Kamati za Lowassa na Zitto zavunjwa

Kamati za Lowassa na Zitto zavunjwa

Hii nikuonyesha zahiri kuwa Zitto Kambwe alikuwa Mwiba mshungu kwa mafisadi ambao Mh Kikwete kashindwa kuwazibiti na sasa wanamzibiti yeye kwa kuipangia Serekali iendeshe mambo vipi.

Hongera Mh Zitto kwa uzalendo wako na ushujaa wako kazi ulio ifanya tumeiona na tunasamini ushujaa wako.
 
huo ni uwoga wa membe na walioficha mabilioni.zitto usikate tamaa.first lady anaogopa kivuli chake:crazy:.rais ajaye kama ni waCCM au CHADEMA asitoke kusini yaani lindi au mtwara.washapata miaka 10 inawatosha.gesi siyo ya kwao,ni ya watanzania wote.baba wa taifa hakukosea, aliwajua hao wakorofi, ndio maana hawakuwajengea hata barabara.
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimedhamiria kumtumia Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuandaa mkakati wa kuwaumbua na kuwazima kisiasa wanasiasa kadhaa wa CCM na upinzani wanaosemekana kuwa “wasumbufu”, wakiwamo Spika aliyepita Samuel Sitta, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Katika kutekeleza dhamira hiyo, Makinda anachukua hatua mbalimbali za kiutawala, zenye lengo la kupunguza makali ya wanasiasa hao, wanaoonekana kuwa na malengo mapana ya kisiasa mbele ya safari.
Mbali na hilo, Makinda, ambaye pia anasemekana “kuwekwa mfukoni na serikali” amedhamiria kupunguza nguvu za upinzani kwa ama kutumia kanuni za Bunge au kuvunja baadhi ya kanuni hizo.
Katika kutekeleza moja ya hatua hizo, jana Makinda alifanya mabadiliko makubwa ya kamati za Bunge, akafuta baadhi ya misingi iliyoachwa na Sitta.
Katika kukamilisha mpango huo, Makinda aliunganisha kamati mbili za Bunge zilizokuwa zinaongozwa na wabunge wa upinzani - Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma iliyokuwa chini ya Zitto na Kamati ya Hesabu za Serikali iliyokuwa chini ya John Cheyo wa UDP.
Maana yake ni kwamba, Zitto na Cheyo watalazimika kupigiwa kura ili apatikane mmoja wa kuongoza kamati mpya.
Baadhi ya wachambuzi wa habari za siasa wanasema kimantiki iliyovunjwa ni kamati ya Zitto, ambayo inaunganishwa na ya Cheyo.
Wanasema lengo ni kumaliza nguvu na machachari ya Zitto, ambaye hana ukaribu na CCM kama alivyo Cheyo.
Mbali ya mkakati huo wa kumkomoa Zitto, Makinda pia ana mkakati wa kupunguza idadi ya wapinzani katika Kamati ya Uongozi ya Bunge kutoka watatu hadi wawili.
Wachambuzi wanasema hizi ni jitihada za Makinda kufuta nyayo za Sitta, kwani ndiye aliyepitisha kanuni zilizowapatia wapinzani kamati tatu, na kuingiza wajumbe watatu wa upinzani katika kamati ya uongozi.
Makinda hakuishia hapo. Amevunja pia Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, ambayo pia iliasisiwa na Sitta.
Lakini tafsiri pana ya uamuzi huo ni kwamba, kwa kuivunja kamati hiyo na kuunda mbili, amemfanya Lowassa aongoze Kamati ya Ulinzi na Usalama, huku ya nje ikitafutiwa mtu mwingine.
