Kamati ya ulinzi na usalama Mwanza yaamuru wabunge wa CHADEMA wakamatwe

Ninachokiona hapa ni ccm kutaka kulivuruga taifa letu kwa kisingizio cha amri za viongozi wa serikali kama wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa nk. Kwa wawakilishi wa wananchi, kama wabunge. Wakuu wa wilaya na mikoa na makada wataliangamiza taifa letu kiushabiki. Kukamata wabunge lengo ni kuivuruga mwanza na cdm. Ccm ni janga, mungu aepushie mbali.
 
Dah! Tanzania yetu sasa inakuwa ni mali ya wahuni fulani,inamaana CHADEMA wanadhani sie mabwege?

Wao wanataka wao wawe dini yetu,wao wawe miungu yetu,walimu wetu wanataka watuendeshe wanavyotaka,waende Kilimanjaro wakatawale huko wehu wao.

Sijaona hoja yako zaidi ya matusi
 
hapan ni ccm, unasemaje?
ngoja nikufundishe maana wote tukiwa na jazba sijui nani atajenga nchi hii.umma ni watu wote wenye uraia wa nchi husika.wawe chadema,wawe ccm,wawe viongozi,wawe watoto,wawe hawana chama,au vyonyote watakavyokuwa maadam ni raia kamili basi ni sehemu ya umma.kwa hiyo kundi moja likiibuka likidai lenyewe ndo umma;na wakaibuka watu eti wanalitetea kuwa lenyewe ndo umma,hapo mimi napata shida kidogo.sijui wewe mwenzangu?
 
argue dont shout! Unamjua jamaa mmoja anaitwa john shibuda?unajua chadema wanafanya nini kawe?
Ya Shibuda na Kawe yana tofauti gani na ya CCM na Lowassa na Membe au Lowassa na Sitta? Au hujui?
Na hilo la kawe ni lipi mkuu liweke hapa kama wewe sio mbea
 
ngoja nikufundishe maana wote tukiwa na jazba sijui nani atajenga nchi hii.umma ni watu wote wenye uraia wa nchi husika.wawe chadema,wawe ccm,wawe viongozi,wawe watoto,wawe hawana chama,au vyonyote watakavyokuwa maadam ni raia kamili basi ni sehemu ya umma.kwa hiyo kundi moja likiibuka likidai lenyewe ndo umma;na wakaibuka watu eti wanalitetea kuwa lenyewe ndo umma,hapo mimi napata shida kidogo.sijui wewe mwenzangu?

Mimi naendele kukumbusha kuhusu matumizi ya madaraka in a balacsed sate

la kwanza la Adam malima na SMG Morogoro (Mbuge CCM) hujajibu alishia wapi?

la pili la Hamis Kigwala (Mbunge ccm) Nzega na maandamano kupinga wawekezaji alikamatwa au kuhojiwa na nani

Nitaendele kukumbusha kila tunavoenda mbele kama ccm wanaruhusia kuvunja sheria na kama hapana je huo ndio utawala bora?
 
ya shibuda na kawe yana tofauti gani na ya ccm na lowassa na membe au lowassa na sitta? Au hujui?
Na hilo la kawe ni lipi mkuu liweke hapa kama wewe sio mbea
wote ki msingi wako sawa.sasa mbona wewe washabikia makundi ndani ya ccm? Au ndo "waswahili husema nyani haoni..................."

 
Dah! Tanzania yetu sasa inakuwa ni mali ya wahuni fulani,inamaana CHADEMA wanadhani sie mabwege?

Wao wanataka wao wawe dini yetu,wao wawe miungu yetu,walimu wetu wanataka watuendeshe wanavyotaka,waende Kilimanjaro wakatawale huko wehu wao.

Wewe huna hoja. Unatetea visivyotewa. Acha umandazi.
 
MImi ninachowalaumu viongozi wa chadema ni jazba na kutofuata utaratibu?nani kasikia waliyokuwa wanayasema hawa jamaa?Eti wanataka wakamng'oe mkurugenzi kwa maandamano! This is a craizy decision! Toka lini watumishi wa uma wakuajiriwa wakang'olewa kwa maandamano ya makundi ya kisiasa?
Acha porojo wewe!\ulikuwepo kwenye mkutano pale Furahisha? au unajiongelesha tu!! Hii tabia ya watanzania kujisikia wanajua mambo ambayo hawayajui ni upuuzi.

Wenje na kiwia walichofanya ni kukusanya majina na sahihi za wakazi wa Nyamagana na ilemela ili waweze kwenda kushinikiza mkurugenzi wa jiji kuondolewa.
hayo maandamano unayoyasema wewe uliyasikia wapi???

Nonsense.
 
hakushinda kikwete.alishinda silaa.kuhusu idadi ya kura hakuna anayezijua zaidi yako wewe na viongozi wa chadema kwa sababu wao peke yao ndo wenye akili nawaliosoma.

