#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Kwa tulioofika sasa maamuzi ya kutumia chanjo kwa mtu atayetaka ni lazima yawe hivyo la sivyo huko mbele ya safari mambo mengi hayatakwenda, hiyo chanjo ingeweza kukataliwa lakini nchi nyingine zote zimekubali chanjo ila zinaangalia iliyo salama hapo ndo tupiganie kupata kilichobora, maana kuna watu wanatoka nje ya nchi ni hilo ni hitaji la nchi zinazotembelewa pia kuna watu wanakuja kwenye nchi yetu kutoka nje wanakuwa wamechanjwa na chanjo nyingi zinakuwa ni huo ugonjwa ukiwa na kinga sasa hao watakao kuwa wamechanjwa ndo watakaotuambukiza sisi ambao hatujachanjwa hasa wenye kinga ndogo hivyo hii kujichanganya lazima hatua zichukuliwe na hiyo kutangaza takwimu ni sawa tu Ili wagonjwa wajulikane na wahudumiwe vizuri kuliko kujificha alafu mtu akiumwa hospitali zinamkataa maana hakuna maandalizi ya huduma hiyo mwisho mtu anakufa ghafla, pia vipimo viwe na gharama ya chini Ili huo ugonjwa uwe ni kitu cha kawaida Kama malaria watu wapimwe na wapate huduma na vifaaa vya kujikinga viwepo kwa gharama ndogo isiwe kibiashara.
 
Ukisoma ripoti nzima hakuna jipya na ni yale yale tunayoyasikia mataifa ya nje.Inaonekana hawakutumia ujuzi na akili zao wala kusikiliza maoni ya wananchi bali wamekopi na kubandika.
Hivi kamati haijasikia kwamba chanjo nyingi zina madhara na mataifa kadha wa kadha wanazirejesha kwao.
Na hawajasikia kuwa taifa lillochanjwa kwa zaidi ya asilimia 60 corona ndio kwanza inaongezeka.
Na kwamba sasa corona huko ilipo haichagui tena umri,mbona wao bado wanagwa makundi ya watoto na wazee.
Jamaa aliwaharibu sana vichwa vyenu!
 
Ni ajabu tunataka kwenda China ( Guanzhou) na ATCL na tunafurahia lakini tunashindwa kuelewa tunakoelekea hakuna nchi tutaingia kufanya kazi/biashara kama huna chanjo ya covid.
 
Kwa hiyo unataka chanjo kama wazungu. Tatizo lako unakopi na kutuletea unayaona mitandaoni na kuyasikia kupitia king'amuzi. Unavyoona kwa miaka miwili na zaidi ya kuishi na COVID-19 hali ni ngumua kiasi cha kuhitaji na kukubali madhara hayo ya chanjo? Madhara ya chanjo baada ya miaka 3, 5, 10 n.k. umeshayaelewa? Ni kweli hutambui chanjo zote zimepitishwa kwa mpango dharula kuokoa wanavyoteketea? Je sisi tunateketea? Kenya waliteketea? Burundi Uganda, Rwanda, majirani ...... wanateketea.

Tumieni akili bhana!
Una hisi hatuna akili kama wewe?
 
Twafaaaaaa jamani hao wazee wanaotaka chanjo wajichanje wenyewe watuache vijana manake wao wanataka kuharakia kufa sisi vijana watuache tuendeleze taifa manake nasikia chanjo mbeleni huko miaka 30 hivi ijayo genes zetu zinaweza badilika chanjo ni mbaya wazungu wenyewe hawaitaki
 
Uko lndia ambao ni watengenezaji wakubwa wa chanjo, unaona wamepotea wangapi kwa siku? Wewe ni njinga kama wajinga wengine haujui dunia inavyoenda.Ngoja takwimu kuhusu corona zianze kutoka,ili mfungiwe ndani kama kuku ndio utajua, maana Samia ndicho anachokitafuta

Tume ya mama imekuja na majibu kama ambayo tumekuwa tunayapigia kelele muda wote. Labda kama tume ya mama ni ya wajinga.

India kuna watu 1.3bn hao wanaokufa kwa siku ni % ngapi? Una uhakika gani % ya Tanzania leo kama ni ndogo au kubwa kuliko hiyo?

Kwa nini mnadhani mnajua hali hakuna mjualo?

Tutafuata maelekezo ya tume ya mama. Sasa kazi tu! Wajinga wajinga wote hata kwa kiboko mtanyoroka tu.
 