Wajuzi wa siasa za ndani ya CCM wanasema uamuzi huo umelenga kumnusuru Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ambaye hakuwa anapenda wizara yake kuwekwa chini ya kamati inayoongozwa na Lowassa.
Ikumbukwe Membe amekuwa akitajwa kuwa hasimu wa kisiasa wa Lowassa ndani ya chama katika kinyang’anyiro cha kuwania urais 2015.
Miezi kadhaa iliyopita, Membe alilalamikia hatua ya kamati ya Lowassa kutembelea balozi za Tanzania nje ya nchi, hasa Ulaya na Marekani.
Malalamiko hayo yalihisiwa kwamba kuna jambo Membe hakutaka kamati ya Lowassa ilijue katika balozi zetu; na kwa mantiki hiyo hakutaka kuwajibika kwake kwa sababu za ushindani wao wa kisiasa.
Mbali na Membe, mtu mwingine ambaye amekuwa hasimu wa kisiasa kwa miaka ya karibuni ni Sitta, ambaye aliunda kamati iliyofanya uchunguzi wa sakata la Richmond, ambalo lilimfanya Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008.
Kwa kuwa na wizara ya Sitta ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikuwa chini ya kamati ya Lowassa, kitendo cha Makinda kuiondoa kwake kinampa ahueni Sitta, ambaye naye asingependa kusimamiwa na kamati inayoongozwa na Lowassa.
Baadhi ya wabunge wanaomkosoa Makinda, pamoja na kutambua kuwa anafanya hivyo kumnusuru Membe na kupalilia sokomoko la kisiasa ndani ya CCM, wamesema analenga pia kudhoofisha nguvu ya upinzani bungeni.
Wanasema anafanya hivyo ili kujipendekeza kwa serikali na CCM, huku akilenga kuwania tena uspika 2015, kipindi ambacho tayari ameshatangaza kuwa hatagombea ubunge.
Miongoni mwa mawaziri ambao wanasemekana kutumiwa na serikali kumdhibiti na kumpotosha Makinda ni William Lukuvi.
Vile vile, wachambuzi wanasema hakuna mantiki ya kuivunja kamati ya Zitto, yenye kushughulikia mashirika 280, halafu ikaunganishwa na kamati yenye majukumu mazito kama ya Cheyo.
Wanadai Makinda anakusudia kupunguza makali ya kamati tatu nyeti zilizokuwa zinatumiwa na wapinzani kuleta uwazi zaidi katika kuisimamia serikali.
Kamati ya wapinzani ambayo haikuguswa ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP), anayesemekana kuwa kipenzi cha CCM na Rais Jakaya Kikwete.
Kabla yake, kamati hiyo ilikuwa inaongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA).
Kamati hizi zimekuwa msaada mkubwa sana kwa kusimamia fedha za serikali kuu na zile za mitaa, lakini kwa mabadiliko yaliyofanywa na Makinda, wapinzani watabakiwa na fursa finyu.
Kwa siku za karibuni, Zitto ameonekana kuisumbua serikali katika masuala mbalimbali, na alitoa matamko makali katika sakata la gesi ya Mtwara.
Kijumla huu ni mkakati wa Makinda kuidhibiti CHADEMA bungeni ili isiongoze kamati nyeti, kwani hata jinsi Mrema na Cheyo walivyopewa fursa hizo, ilitokana na kupindwa kwa kanuni.
Kimsingi kamati zao zilipaswa kuongozwa na wabunge wa CHADEMA ambao kikanuni ndio wanaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Baadhi ya wabunge wanasema huu ni ushahidi mwingine wa ubabe wa Makinda, kwani kanuni za Bunge hazijabadilishwa ili kumwezesha kuunda na kuvunja kamati hizi mpya.


