#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Tunaenda kinyume nyume , dunia iko kwenye hatua za mwisho za corona Rais anataka tuanze upya , yaani turudi 2020 kukabiliana na corona, huyu Rais mshauri wake ni nani? anajua madhara ya kutanga corona hewa? kweli tuna kiongozi bendera fuata upepo.
 
..hakuna jipya kwenye corona.

..njia ya kujifukiza imeondoka na bwana mkubwa na wasaidizi wake wa karibu.
 
Matumizi mabaya ya kodi za wananchi tu taarifa gani watazitoa zaidi ya porojo tu hv watanzania wanaitaji tume kuja kuambiwa wavae barakoa,wanawe mikono na maji tiririka ,wakae social distance kweli? Maana hakuna jipya watakalokuja nalo zaidi ya porojo hizo

Dunia nzima inajua covid ipo. Tanzania tulisema Covid hakuna kwetu na mazingira tunavyoishi mtaani kama ingekuwepo kweli kila siku tungekuwa tunazika watu .

Waje na porojo zao but swala la lockdown na chanjo hatutaki ..maana chanjo imekuwa ni biashara kubwa na inampaka madalali na nina imani hata watu wa tume madalali wameshawafata

Naona kuna mtu anataka kufungua duka saa 2 usk wakat wenzie wanakaribia kufunga biashara .
Mechi ya Corona inakaribia kuisha mtu ndo anataka kuingiza timu uwanjani kucheza mchezo ambao wenzie wanakaribia kuumaliza.
Nilitarajia tume ije na majibu kwamba wamefanyia utafiti zile chanjo na wameona iliyobora kwa mzingira yetu ni astrazeneca au Johnson Johnson au nyingineyo katika zilizogunduliwa. Au watoe suggestions juu ya side effects zinazo ambatana na dawa hizo kama kuganda kwa damu kushindwa kupumua na vifo.
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:

a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Nchi ishapotea hii sasa.

Yaani imeishauri serikali itangaze uwepo wa corona?hii corona mbona inapaishwa sana saiv
 
... Rais na Mwenyekti wa Kamati kwenye makabidhiano ya ripoti (just two people) wamevaa barakoa halafu kapuku mwenzangu unajitoa ufahamu eti hakuna korona! Watch out!
Hii corona ndio imeshika kasi baada ya samia kua Rais au?
Mbona inapigiwa upatu sanaaa wkt mtaani watu washaisahau kama kuna hicho kitu
 
Ndo wameandika hayo mavitabu yote au wamekopi tu maandishi ya wengine na kuyakusanya na kuyaweka yaonekane kama mavitabu?

Halafu sidhani kama Samia atayasoma .

Sidhani kama ni mtu wa kusoma mavitabu kama hayo.

Yeye ni mitandao tu .
We Nyani ughaibuni acha dhihaka kwa Rais SASHA, kwamba yeye hawezi kusoma na kuchambua vitabu bali comments za kwenye mitandao? Duh!!!
 
Kaka hakuna anakuzuia kujielimisha.
1. Ndiyo, chanjo ni kinga. Si 100% lakini kama 80-90%. Imethibitishwa na wataalamu China, Afrika Kusini, Urusi, Uhindi, Marekani, Ulaya, Australia ...

2. Wewe huhitaji chanjo kama hutaki. Ila ukubali wengine wanafanya maazimio yao kwa hiyo usitegemee kuhiji Makka, kufanya biashara China, kusoma Ulaya au Marekani. Ni azimio lako. Pamoja na kutoingia katika nchi jirani zitakazoweka mashariti ya kuonyesha kadi ya chanjo wakati ujao.

3. Tatizo la Uhindi ni: A) hadi sasa walifikia asilimia ndogo mno wa watu wao, hata kama wamshapiga mamilioni lakini wako zaidi ya biloni. B) baada ya kupita vema awamu ya kwanza sisas yao ililegea. Waziri Mkuu Modi anatafuta kura za wafzasi wa Uhindi, hivyo hakutaka kutamka maonyo au kutangaza mashariti wakati wa sikuu kubwa ya Kinhidu ambako mamilioni walihiji na kuktana; pia walikuwa na kampeni za uchaguzi katika majimbo kadhaa bila mashariti yoyote kwenye miktano ya hadhara. Sasa wanavuna matokeo.

Katika yote nahofia Tanzania imeshapitiwa na wakati kupata chanjo karibuni. Nchi kadhaa zilichangia pesa ili Afrika ipate kiasi cha chanjo; akiba hii inakwisha sasa. Uhindi walipata mlipuko ho hivyo hao, ilhali ni watengenezaji wakuu wa madawa duniani, wamapiga marufuku kuuza dawa la chanjo nje ya Uhindi hadi waendelee kufikia watu wao wenyewe.
Mkuu hapa si kuwa hatuikubali chanjo, ila je tumeijiandaa na chanjo? Je Ni kwel tunahitaji kulitangazia taifa tunahitaji chanjo? Je mkuu unajua hw long chanjo huwa inakuwa examined?? Kwa nn hatujafkiria madhara yaliyopo?? Yaan tumewaza tu kwenda USA. Na ulaya ili tusitengwe na jamii ya kimataifa??

Mkuu unajua kuwa tz tuna kitu inaitwa herd immunity (Kama ntakuwa sijakosea)
Yaan kulingana na ugonjwa ulivokuja we did it and we made it... Tatzo tulipaswa kuwa na strong institute ambayo ingeweza kujendeleza Yale mazuri...

