Kamati za Lowassa na Zitto zavunjwa

Kamati za Lowassa na Zitto zavunjwa

Imeunganishwa na PAC ya Cheyo.

Hii kamati itakuwa imepewa majukumu mengi ukilinganisha na jinsi mashirika yalivyooza kwa udokozi. nikiangalia wanachofanya ni kuwa na Parliamentary committees kama za UK. It'll be interesting ni kina nani watakuwa wajumbe wa PAC, hasa hasa mwenyekiti na makamu wake.
 
I think, this is latest hata hivyo ngoja tumsubiri Mpaka kieleweke amesema atarudi baadaye.

Ingia kwenye site www.parliament.go.tz...........on top of site kuna section ya publications ambayo ni drop down.......fungua............choose standings order na utapata hizi kanuni za bunge.

Nimeona lakini za Nyongeza kuanzia I hadi VIII hakuna kitu.
 
Hii kamati itakuwa imepewa majukumu mengi ukilinganisha na jinsi mashirika yalivyooza kwa udokozi. nikiangalia wanachofanya ni kuwa na Parliamentary committees kama za UK. It'll be interesting ni kina nani watakuwa wajumbe wa PAC, hasa hasa mwenyekiti na makamu wake.

Well kama walikuwa wamepanga haya yote, watakuwa wameshapanga nani atakuwa mwenyekiti na wajumbe.

UK haiwezi kuwa na POAC kwa sababu hawana mashirika ya umma.
 
Nimeona lakini za Nyongeza kuanzia I hadi VIII hakuna kitu.

Mkuu, Usishangae

Hiyo ndiyo Tanzania. hata tofuti ya bunge ni matatizo, na hakuna hata mbunge mmoja aliyeona hili na kulalamika. We'll never be serious.

Ndiyo hayo yanayotokea kwa sasa. serikali inaleta mswaada wa mabadiliko na wabunge wanapitia na kuruhusu lakini pale inapokuwa implemented ndiyo wanaanza kujua kama kulikuwa na makosa na kelele zinaanza.
 
sijui ni hii habari ina utata ama ni uamuzi wa madam spika ndiyo wenye utata?nashindwa kujua kama kamati zimevunjwa na kuundwa upya ama zimekuwa merged/kuunganishwa?

Ushahidi wa kuvunjwa ni member wa kamati za Lowassa na Zitto kuwa dissolved na kuambiwa wachaguwe ni kamati ipi wanataka kuwa members na wajaze fomu za maombi.Na ushahidi wa kuunganishwa ni shughuli/majukumu ya POAC kuhamishiwa PAC?(still confused),Mara ya Lowassa imevunjwa then imekatwa vipande(ulinzi na usalama na mambo ya nje)

Anyways kuna dalili kubwa sana za shinikizo la kisiasa kwenye maamuzi haya.

Dada Tina ulikuwa una haraka ama ni uko uliko hutumii kiswahili tena?:confused3:
 
Last edited by a moderator:
Well kama walikuwa wamepanga haya yote, watakuwa wameshapanga nani atakuwa mwenyekiti na wajumbe.

UK haiwezi kuwa na POAC kwa sababu hawana mashirika ya umma.

Uk has Public account committee inayojumuisha hata mashirika ya umma kama UK financial investment,na mengine ambayo Uk government ina shares ndani yake
 
sijui ni hii habari ina utata ama ni uamuzi wa madam spika ndiyo wenye utata?nashindwa kujua kama kamati zimevunjwa na kuundwa upya ama zimekuwa merged/kuunganishwa?

Ushahidi wa kuvunjwa ni member wa kamati za Lowassa na Zitto kuwa dissolved na kuambiwa wachaguwe ni kamati ipi wanataka kuwa members na wajaze fomu za maombi.Na ushahidi wa kuunganishwa ni shughuli za POAC kuunganiswha na PAC.
Kuna dalili kubwa sana za shinikizo la kisiasa kwenye maamuzi haya.

Ni vigumu sana kujua kama ni shinikizo la kisiasa au la. Unajua ukishang'atwa na nyoka, hata kelele za majani utapatwa na wasiwasi.

Ndiyo hii inatufanya kuanza kupatwa na maswali mengi hasa majibu yanapoonekana kama hayaridhishi kufanya uamuzi huo. let keep our eyes peeled
 
Hivi hizo kamati zilikuwa na malengo?Na malengo hayo yamefikiwa?
 