h.sep3.gif


[TD="bgcolor: #ffffff"]
• Adaiwa kumtafutia unafuu Membe

na Waandishi wetu


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
 
Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, iliyokua inaongozwa na Edward Lowassa imevunjwa na kuundwa kamati mbili ya Ulinzi na Usalama na ingine ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ya Zitto Kabwe, imefutwa kabisa.

Basically kilichotokea ni hivi (Analysis ni yangu):

Ya Lowassa imekatwa vipande; Imeundwa upya na Spika na Kamati ya Kanuni... Imeundwa Kamati 2 ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Mambo ya Nje, na ya Zitto (POAC) imevunjwa kabisa imeunganishwa na PAC ya Cheyo!

Wabunge wa kamati hizo (akiwamo Lowassa na Zitto) watalazimika kujaza fomu kuomba upya wawekwe kamati gani na wataomba kamati 3 ambapo Spika atachagua mojawapo ndio awaweke. kamati zitaundwa upya, maana zimetajwa upya kabisa.

My Take:
Kwa maana hiyo itakapounda upya ndio tutajua; ama EL anaondolewa kudhibiti vyombo vya Ulinzi, ama anaondolewa kuwadhibiti ama kuwafuatilia Membe na Sitta.

Akiwekwa kamati ya Ulinzi maana yake anaepushwa kusimamia Wizara ya Mambo ya nje na ile ya Afrika Mashariki.

Akiwekwa Mambo ya Nje ataonekana ameondolewa Ulinzi na Usalama.
lakuvunda halina ubani,kila hila ya ccm ni pembe la ngombe halifichiki,mambo yote hadharani,ccm wanazidi kujiumbua
 
Wanataka kutoa hilo kwa cheyo na siyo Zitto wanaona jamaa anawaumbua sana na hivyo mambo gani haya katika Bunge
 
Masalia Zitto kweshine, sasa naona utakuwa na adabu ndani ya chama, na kiherere kitakuisha cha kuanzzisha mtandao, sasa utakuwa mbunge tu, na soon kwenye chama utakuwa member wa kawaida tu, believe me, utabaki kuwa mwanachama,

Ndio uanze kupotea kwenye siasa, uendelee kutoa matamko ya kibinafsi, na uunde kundi jingine tena, mnafiki,
Vipi posho za NSSF utaendelea kutafuna?

Dhambi ya usaliti inakutafuna, RIP PAOC
 
Wanataka kutoa hilo kwa cheyo na siyo Zitto wanaona jamaa anawaumbua sana na hivyo mambo gani haya katika Bunge

Its true lakini alikuwa anawaumbua kwa minajili ya kujijenga binafsi, kuliko chama wala umma, go to hell mzee wa matunguli, panya hawatapona!
 
Hili litasaidia kuleta mabadiliko ya haraka zaidi katika nchi maana wenye akili zao wote wataungana kinyume na wale wenye malengo binafsi.....Its still a gud move go on mama supika, its a decree you cannot go against it....Hata shetani alifikiri akimsulubisha Yesu basi amemaliza kazi kumbe hakujua kuna kufufuka na kaburi haliwezi zika 'kweli'...utukufu wa ufufuko ulikuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo...Go go gooooooo all nature hears the word of God and you are part of it!


La pili my sincere advice to one of the kamandaz..my brother ZZK I warned you long time a go kuwa unapanda mlima kwa baiskeli badala ya kutumia engine....Kama ungejijenga kitaasisi (kama wengi walivyokushauri kwa muda mrefu sana nikiwemo) basi wenzako wangekuwa na sababu ya kuku support sasa hivi na hata magamba wasingethubutu ku-touch your position ila wamekupima kwenye mizani yao na wamekuta umepelea. Hili ni somo kwako kutoka lile neno la Mungu linalosema, '....ni bora kuwa ama baridi au moto ukiwa vuguvugu nitakutapika'. Naomba uelewe jambo moja mimi utanichukia, lakini uelewe hili its not by choice ila kwa mapenzi ya Mungu katika spiritual realm nina powers za kukuzidi sana hata 1% huwezifika ni bora ukanisikiliza otherwise wait to see the worse! Hili silisemi kwakujificha I know you know me na kwasababu hiyo ukipenda waweza nisikiliza ukiona vipi ni potezee....

I somewhere told you kuwa ninaomba na kufunga kwaajili yako and God answered my prayers sitaki kuku blackmail but the truth has to be said kwani haya yote si kwaajili ya kitu chochote bali welfare ya watoto wa Tz ambao nina convenant nao mbele ya Mungu. Uelewe God ordains some people for certain reasons hii siyo democracy it is a law of nature, and he chooses whoever he likes, siyo lazima mtu aamini lakini power will demonstrate itself and when it happens every tongue shall confess and each knee shall bow before the truth. Ukibisha basi endelea tu, ukijifunza utanikuta am still there waiting for you na nitakwambia chakufanya!
 
Back
Top Bottom