Ukisoma ripoti nzima hakuna jipya na ni yale yale tunayoyasikia mataifa ya nje.Inaonekana hawakutumia ujuzi na akili zao wala kusikiliza maoni ya wananchi bali wamekopi na kubandika.
Hivi kamati haijasikia kwamba chanjo nyingi zina madhara na mataifa kadha wa kadha wanazirejesha kwao.
Na hawajasikia kuwa taifa lillochanjwa kwa zaidi ya asilimia 60 corona ndio kwanza inaongezeka.
Na kwamba sasa corona huko ilipo haichagui tena umri,mbona wao bado wanagwa makundi ya watoto na wazee.
Ebu tupe jina la ilo taifa ambalo wamechanja 60% lakini maambukizi yanapanda ,please kaka tupe jina ikiwezekana weka link kuhusiana na hiyo namba.
 
Twafaaaaaa jamani hao wazee wanaotaka chanjo wajichanje wenyewe watuache vijana manake wao wanataka kuharakia kufa sisi vijana watuache tuendeleze taifa manake nasikia chanjo mbeleni huko miaka 30 hivi ijayo genes zetu zinaweza badilika chanjo ni mbaya wazungu wenyewe hawaitaki
Unajuaje hawataki? Mimi naona picha hizi za watu wanaosubiri kwenye foleni kupigwa chanjo...
1621267735768.png

Berlin, Ujerumani terehe 16 Mei
1621267769053.png

Hamburg, Ujerumani, tarehe 15 Mei
1621268121449.png

Uingereza, juzi hivi
 
Huyo ndio kiongozi wa Kweli, maana ya kiongozi ni kujitoa kwa ajili ya watu wako,hata kama itakugalimu maisha yako,sio huyu takataka kazi ni kujipamba na kupaka lipstick tu, unafikiri anatafuta umiss Tanzania
Wewe ulishakua kiongozi wapi,au ujuaji tu wakijinga hapo ulipo utakuta ata familia yako tu inakushinda.
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788475

Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:


a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Naunga mkono hoja kwamba ni upotezaji wa rasilimali za nchi kwa kuja na matokeo ambayo yangepatikana kutokana na dodoso kujibiwa na watalaamu bila kutumia gharama bila tija yoyote ile kisa wanataka kufurahisha jamii ya kimataifa.

Usanii uliotukuka kwa kuwa hakuna hitimisho maana inaelekeza viongozi wa dini waendelee kushirikishwa na dawa mbadala ziendelee kufanyiwa uchunguzi wa kisayansi. Maajabu
 
Kwa hiyo unataka chanjo kama wazungu. Tatizo lako unakopi na kutuletea unayaona mitandaoni na kuyasikia kupitia king'amuzi. Unavyoona kwa miaka miwili na zaidi ya kuishi na COVID-19 hali ni ngumua kiasi cha kuhitaji na kukubali madhara hayo ya chanjo? Madhara ya chanjo baada ya miaka 3, 5, 10 n.k. umeshayaelewa? Ni kweli hutambui chanjo zote zimepitishwa kwa mpango dharula kuokoa wanavyoteketea? Je sisi tunateketea? Kenya waliteketea? Burundi Uganda, Rwanda, majirani ...... wanateketea.

Tumieni akili bhana!
Taifa linakwenda kuanguka.. tulikuwa tumejizoea mfumo huu.. sasa malengo yao ya kuitia dunia hofu yamekamilika... Siku tu idadi ikianza kutangazwa nchi itaingia kwenye tahaharuki ya kudondoka mtu..

Ni kwel tunahitaji chanjo?? Au tunahitaji kuingia kwenye Muunganiko wa kuana?? Who knows after kinanachoitwa chanjo??

Kama ni Kinga kwel y India imepiga balaa?? Hiv kwel thinktank ya kamati ndo hayo tu mapendekezo? Au yalikuwa maelekezo? Mbona Kama yalijulikana before?? No anynews!!!

Anyway ngoja tutiane hofu ili malengo yafikiwe..
 
Taifa linakwenda kuanguka.. tulikuwa tumejizoea mfumo huu.. sasa malengo yao ya kuitia dunia hofu yamekamilika... Siku tu idadi ikianza kutangazwa nchi itaingia kwenye tahaharuki ya kudondoka mtu..

Ni kwel tunahitaji chanjo?? Au tunahitaji kuingia kwenye Muunganiko wa kuana?? Who knows after kinanachoitwa chanjo??

Kama ni Kinga kwel y India imepiga balaa?? Hiv kwel thinktank ya kamati ndo hayo tu mapendekezo? Au yalikuwa maelekezo? Mbona Kama yalijulikana before?? No anynews!!!

Anyway ngoja tutiane hofu ili malengo yafikiwe
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom