Shemsa Mohammed aongoza Kamati ya Siasa ya mkoa wa Simiyu kuhitimisha kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wilaya ya Busega

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu chini ya Mwenyekiti wake Ndg Shemsa Seif Mohammed leo tarehe 06/12/2023 imehitimisha ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 ndani ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Busega.

Kwenye wilaya ya Busega, Jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya zaidi ya bilion 1.112 iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekaguliwa.
Miradi hiyo ni pamoja na;

1. Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji Cha Mwakiloba,iliyopo kata ya Lutubiga, itakayogharimu Tsh 100,000,000/.

2. Ujenzi wa Mradi wa Maji Kabita kata ya Kabita, unaogharimu Tsh 767,503,222/

3. Matengenezo ya Barabara ya Magulanja-Bomani(km 1), Nyang'hanga-Mwanogi(km 1.8), Katamilija-Milimani(km 1.04), Bus Stand-Methodist sec(km 0.66) uliopo kata ya Nyashimo uliogharimu Tsh 238,000,000/

4. Mradi wa Vyumba 6 vya Madarasa Shule ya Sekondari Masanza kata ya Kiloleli, uliogharimu Tsh 120,000,000/.

5. Usambazaji wa Umeme Kijiji Cha Milambi, kata ya Mwamanyili uliogharimu Tsh 122,800,000/.

6. Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wenye Uhitaji Maalum (GPE LANNESII) Shule ya Msingi Mwamanyili uliopo kata ya Mwamanyili uliogharimu Tsh 100,000,000/

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Simiyu imetoa Ushauri na kuielekeza Serikali ya Mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahya Nawanda kukamilisha Miradi ya Maendeleo Kwa Wananchi kwa wakati.
Huku Kamati hiyo ikiwa imeridhishwa na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi. 2020/2025.

Lumen Mathias Ngunda
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Simiyu

WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.26.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.29.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.46.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.53.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.50(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.49(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.50.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-06 at 19.59.38.jpeg
 
Back
Top Bottom