziri au kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika.
(10) Wajumbe wa kila Kamati watawachagua Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwao ambao kwa muda
wote watakaokuwa Wabunge, wataendelea kushika nafasi hizo
mpaka mwisho wa kipindi kilichotajwa katika fasili ya (7) ya Kanuni
hii, lakini wanaweza kuchaguliwa tena.
(11) Wenyeviti wa Kamati za Bunge zinazosimamia matumizi ya
fedha za Umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya
Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya
Umma watachaguliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Kamati
hizo ambao wanatoka katika Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
 
Point yako naona inaangukia hapa.

(11) Wenyeviti wa Kamati za Bunge zinazosimamia matumizi ya
fedha za Umma ambazo ni Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya
Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya
Umma watachaguliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Kamati
hizo ambao wanatoka katika Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Sidhani kama hiki kipendele kingetakiwa kwanza kielekebiswe kabla ya kuiondoa kwa sababu kipo kwaq ajiri maalum ya kuwapa wapinzani kipao cha mbele.
 
EMT, bahati mbaya device ninayotumia kwa sasa haiwezi kukopy na kupaste, ila naomba mwenye kanuni za Bunge aweke kanuni yote ya 113 , itasaidia sana wengi kupata mwanga , hada wale ambao wana nia ya kujifunza.

Pili, POAC ilikuwa kamati ya kudumu ila maisha yake ni miaka miwili na nusu na inaundwa upya kama zilivyo kamati nyingine, ila ninachosema ni kuwa kamati tatu za mahesabu zimeundwa kwa kutajwa majina na kanuni, sasa kuziondoa ni lazima ufute kwenye kanuni kwanza, pili hata kifungu cha sheria ulichonakili hapo ndio ambacho kimefutwa leo na kubadilishwa, hivyo serikali na Spika walishakubaliana kuifuta POAC ndio maana kifungu kipya hakikutaja tena hizo kamati, so huu ni mkakati wa serikali kwa kushirikiana n Spika.

Wabunge wanapaswa kumbana huyu mama hapo, kuwa sheria ilitangulia na yeye baadae kaja kutamka tuu...

Nimekupata Mkuu. I hope atakayekuwa na hizo kanuni ataziweka hapa though umeshafafanua vya kutosha.

Kama kifungu cha 38(1) cha Public Audit Act 2008 kimefutwa, inaonyesha wazi kuwa kulikuwa na "conspiracy" kati ya serikali na sehemu fulani ya bunge kuitumbukiza POAC baharini.

Inaonyesha wazi kabisa kuwa maamuzi ya kuifuta POAC yamefanywa na serikali na siyo kamati ya Kanuni. Kamati imetumika kama tuu rubber stamp ya maamuzi yaliyokwishafanywa na serikali kuitokomeza POAC.

Lakini nimeshangaa sana kwamba wakati wabunge hasa wa upinzani na wale walioko POAC wanapitia
Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Mwaka 2013, kweli kabisa hawakuona na kuhoji kwa nini POAC inaondolewa kama moja ya Parliamentary Oversight Committees under the Public Audit Act 2008?

Kweli tuna wabunge.

wa ccm ni 9+2cuf dhidi ya 3 upinzani sasa matokeo yake unategemea nini?

Wajumbe wa kamati siyo wanateuliwa kwa kujaza hafasi tu, kuna vigezo vinatumika. wabunge wa upinzani wanakuwa wachache kwa sababu hata namba yao bungeni ni ndogo halafu uzoeefu na fani zao zinachangia pia.
 
Mimi nakuelewa kwani una hasira kuwa Kamati ya mtu wako imevunjwa na kupunguziwa mamlaka ya kujua nini kinaendelea kwenye masuala ya ulinzi na usalama, .....
Liandikwalo, ndilo liwalo!. No one can stop, destiny!.
"Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".
Pasco.
 
Nimekupata Mkuu. I hope atakayekuwa na hizo kanuni ataziweka hapa though umeshafafanua vya kutosha.

Kama kifungu cha 38(1) cha Public Audit Act 2008 kimefutwa, inaonyesha wazi kuwa kulikuwa na "conspiracy" kati ya serikali na sehemu fulani ya bunge kuitumbukiza POAC baharini.

Inaonyesha wazi kabisa kuwa maamuzi ya kuifuta POAC yamefanywa na serikali na siyo kamati ya Kanuni. Kamati imetumika kama tuu rubber stamp ya maamuzi yaliyokwishafanywa na serikali kuitokomeza POAC.

Lakini nimeshangaa sana kwamba wakati wabunge hasa wa upinzani na wale walioko POAC wanapitia
Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Mwaka 2013, kweli kabisa hawakuona na kuhoji kwa nini POAC inaondolewa kama moja ya Parliamentary Oversight Committees under the Public Audit Act 2008?

Kweli tuna wabunge.

Kuhusu wabunge wa upinzani walihoji sana na walipeleka hoja ya marekebisho ya Halima, wengine walikua Mnyika na Cheyo , ila CCM waliounga mkono walikuwa January , Serukamba na wengine ambao siwakumbuki.

Kuhusu kutoona POAC ni kweli kwani hata hizo kamati nyingne mbili hazikutajwa pia , ila walisema tuu kuwa kamati za mahesabu hazitajadili mpaka............so kwa mtu ambaye hukua unajua nini kilipangwa wakitaja kamati za mahesabu basi kila mtu anajua ni zile tatu kumbe walikuwa tayari wameingiza jambo walilokuwa wanajua lingetokea baadae......

Pili, kuhusu kamati kutumika ni kweli kabisa na hata hivyo akidi haikutimia , naomba aliyeweka kanuni ya 113 atuwekee nyongeza ya nane ya kanuni yote then mtanielewa naongea nini .
 
  • Thanks
Reactions: EMT
mkuu,
Nimekupata.
Hebu tujaribu kupambanua hili neno KUMSHAURI. Hudhani hata kuunda kamati hizi lazima kuna ushauri aliopata kutoka kwa hawa wajumbe wa kamati ya kanuni. Na kama sivyo, kwa nini hajitokezi hata mjumbe mmoja katika kamati hiyo na kutoa dukuduku lake kuhusiana na hilo.

Kwanza kifungu kinasema chochote kuhusu koramu?

Kushauri kama kawaida ya sheria zetu nyingine, spika ndiye atakuwa na maamuzi ya mwisho au discretion.
 
Kwa ujumla kamati ya POAC ilikuwa na tija kwa watanzania na ilimpata Mh.Zitto na makamu wake Mh. Filikunjombi wote walikuwa makini katika kusimamia mahesabu ya mashirika ya umma. Kwa kuiondoa hii kamati ni pigo kwa watanzania kwa ujumla. Inatufundisha kitu sisi watanzania kuwa baadhi ya viongozi hawako kwenye nafasi zao kuwatetea wanyonge bali ni watu wachache wenye nguvu katika nchi na ndo waliowaweka kwenye nafasi husika. Hima watanzania tuseme basi sasa yatosha na umangimeza wa viongozi wetu na chama chao.
 
Kwanza kifungu kinasema chochote kuhusu koramu?

Kushauri kama kawaida ya sheria zetu nyingine, spika ndiye atakuwa na maamuzi ya mwisho au discretion.

Koramu imetajwa kwenye kanuni nyongeza ya nane , nyongeza hii iwekwe yote then mjadala utakuwa guided vizuri.....
 
Back
Top Bottom