Kwa mujibu wa kanuni za bunge, kamati huwa zinabadiliswa baada ya nusu ya maisha ya bunge kwa maana kuwa, zinabadilishwa baada ya miaka miwili na nusu ya bunge bila kujali kama kuna malengo au hakuna malengo.
 
Taratibu mkuu,unaposema bila kujali kama kuna malengo au hakuna malengo una maanisha kitu gani haswa?Kwamba zilipoundwa hazikuwa na malengo ama madhumuni ya uundwaji wake?
 
Anyways kuna dalili kubwa sana za shinikizo la kisiasa kwenye maamuzi haya.

Of course. kabla ya hizi kama kuvunjwa au kuwa merged, serikali ilipeleka Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Mwaka 2013 (The Written Laws Miscellaneous Amendments Bill 2013).

Madhumuni ya Mswada huu ulikuwa ni kufanya mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumfunga kofulo CAG. Pia Mswada ilikuwa na kule kufanya mabadiliko kwenye kifungu cha
38 cha Public Audit 2008 ambacho kinasema "The Public Accounts Committee, Local Authorities Accounts Committee and Parastatal Organisations Accounts Committee shall discuss the reports of the Controller and Auditor-General after they have been tabled in the National Assembly."

Inaonekana Mswada imefuta hiki kifungu ili kurahisisha pamoja na mambo mengine kuifuta POAC.
 
Taratibu mkuu,unaposema bila kujali kama kuna malengo au hakuna malengo una maanisha kitu gani haswa?Kwamba zilipoundwa hazikuwa na malengo ama madhumuni ya uundwaji wake?

Umaana wa maelezo yangu yako kwenye kanuni hii,

(7) Ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge.

(8) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (7) ya Kanuni hii, Mbunge yeyote anaweza kuteuliwa tena katika Kamati aliyokuwa anaitumikia katika nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge.

(9) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (7) ya Kanuni hii, Mbunge atakoma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge endapo atateuliwa kuwa Waziri au kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika.

(10) Wajumbe wa kila Kamati watawachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwao ambao kwa muda wote watakaokuwa Wabunge, wataendelea kushika nafasi hizo mpaka mwisho wa kipindi kilichotajwa katika fasili ya (7) ya Kanuni hii, lakini wanaweza kuchaguliwa tena.
 
Of course. kabla ya hizi kama kuvunjwa au kuwa merged, serikali ilipeleka Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Mwaka 2013 (The Written Laws Miscellaneous Amendments Bill 2013).

Madhumuni ya Mswada huu ulikuwa ni kufanya mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumfunga kofulo CAG. Pia Mswada ilikuwa na kule kufanya mabadiliko kwenye
kifungu cha 38 cha Public Audit 2008 ambacho kinasema "The Public Accounts Committee, Local Authorities Accounts Committee and Parastatal Organisations Accounts Committee shall discuss the reports of the Controller and Auditor-General after they have been tabled in the National Assembly."

Inaonekana Mswada imefuta hiki kifungu ili kurahisisha pamoja na mambo mengine kuifuta POAC.

Mkuu, EMT

Una maana hiki kifungu cha 38 kimeondelewa kabisa kwenye sheria za The Public Audit Act 2008? au kimefanyiwa marekebisho gani hayo?
 
wakitaka wavunje zote tuu si wanawingi wa wabunge wakukubali jambo pasipo kifikiria ni nini madara yake? Bora chama kiwe hai kuliko mashahi ya taifa kuwa hai.
 
Umaana wa maelezo yangu yako kwenye kanuni hii,

(7) Ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge.

(8) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (7) ya Kanuni hii, Mbunge yeyote anaweza kuteuliwa tena katika Kamati aliyokuwa anaitumikia katika nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge.

(9) Bila ya kuathiri masharti ya fasili ya (7) ya Kanuni hii, Mbunge atakoma kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge endapo atateuliwa kuwa Waziri au kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika.

(10) Wajumbe wa kila Kamati watawachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwao ambao kwa muda wote watakaokuwa Wabunge, wataendelea kushika nafasi hizo mpaka mwisho wa kipindi kilichotajwa katika fasili ya (7) ya Kanuni hii, lakini wanaweza kuchaguliwa tena.
Nashukuru mkuu,ila naona kama tunapishana hapa,mimi nazungumzia malengo wewe unanieletea kanuni za uundwaji.