Wengine wote wakiwemo walioendesha zoezi la uchaguzi hawajui kitu.
walioendesha uchaguzi waliendesha kwa akili ya kiccm! Ccm ni janga,mungu aepushie mbali.
 
wote ki msingi wako sawa.sasa mbona wewe washabikia makundi ndani ya ccm? Au ndo "waswahili husema nyani haoni..................."

Usiwe mpuuzi wewe, hiyo ndio Siasa. Huwezi kuwepo kwenye siasa bila ya kuwa na mamluki ndio maana kila mamluki anadhibitiwa kulingana na athari zake kwa chama. Wengine wamelishwa sumu, wengine wameharibiwa macho, wengine wametengenezewa kashfa ambazo kiuhalisia sio zao peke yao, wengine wamefukuzwa kwenye vyama vyao na visisimizi kama vishibuda vinaachachwa lakini vinaangaliwa kwa macho makali, vikizingua vinashughulikiwa based on their impact kwa chama...
 
kwa hiyo unadhani kuna haja ya kuwa na taasisi mbalimbali?unadhani tuna haja ya kuwa na utawala wa kisheria?unadhani ipo haja ya kuwa na taratibu na kanuni?
na je hilo la kada wa ccm kutoa amri ya kukamata mbunge? Au mwakilishi wa wananchi? Nao huo ni utawala wa sheria? Ccm ni zaidi ya uijuavyo!
 
ngoja nikufundishe maana wote tukiwa na jazba sijui nani atajenga nchi hii.umma ni watu wote wenye uraia wa nchi husika.wawe chadema,wawe ccm,wawe viongozi,wawe watoto,wawe hawana chama,au vyonyote watakavyokuwa maadam ni raia kamili basi ni sehemu ya umma.kwa hiyo kundi moja likiibuka likidai lenyewe ndo umma;na wakaibuka watu eti wanalitetea kuwa lenyewe ndo umma,hapo mimi napata shida kidogo.sijui wewe mwenzangu?

Ukinijibu ya Adam malima na hamisi kigwangala untanijibu ya Epa na wahalifu wanaorudisha fedha bila adhabu, ya Richmond

na utekelezaji wa maazimio ya bunge, ya mkapa na Kiwira coal mine na mengine mengi ya kipuuzi kuhusiana na serikali yako ya

ccm.

Tunachoongelea hapa ni matumizi ya madaraka in a balanced state. yaani kama utamhukum CUF au NCCR au Raia

yoyote kwa kosa flani lazima utaratibu huohuo utumike kuwahukumu ccm pia pale wanapokosea. Tatizo ni matumizi ya ovyo ya

madaraka kwa kuona watu wa vyama vya upinzani wanapokosea, na kufumba macho makada wa ccm wanapokosea.

Tiririka betlehem kuelezea hao wakosaji ukizingatia utawara bora kama kweli haki, sheria na taratibu zinafuatwa na watawala

hususani pale makada wa ccm wanapokesea. (Tukisema wapinzani wanakandamizwa tunakosea?)
 
Sasa baba v,matusi hapo ni yapi?hivi mtu anakurupuka na kushawishi watu kufanya fujo wewe na uelewa wako unaona wapo sawa?wangesema haya waislam tungeanza kusema wahajasoma,wamesema chadema wako sawa siyo?watu wanadai kulia na kucheka zote kelele.
 
Tupendekeze kwenye katiba mpya jeshi letu liwe na operational independence ili kusiwe na mianya ya viongozi wa serekali na vyama vya siasa kuwaingilia polisi kwenye kazi zao, waachwe wafanye kazi kwa kutumia taaluma yaona si vinginevyo. Kama mtu ametoa matamko mahali basi iwe ni juu ya polisi kuya analyse na kuamua kama kuna haja ya kumkamata mtu au hakuna.
 
CHADEMA wao wanapingana na kila mtu serikalini.sio kwamba ndo wanaanza na mkurugenzi leo.WAlianza na kikwete alipochaguliwa kuwa raisi.walisema hawamtambui bila maelezo ya kueleweka. Slaa alipohojiwa BBC kuhusu kutomtambua Kikwete akawa anajichanganya mpaka watangazaji wakawa wanacheka!,Kikwete alipofika bungeni wakamsusia; wakakoka nje eti wanachungulia madirishani!, waliposhindwa hila zao hizi wakaamua kumtembelea ikulu kisha wakaanza hila nyengine.

Mara ngapi wamekuwa wakipingana na wakuu wa mikoa?wakielekezwa jambo "A" wao wanasema sisi tutafanya "B" tuone watatufanya je? mara ngapi wamekuwa wakiwapinga polisi akiwemo IGP? (Kwa hiyo kwa mtitazo wa CHADEMA ;kama ni kutaka kuwaridhisha;basi tuondoe wakuu wa wilaya.mikoa,rais,polisi n.k).