Mkuu hv unajua c19ipo ikulu na kwenye mikutano ya kisiasa, na dhifa za kitaifa hapo ndo unajua ahaaa kumbe cvd ipo bt kwenye jamii huku asee hicho kitu hakipo kabisa, tunaishi nao Kama vile HIV. Maralia. Au mafua.... Ila hatuna hlo janga...

Nw ndo wanataka kulileta wanaondoa kujiamini, wanaleta hofu na kuuwana ukwel Ni huuu.. MAMA aliua taifa kabisa.. ikiwa atafanya makosa ya kiufundi..
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:

a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Duuh R.I.P JOHN JOSEPH MAGUFULI.... huyu jamaa alikuwa ni gifted kwenye hili taifa aliweza kuona mbali sana!!!!
 
Matumizi mabaya ya kodi za wananchi tu taarifa gani watazitoa zaidi ya porojo tu hv watanzania wanaitaji tume kuja kuambiwa wavae barakoa,wanawe mikono na maji tiririka ,wakae social distance kweli? Maana hakuna jipya watakalokuja nalo zaidi ya porojo hizo

Dunia nzima inajua covid ipo. Tanzania tulisema Covid hakuna kwetu na mazingira tunavyoishi mtaani kama ingekuwepo kweli kila siku tungekuwa tunazika watu .

Waje na porojo zao but swala la lockdown na chanjo hatutaki ..maana chanjo imekuwa ni biashara kubwa na inampaka madalali na nina imani hata watu wa tume madalali wameshawafata

Naona kuna mtu anataka kufungua duka saa 2 usk wakat wenzie wanakaribia kufunga biashara .
Mechi ya Corona inakaribia kuisha mtu ndo anataka kuingiza timu uwanjani kucheza mchezo ambao wenzie wanakaribia kuumaliza.
Umeambiwa chanjo ni hiari na hakutakua na kufungiwa ndani hivyo hakuna haja na kua na wasiwasi
 
VP kwenye utafiti wenu mmeeleza maside effect ya hzo chanjo? au tunaende tunaenda tu? nmeona mmezungumzia umri wa watu wazma na kuna baadh ya chanzo zmezuiliwa kutolewa kwa watu wazma kuanzia miaka 60, kuna chanjo inasifa ya kugandisha damu, kuna chanjo baada ya kutumia wengne wanashndwa kusee cku zao, au mnaangalia matumbo yenu na matrilion ya madili hayo mnayoita ya msaada wakati mnafidiana kwa tanzanite? chanjo ni jambo jema ila mjiandae kwa mtafaruko utakao letwa na hao walala hoi endapo hio chanjo ikaleta negative effect.
 
Hayo Ni Copy and Paste Tu, Uongo na Ujinga Mwingi Ndani Ya Hayo Mavitabu
Well said, baada ya kupitia machapisho ya: WHO, NHS ya Uingereza na mapendekezo ya Serikali ya Merikani kuhusu njia ya kudhibiti ugonjwa wa COVID-19 ni wazi wenzetu wame borrow a leaf kutoka kwenye taasisi - tuombe Mungu wasije wakapendekeza kwamba Watanzania wachanjwe chanjo zinazo tokana na mRNA badala ya chanjo zinazo zalishwa kwa kutumia njia ya asili (attenuated covid virus) - au kama vipi basi waache Watanzania wachague aina/type ya chanjo kila mtu anayo taka adungwe baina ya chanjo za type ya mRNA zinazo zalishwa na makampuni ya magharibi ya madawa na chanjo au chanjo zinazo zalishwa kwa njia ya asili zinazo toka huko Uchina,Urusi pamoja na Cuba.
 
Taifa linakwenda kuanguka.. tulikuwa tumejizoea mfumo huu.. sasa malengo yao ya kuitia dunia hofu yamekamilika... Siku tu idadi ikianza kutangazwa nchi itaingia kwenye tahaharuki ya kudondoka mtu..

Ni kwel tunahitaji chanjo?? Au tunahitaji kuingia kwenye Muunganiko wa kuana?? Who knows after kinanachoitwa chanjo??

Kama ni Kinga kwel y India imepiga balaa?? Hiv kwel thinktank ya kamati ndo hayo tu mapendekezo? Au yalikuwa maelekezo? Mbona Kama yalijulikana before?? No anynews!!!

Anyway ngoja tutiane hofu ili malengo yafikiwe..
We umepigwa chanjo ngapi toka uko mdogo na uko hai mpaka leo? USA karibia nchi nzima wamepata chanjo,same hata UK na Mataifa yote ya ulaya. China, Russia na other big nations za Asia wame fanikiwa kutoa chanjo ya kutosha kwa watu wao. Huko kote wako kwenye mkakati wa kupunguza watu wao miaka michache ijayo kwa kutumia covid19 vaccine?
 
Wenye ndoto za kujilipua chanjo ikija fanya hima upate, Binafsi leo nimesherehekea report ya kamati.
Covid passport ni Kama ilivyokuwa kadi ya yellow fever, Huna chanjo hakuna Safari.

Wale wa dar, mbeya, Dodoma mnaweza endelea kukaa bila chanjo, Kamati imesema sio lazima.
 
Ucje ukakubal chanjo hii ngie mwilin mwako bila kujua uwakika wa utendaji kazi mwilin mwako, af kinacho nishangaza apa hao wanao chanja ndo wanakufa wengi kuliko sisi ambao bado hatujaanza kuchanja rate ya vifo ya tz na India vya covid havfanan af kule wana chanjo zao na za kutoka Uingereza , ndo kitu knanfanya nishindwe kuchanganyikiwa
 
Back
Top Bottom