Sasa ndiyo nimeelewa ni kwanini uliniambia kuwa haijalishi kama wana malengo ama hawana.

Ila mkuu mimi nilimaanisha kuhusu kamati hizo walichokuwa wakifanya,yani majukumu yao.Ukingalia majukumu yao ndipo utaweza kuona malengo yao.Sasa ndiyo maana nikauliza kama malengo hayo yalifikiwa.

Labda nijaribu kwa namna nyingine,hizo kamati ziliundwa kwa madhumuni gani?
 
ccm,ccm,ccm,ccm,ccm.............kidumu chama cha mapinduzi,zidumu fikira sahihi za mwenyekiti wa ccm.....zidumu,ndugu zangu leo tumekuja kufanya mambo mawili cha kwanza ni kummaliza Lowassa ili urais uwe hadithi,na pili Zitto kabwe kwani amezoea sana kuchunguza chunguza hela za wakuu huko Uswiss,so tunamziba mdomo

idumu na serikali sikivu
 
Wanajitahidi kila namna kuyafuta. Tangu June 2012 hadi hii leo bado wanaendelea na uchunguzi tu!!!! Balozi wa Switzerland nchini hivi karibuni aliianika Serikali hadharani kwamba haijaomba msaada wowote toka Serikali yake katika kufuatilia/kuchunguza hayo "mabilioni ya uswiss" na kuangalia namna ya kuyarudisha nchini. Eti wakamjia juu asiingilie mambo ya ndani ya "Sirikali".

Na yale mabilioni yaliyopo Uswiss na kwingineko nayo YAMEFUTWA?
 
Nashukuru mkuu,ila naona kama tunapishana hapa,mimi nazungumzia malengo wewe unanieletea kanuni za uundwaji.

Sasa ndiyo nimeelewa ni kwanini uliniambia kuwa haijalishi kama wana malengo ama hawana.

Ila mkuu mimi nilimaanisha kuhusu kamati hizo walichokuwa wakifanya,yani majukumu yao.Ukingalia majukumu yao ndipo utaweza kuona malengo yao.Sasa ndiyo maana nikauliza kama malengo hayo yalifikiwa.

Labda nijaribu kwa namna nyingine,hizo kamati ziliundwa kwa madhumuni gani?

Mkuu nimekupata.

kila kamati ina majukumu yake lakini maajukumu ya jumla ni haya,

4.0 MAJUKUMU YA MSINGI NA YA JUMLA YA KAMATI

4.1 Kwa mujibu wa mgawanyo wa Mamlaka kama ilivyoainishwa katika vifungu vilivyotangulia, Bunge na Kamati zake za Kudumu hufanya kazi za kusimamia Utendaji wa Serikali kwa niaba ya Wananchi.

Bunge na Kamati zake ndiyo darubini (Oversight or Watch-dog organ) ya kuhakikisha kwamba mambo yote ya uendeshaji wa kazi za Dolaunafanywa kwa kuzingatia Katiba, Sheria na Kanuni zilizowekwa.
Kwa hiyo, kuna majukumu ambayo hutekelezwa na Bunge lenyewe nabaadhi ya majukumu ambayo utekelezaji wake ni wa siku hadi siku yanashughulikiwa na Kamati za Kudumu.
7
4.2 Kila Kamati ya Kudumu ina majukumu ya msingi na inalo jukumu la jumla la kufuatilia utekelezaji wa Ahadi za Serikali zilizotolewa Bungeni ambazo zinagusa mambo yaliyo katika Mamlaka ya Kamati inayohusika. Aidha, Kamati inaweza kupendekeza kwa Spika nyongeza ya majukumu ambayo yatajitokeza katika kutekeleza majukumu ya msingi. Kwa upande mwingine, Spika anaweza kukabidhi jambo lingine lolote kwa Kamati yoyote kama atakavyoona inafaa, kwa ajili ya kushughulikiwa na Kamati hiyo, kwa mujibu wa
Kanuni za Kudumu za Bunge Kanuni ya 90(1) na (2).

Kwa mfumo huu hizo kamati zitakuwa zinatumiwa kama njia za ulaji tu pamoja na siasa.Mfumo wetu wa siasa ni wa hovyo kabisa.

Hizo kamati zilizovunjwa zilikuwa ni kamati za kudumu?
 
yes, zilikuwa ni kamati za kudumu za bunge
 
Back
Top Bottom