Kwa hiyo CHADEMA wanataka watu waamini kwamba wao tu tu ndo wenye akili, wao tu ndo wenye haki,wao tu ndo wasomi, wao tu ndo wanaojua lakini wao tu ndo wanaodhulumiwa. CHADEMA wanataka kutuaminisha kwamba wao ni zaidi ya serikali,wao ni zaidi ya polisi, wao ni zaidi ya sheria. CHADEMA wanataka kutuonesha kwamba wao wanaweza kufanya lolote watakalo bila kuulizwa na yeyote.

CHADEMA wanataka Watanzania waamini kwamba,watumishi wa umma hawana akili wala hawajasoma,wanasheria hawajui walitendalo, viongozi wa serikali hawajasoma na hawana akili sawasawa na polisi kadhalika hawajui walifanyalo.Watu wenye fikra za namna hii ni watu wa hatari kwa taifa lolote lile na "kama tukitegemea watu hawa ndo watakaoikomboa tanzania; tutakuwa watu maskini kupita watu wote".
Mkuu tutakuwa masikini mara ngapi tena maana tumeshakuwa masikini tayari. Ila hapo kwenye red naona ndivyo walivyo, kama unaweza kumpa nafasi ya uongozi mtu anayemiliki kampuni inayoshiriki katika kuiba maliasili Tanzania hivi kweli wana akili timamu kama siyo marobot ni nini? mapolisi wanashirikiana na wezi, wanua waandishi wa habari na wananchi wengine kwa sababu ya kulinda mali za matajiri utasema wana akili kweli au ni hayawani! Kuhusu kusoma au kutosoma nakubaliana nawe kwamba kama tunatafuta wasomi viongozi wetu na watumishi wa umma kwa ujumla wamesoma lakini hawajaelimika ndiyo maana wanaongoza taifa kwa kasi isiyoridhisha na kila siku tija ya watumishi wa umma inashuka. Hatuwezi kuendelea mpaka tutakapopata watumishi walioelimika badala ya waliosoma tulionao sasa.
 
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na mkuu wa wilaya ya Nyamagana, ambaye pia ni kada maarufu wa CCM amemuamuru kamanda wa polisi wilaya(OCD) kuwakamata mara moja wabunge wa Chadema, Ezekiel Wenje na Highness Kiwia kwa kile kinachosemwa kuwa walitoa matamko ya uchochezi katika mikutano yao
Tabia ya serikali ya CCM kuwadhalilisha wabunge wa upinzani ndilo chimbuko la ghasia mara kwa mara, sasa fikiria watu wa Mwanza wakiandamana kudai wabunge wao waachiliwe si utakuwa mwanzo wa vurugu na kuuwa watu kama kawaida ya CCM na serikali yake??? Mkuu wa wilaya anamamlaka gani ya kumuweka ndani mbunge wa wananchi??? Katiba mpya iweke wazi kazi za wakuu wa wilaya na mikoa, tena hivi vyeo ni vya kisiasa
vifutwe tuweke watawala wa kiserikali wawajibike kwa wananchi sio chama cha siasa kama ilivyo sasa!!!!
 
MImi ninachowalaumu viongozi wa chadema ni jazba na kutofuata utaratibu?nani kasikia waliyokuwa wanayasema hawa jamaa?Eti wanataka wakamng'oe mkurugenzi kwa maandamano! This is a craizy decision! Toka lini watumishi wa uma wakuajiriwa wakang'olewa kwa maandamano ya makundi ya kisiasa?JE! tukiruhusu makundi mbalimbali yakiona hayaridhishwi na utendaji wa mtumishi fulani (wa kuajiriwa;si wa kisiasa) yawe yanavamia halmashauri na kumuondoa huku ana mikataba nakadhalika unadhani tutakuwa tunafanya mambo ki taalam au kwa emotions! unadhani ni nini matokeo yake?unadhan hali ya usalama wa watumishi wa umma itakuwa je?unadhani ni nini majukumu ya vyombo vya usalama?Rais mwenyewe anaweza kufika mahali akakuta mtendaji flani hafanyi vizuri;anachofanya si kumuondoa bali kuagiza mamlaka inayohusika imchukulie hatua.Sasa ninichojiuliza kwamba kama chadema hawana tabia ya kufuata utaratibu na kuheshimu vyombo na mifumo vilivyopo(Institutional and structural framework) pamoja na mgawanyo wa majukumu na madaraka, wakiwa nje ya serikali; sijui wakiwa wao ndo viongozi wa serikali itakuwaje?
Mkuu soma habari za Misri utapata majibu, haki inapatikana kwa maandamano ikiwa itadhulumiwa kwa nguvu za watawala, unadhani Mbaraka angeliondoka Cairo????

 
Mkuu umemaliza hii mijitu inatumia kichwa kufugia nywele yanauzi balaa
Dah! Tanzania yetu sasa inakuwa ni mali ya wahuni fulani,inamaana CHADEMA wanadhani sie mabwege?

Wao wanataka wao wawe dini yetu,wao wawe miungu yetu,walimu wetu wanataka watuendeshe wanavyotaka,waende Kilimanjaro wakatawale huko wehu wao.
 
Back
Top Bottom